Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa changamoto hiyo kwa muda mrefu iliyoathiri utoaji wa matibabu kwa wagonjwa na wahudumu kushindwa kuhudumia vizuri.
Akizungumza wakati wa kukagua ukamilishwaji wa kazi ya kurekebisha mfumo wa maji katika kituo hicho, Mhe. Mbunge Mecktridis amesema kuwa kituo hiki cha afya kinafanya kazi kubwa ya kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa walio wengi wa Kata hii ya Itete, hivyo ukosefu wa maji katika Kituo hiki ni changamoto inyotishia na inayoathiri shughuli nzima za uuguzi kwa wagonjwa wanaokuja katika Kituo hiki.
Ameongeza kwa kumpongeza Mhe. Diwani wa Kata ya Itete Dr...Saulo kwa kuibua changamoto hii ya ukosefu wa maji katika kituo chicho na kuifikisha katika ofisi ya Mbunge kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi wa changamoto hii iliyodumu kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Daktari Kiongozi wa Kituo cha Afya Itete Dkt. Yusuf Nesta Mgeta amemshukuru Mhe. Mbunge kwa mchango wake wa thamani kwetu kwa kukikumbuka kituo hiki na kusaidia katika kuboresha mazingira ya utoaji tiba kwa wagonjwa.
"Kwa kweli shida ya maji ilikuwa kubwa na iliathiri sana utoaji wa matibabu kwa wagonjwa, baadhi ya Idara zilikuwa zikipata wakati mgumu kutokana na uhaba wa maji," amesema Dkt. Mgeta.
"Kwa sasa maji katika kituo chetu yapo ya kutosha na huduma zinatolewa vizuri kabisa, tunamshukuru sana Mhe. Mbunge," ameeleza Dkt. Yusuf.
Ameongeza pia kuwa ilikuwa shida sana hata kufua nguo za wagonjwa wetu tukija maana maji hakuna, lakini kwa sasa maji yamesaidia sana kuboresha huduma nyingi.