Mbunge wa Gairo, Shabiby ataka fedha za bima kwa wote zikatwe kwenye laini za simu

Nilitaraji ataitaka serikali ijibane na pia iwabane wote waliofisidi michango ya bima na kusababisha kadhia hii.
 
Shabiby nakwambia haya maoni Yako yakipitishwa utalipia line zangu. Ninazo mbili... Wewe kweli wa kitugeuka sisi Ili tukamuliwe... Nimesikitika sana
Kila mbunge angetoa nusu ya mapato wanayovuna wakiwa usingizini...... Wangestahili wapate milioni 5 na the rest zikatumike bima ya afya !!
 
Ni pendekezo la hovyo sana...

1. 2,000 kwa kila mwenye simu its a regressive tax..
2. Simu si kipato au asset, wengi ni kiwezeshi cha mawasiliano. kuanza kukiona kuwa ni mtaji na asset ni uduni wa mawazo.
3. lazima ifanyike study kubwa in the formal na informal sectors na kuainisha kipato kwa kila mmoja katika hizo sector then kuweka kiwango ambacho ni progressive kadiri ya kipato
4. Tusirudie kosa la kodi uzalendo wa sh 1,000 kila mwezi, matozo ukituma na ukipokea muamala etc... na hatuwahi kupata hesabu kamili ya kipato kile kiukaguzi...

Bima ya Afya kwa wote si jambo la kukurupuka..

Wapo wanaokatwa hadi laki 2 kwa mwezi na sasa dawa na huduma nyingi hatupati au tutatoa pesa mfukoni..
 
Dah! Hayo maombi yako ni haramu mbele za MUNGU
 

Hakika hili suala la bima kwa wote linahitaji akili kubwa maana regressive tax huwa ni mzigo mzito kwa wenye kipato duni au wasio na kipato na kingine kwa ufanisi upi serikali inaweza simamia hayo makusanyo maana kama hapo awali pesa zimechotwa kwenye mfuko (NHIF) na hazilipwa mpaka leo. Kwanini wasije na mpango wa kupunguza matumizi ya wabunge kama posho, mishahara yao, mafao kwa wake za viongozi, manunuzi ya magari ya kifahari kila mwaka, kudhibiti mianya ya ufisadi ripoti za CAG zinabainisha ufisadi kila mwaka, kuacha safari zisizo na ulazima kwa viongozi hasa nje ya nchi nk. Waache kufikiria mambo rahisi kwa mambo tata kama bima kwa wote
 
Idea NI nzuri, Ila rekodi ya usimamiz na matumiz ya pesa za watu ndo mbaya Sana, kuamini CCM NI dalili nyingine ya tatizo la kufikiri na akiri finyu...TUTAFIKA hatua tutaanza kumshambulia MTU binafs badala ya mfumo ili kuondoa generalisation. Shabib kuwa bungeni NI matumiz mabaya ya Bunge, aende kwenye biashara zake apambane na kile wafanyabashara walioko nje ya Bunge kadhia wanazopata .
Asome Sera ya JOE BIDEN kuhusu BIMA ya afya na nia aliyokuwa nayo OBAMA..
 

Attachments

  • FB_IMG_1712248285243.jpg
    77.3 KB · Views: 2
Kukurupuka ndo huku tozo (Mwigulu) ziliishia wapi hata kiasi kilichokuwa kikikusanywa hakijulikani
Kuna uwezekano hawa mawaziri kila wiki wana mgao wa pesa kila mmoja si chini ya milioni 10 kwa kila wiki.
Maana pesa ni nyingi sana na wenye pesa wananchi wanezubaa
 
Wanashindwa kujipunguzia pesa za anasa wanazopata, magari ya gharama wanayotumia wao wabunge, mawaziri na manaibu wao, wakuu wa mikoa na wilaya, wakurugenzi nk wanalipana mishahara minono, posho na kusukuma ndinga za maana bila haja yoyote.

Wapunguze huko mbona hiyo bima inawezekana tu.
 
Kwa staili hii naona huduma ya Posta ya kusafirisha barua ikiimarika kadri siku zinavyosogea!!!
 
Safi sana safi sana mh mbuge wetu hakika umewakilisha mawazo yetu huku jimboni,hiyo elfu 2000 ni ndogo sana ukizingatia uchumi wa mtu mmoja mmoja umeongezeka.Tukatwe elfu 10 TU alafu nyie wawakilishi wetu kwasababu mnakazi ngumu ya kulipigania taifa msikatwe hata 100.
 
Safi sana safi sana mh mbuge wetu hakika umewakilisha mawazo yetu huku jimboni,hiyo elfu 2000 ni ndogo sana ukizingatia uchumi wa mtu mmoja mmoja umeongezeka.Tukatwe elfu 10 TU alafu nyie wawakilishi kwasababu mnakazi ngumu ya kulipigania taifa msikatwe hata 100.
 
Hayo ndio mawazo ya watu wenye akili nzuri !
Sio hoja kuwa na madigirii mengi kwenye makaratasi halafu kichwani ni peupe inakuwa ni Kazi bure !

Naunga mkono wazo la Shabiby !
Jamaa yupo vizuri !
 
Na vipi Hela wanazojikopesha, na hazirudi kukopi mambo ya Korea kusini TAIFA ambalo liko mile 1000000000 zaidi yetu Kwa Kila kitu ni uzwazwa
Umeme tu shida hyo mifumo SI ndo itadukuliwa umeme ukiwa umezima na kuchota Hela zote, naona kama Mzee wa SKAFU SHINGONI ANATIKISA KALAMU NJISI SHA-BABY ALIVYOMUKOSHA NA DILI JINGINE BAADA YA TOZO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…