Mbunge Tarimba apendekeza TANESCO kufumuliwa na kuwepo kampuni 3 kwa ajili ya Uzalishaji, Usafirishaji na Ugawaji umeme

TANESCO ndiko wakubwa wanakopigia pesa
 
TANESCO wakubwa wanapigia pesa
 
Hivi mbona enzi za Mwendazake is like matatizo ya umeme yalikua ni kama yameisha? What is wrong now??? Tunataka kujisahaulisha hata kwa jambo ambalo hata mwaka halijamaliza? Shida ya Tanesco sio hi ambayo bwana mbunge wa Kinondoni anataka tuijue, tatizo la umeme Tanesco linaeleweka, mwendazake aliisha twambia. BAdo najiuliza, hi akili ya Watanzania kusahau vitu kwa muda mfupi namna hi inatokana na nini yaani?
 
Kwanini hiyo budget isiongezwe kwa Tanesco ya sasa? Kwanini rasilimali watu, technology na miundombinu isiongezwe kwa Tanesco ya sasa. Kwanini Tanesco ya sasa isiwajibike kwa umma na hiyo iltakayogawanywa ndio iwajibike?
 
Kwanini hiyo budget isiongezwe kwa Tanesco ya sasa? Kwanini rasilimali watu, technology na miundombinu isiongezwe kwa Tanesco ya sasa. Kwanini Tanesco ya sasa isiwajibike kwa umma na hiyo iltakayogawanywa ndio iwajibike?
Mkuu, nadhani nitachoka kulielezea hilo.
Nimeshasema uzi mzima huu kwamba kuna options mbili, moja kuliongezea uwezo likiwa moja hivyo hivyo, au kuligawa na kuliongezea uwezo.

Nimeshatoa ufafanuzi kwenye comments zangu za juu.

Hapa pia nilikua najaribu tu kutetea uhuru wa maoni ya Tarimba kwamba yeye anaona approach ya kuligawa ni bora zaidi.
Cha ajabu ni sisi "watanzania wenzake" tunaona kama kaleta wazo la ajabu, geni na ambalo halijawahi kutokea duniani.
Haiwezekani watanzania wote milioni 60 tukawa na mawazo yanayofanana. Suala la kugawa taasisi ili kuongeza tija na ufanisi sio geni, mifano iko mingi.

Bottom line ni kwamba TANESCO inatakiwa kuboreshwa, whatever the means.
 
Moja imewashinda tatu mtaweza?

TANESCO walipaswa wapate mshindani mmoja tu kutoka nje ya nchi awafunze adabu.

Wangeoneshwa namna ya kutoa huduma sio ujinga walionao sasa.
Hii kwangu ndio comment bora zaidi.
 
Nimekuelewa vyema mkuu japo hujanijibu mimi, nimesoma pia comments zako toka huko juu.

Sasa mm najiuliza swali moja tu, TANESCO anafeli wapi kuajiri watu, fedha za miradi kujiendesha ktk miundombinu, Uzalishaji n.k ikiwa yeye ndo muuzaji mkubwa wa umeme Tanzania?

Mbona mimi naona hakuna shirika ambalo linapaswa kuingiza fedha nyingi hapa Tanzania kuliko Tanesco?

Naomba kueleweshwa wana JF.
 
Nishati sio Kitu cha Kuchezea kabisa, Tanesco iendele kuwa State Owned Entity kwa Masilahi mapana ya Nchi, Katika Vitu nyeti Nchi hii ambayo si vya kuchezea ni Nishati acheni masihala wazee
Dadavua kama hautajali.
 
Thinking ya Tarimba iko chini sana sidhani kama huyu jamaa hata fomfoo alimaliza , ndio wale wale tu umeme unakatika kinavunjwa kitengo cha Mawasiliano. Mkiambiwa muwe mnachagua watu angalau wanaojitambua mnakua wabishiiiiii, haya ndio matatizo yake sasa, huyui akacheze tu mamichezo yake ya kubeti kule sportspesa hana anachojua zaidi
 

Nimekuelewa...
 
Shirika linahitaji maboresho makubwa zaidi kuliko hao "mtu mmoja mmoja" hapo juu.

Management effective inahitaji kiongozi mahiri!! Kuongoza ni kuonesha njia kwa wale unaowaongoza. ! I do not see that in the current TANESCO line up!
 
Sijui unapata wapi ujasiri wa kumuuliza mwingine kwanini ana maoni X na sio maoni Y.

Nakuuliza kwasababu wewe ndio umeweka hizo options mbili na hujajenga hoja ya kuonesha ipi ndio chaguo lako!!! Unasema tu Kuwa inahitajika kuboresha technology inayotakiwa kuboresha shirika na ndio hapo unauluzwa kuwa hayo maboresho yanafanya kazi kwa kuivunja Tanesco tu? Jibu hoja iliyo mezani kwanini tuvunje shirika na kuwauzia wahuni!!

Mliuza TTCL mkapata 10% yenu; halafu mtawala mwingine akaja akalinunua shirika lile lile kutoka kwa mliemuuzia kwa bei kubwa! Huo ni ujinga usio kipimo na inawezekana Tanzania tu!!! Halafu yule yule aliyekiwa dalali wa kuiiuza TTCL ndio mnamfanya Mwenyekiti wa TANESCo ; mnataka tuwaeleweje? Hili sio Taifa la watu wote walio wapumbavu!
 
Nadhani tuishie hapa. Maana tumeanza kulishana maneno sasa, sikumbuki wapi nimesema tuwauzie hao uliowaita wahuni.
Uwe na siku njema.
 
Nishati sio Kitu cha Kuchezea kabisa, Tanesco iendele kuwa State Owned Entity kwa Masilahi mapana ya Nchi, Katika Vitu nyeti Nchi hii ambayo si vya kuchezea ni Nishati acheni masihala wazee
Hilo hatujakataa ila ili kuongeza ufanisi inabidi tanesco baadhi ya sekta wawaachie kampuni binafsi kwa muongozo maaalum

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…