Kwa Kanisa Katoliki kikwazo pekee, ambacho kwa kweli hakitenguliwi isipokuwa kwa kifo, ni kuwa na ndoa nyingine. Kama aliwahi kufunga ndoa na mmojawapo wa hao wanaume watatu (au mwingine yeyote) na mwenzake angali hai, na Kanisa likajulishwa, hapo ameula wa chuya. The best kwake ni kubadili dini ili aweze kufikia matarajio yake ya kuolewa tena.
Ila hao wanaume nao ni washenzi, kwani kuzaa na mwanamke ndio iwe sababu ya kumuwekea pingamizi? Huu ni ujinga uliopitwa na wakati. Hakuna sababu ya kumharibia dada wa watu maisha simply kwa kuwa umezaa naye au umemjengea nyumba au kumnunulia magari.
Naye huyo Vicky ana matatizo. Kwanza kuzaazaa ovyo (watoto wa3!); huyu maadili yake ni machafu. Wanasema kosa sio kosa bali kulirudia. Pili, kama alishafanya kosa mbwembwe zote hizo za nini? Eti harusi ya m.96, so what? Siku hizi hata Ulaya na Marekani wenye hela zao na umaarufu wa kupindukia hawafanyi mbwembwe za kijinga hivyo. Issues zinafanywa kimya kimya bila kustua waliolala. Eti ana mimba ndio inayomletea matatizo! Misifa mingine ya kijinga, mimba kaanza kuwa nayo yeye?