Mbunge wa Geita Mjini anatia mashaka. Anataka kusema Musukuma ni muongo?

Mbunge wa Geita Mjini anatia mashaka. Anataka kusema Musukuma ni muongo?

Tusiwalaumu sana hawa madiwani waliopitisha, sifa ya kuwa diwani au mbunge ni k mbili tu, kujua kusoma na kuandika. Ni wakati muafaka kwa chama changu pamoja na vyama vingine vidogo vidogo, kulitazama upya hili japo tuongeze wagombea wajue kusoma, kuandika na uwezo wa kufanya tathmini kwa walichoandika na kusoma. Hili lita saidia maamzi kama haya ya kununua gari ml 400 kwa ajili ya Kiongozi yasiwepo.
 
Msukuma ni mbunge mpumbavu, anachonganisha watu! Yeye ni nani mpaka akadandie hoja za Geita mji wakati yeye yuko vijijini? Ina maana Mh. Kanyasu hana uwezo wa kusimamia matumizi ya fedha za umma kwenye jimbo lake mpaka apate msaada kutoka kwa Msukuma? Kwa ufupi Msukuma anatafuta sifa za kijingaaaa!
Ni mjumbe wa baraza la madiwani la halmashuri ya Geita.
 
Mbunge wa Geita mjini ni Kanyasu huyo Msukuma anajitia kimbelembele tu. Wala haingii kwenye vikao vya Halmaahauri ya Geita mji. Kwa hiyo Kanyasu asikaumiwe maana yeye ndiyo mwenye Jimbo hilo.
Sio kweli,wote ni wajumbe wa halmashauri ya Geita.
 
Mbunge wa Geita mjini ni Kanyasu huyo Msukuma anajitia kimbelembele tu. Wala haingii kwenye vikao vya Halmaahauri ya Geita mji. Kwa hiyo Kanyasu asikaumiwe maana yeye ndiyo mwenye Jimbo hilo.
Ukiona mambo hayaendi sawa kwa maslahi mapana ya umma,,hupaswi kunyamaza,,ni jukumu la kila mzalendo kufichua uozo
 
Yeye si ni mjumbe kule halmashauri ya wilaya? Kwa maana ya Geita vijijini na siyo halmashauri ya mji ambayo inaundwa na jimbo la Geita mjini!
Geita vijijini sio wilaya ni jimbo la uchaguzi,mpaka sasa halmshauri ni moja tu
 
Wivu upo wapi hapa? Kubwa jinga usie na akili.
Unaweza kuwa wewe - hutaki mbunge aeleze hisia zake dhidi ya DED wake - hutaki kuelewa kuwa DED hakutoa fedha mfukoni na kununua gari isipokuwa vikao vilika na kubariki

RAS alibariki
TAMISEMI ilibariki, kisha
Wizara ya ujenzi ikabariki - sasa hapo wewe unawashwa nini?
 
Geita vijijini sio wilaya ni jimbo la uchaguzi,mpaka sasa halmshauri ni moja tu
Hapana mkuu utakuwa huna taarifa sahihi. Jimbo la Geita vijijini linaunda halmashauri ya wilaya ya Geita na makao makuu yako kwenye kijiji cha Nzera. Majengo yako tayari na Watumishi walishahamia ingawa walikuwa wabishi wabishi! Hivyo Msukuma anasumbuliwa na kukosa fungu la 10! Hiyo ni halmashauri ya Mh. Kanyasu!
 
Msukuma ni mbunge mpumbavu, anachonganisha watu! Yeye ni nani mpaka akadandie hoja za Geita mji wakati yeye yuko vijijini? Ina maana Mh. Kanyasu hana uwezo wa kusimamia matumizi ya fedha za umma kwenye jimbo lake mpaka apate msaada kutoka kwa Msukuma? Kwa ufupi Msukuma anatafuta sifa za kijingaaaa!
Kwani kuna mkurugenzi wa Geita vijijini?
 
Nimemsikiliza mbunge wa Geita mjini ndugu Costantine Kanyasu kwa kweli anashangaza sana. Nini kimemfanya akurupuke kuanza kutoa maoni kama haya kabla ya uchunguzi?

Nilimsikiliza waziri Jaffo alipopewa kazi yake ya kwanza kuunda tume kuchunguza ubadhilifu halimashauri ya Geita,alisema pesa mil 400 zilizotumika hazikupitishwa na baraza la madiwani.

Nashangaa nimemsikiliza mbunge wa Geita anaongea na media na kudai kuwa amepitia document hapo halmashauri na amebaini kuwa pesa hizo zilipitishwa na baraza la madiwani,pia anasisitiza Gpsa walitumiwa kununua hilo gari la mil 400,kwa hiyo taratibu zote zilifuatwa maana Gpsa ndie wakala wa manunuzi wa serikali.

Mbali na hayo anasema mkurugenzi aliyesimamishwa ni muadilifu na amekuwa akipambana na ufisadi kwa muda mrefu. Je ina maana Mbunge wa Geita vijijini ni muongo? Anaropoka hovyo na kumdanganya rais,maana huyu ndie aliyemlipua mkurugenzi kuwa alifanya ubadhirifu wa mil 400.
Mbona huyo Msukuma alisema kuwa budget ya hayo manunuzi ilipitishwa na madiwani ila walipitisha wakiwa kwenye stress za kuelekea uchaguzi mkuu.
 
Wivu upo wapi hapa? Kubwa jinga usie na akili.
Kwenye huu mjadala twendeni tu taratibu mkuu tusitukanane,, mimi niko upande wa DED na Mh. Kanyasu. DED hawezi kujiamulia mambo makubwa hivyo bila baraka za Full council, RAS, PM n.k ila hao wote kwa kumwogopa Magu... hawatafunua makopo yao kumtetea DED. Wamrudishe kazini aisee!
 
Inawezekana taratibu zilifutwa tu Kama mfumo,lakini nyuma ya pazia lilikua chezo,Sasa limegundulika!!
Taratibu za kununua gari ya mkurugenzi yenye thamani ya sh mil 400? Kweli hii nchi ina wenyewe. Bila kujali kama taratibu zilifuatwa au la, lakini kitendo tu cha mkurugenzi anayeongoza halmashauri yenye wakazi mafukara wa nchi ya dunia ya tatu kununua gari la kutembelea tu la sh mil. 400 kinaonyesha huyo mkurugenzi ni fisadi na hafai kuwa kiongozi.
 
Baraza la madiwani ndio linapaswa kumuelekeza mkurugenzi mahitaji ya halmashauri. Kama madawati,zahanati madarasa yanahitajika walipaswa wasipitishe pesa za kununua gari.
Kwa mujibu wa marlezo ya rais alishangaa kwanini wanakimbilia kununua gari wakati hakuna madawati ya kutosha
 
Unaweza kuwa wewe - hutaki mbunge aeleze hisia zake dhidi ya DED wake - hutaki kuelewa kuwa DED hakutoa fedha mfukoni na kununua gari isipokuwa vikao vilika na kubariki

RAS alibariki
TAMISEMI ilibariki, kisha
Wizara ya ujenzi ikabariki - sasa hapo wewe unawashwa nini?
Huna akili wewe fala,wewe ni nani mpaka unipangie nini cha kupost? Kama vikao vilikaa na hao uliowataja kubariki ndio tusijadili kilichotokea.
 
Back
Top Bottom