Echolima1
JF-Expert Member
- Nov 2, 2019
- 9,662
- 8,023
Mbunge wa Irani anaishutumu Israel kwa mlipuko katika bandari ya Bandar Abbas na kufichua maelezo mapya kuhusu kilichotokea jana:
Mohammad Saraj, Mbunge wa Irani, kwenye mlipuko kwenye bandari ya Bandar Abbas:
"Mlipuko katika bandari ya Bandar Abbas haukuwa wa bahati mbaya. Kuna dalili za wazi za kuhusika kwa Israel.
Milipuko hiyo ilitokea kwa wakati mmoja katika maeneo manne tofauti, ikionyesha kuwa vilipuzi vilitegwa ndani ya makontena hayo.
Kemikali huwaka katika sehemu moja na haisababishi milipuko mingi kwa wakati mmoja katika maeneo tofauti.
Makontena hayo 'yalichezewa' ama katika nchi yalikotoka wakati wa usafiri, au na mawakala wa ndani nchini Iran.
Huenda milipuko hiyo ilisababishwa/kuteguliwa na satelaiti au vipima muda(Timer) zilizowekwa kwenye makontena na kusababisha uharibifu mkubwa zaidi wakati yalipowasili bandarini." Kulingana na vyombo vya habari vya Iran, idadi ya waliofariki kutokana na mlipuko katika bandari ya Bandar Abbas imeongezeka hadi 40, na idadi ya waliojeruhiwa imeongezeka hadi 1,205. Moto bado unawaka bandarini, siku moja na nusu baada ya mlipuko huo.