Elections 2015 Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (CHADEMA), ajiuzulu na kuhamia CCM

Elections 2015 Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (CHADEMA), ajiuzulu na kuhamia CCM

Siasa bana..
Mbunge / anahama chama kwa madai kwamba wabunge wa upinzani wanalazimishwa kupinga bajeti na wakifanya vingine wanaonekana wasaliti alafu unahamia chama ambacho wabunge wanalazimishwa kupitisha bajeti na wakifanya vingine wanaonekana wasaliti vilevile
Maajabu haya utayakuta Tz tu!!
 
Huko nape kila siku anaisema serekali na bado haitwi msaliti kikubwa chadema wanatakiwa watafute chanzo cha tatizo

Chanzo cha Tatizo ni Mikakati ya CCM Kutawala Milele ,hizo sababu nyingine hazipo ni kisingizio tu.
 
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Mkoa wa Arusha zinasema Mbunge wa Jimbo la Monduli Juliasi Kalanga kuhamia CCM kesho majira ya saa nne asubuhi.

======

UPDATES; 00:15HRS
View attachment 823188
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Monduli kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Mhe. Julius Kalanga amejiuzulu na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM muda huu kwa kile alichoeleza kuwa ni kuunga mkono juhudi rais Magufuli. Amepokelewa na katibu mwenezi wa CCM ndugu Humphrey Polepole.

Siasa za uhasama, malumbano na chuki zimeniondoa CHADEMA. Nimeamua kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwa maslahi ya taifa... Kwa sababu huwezi kufanya hivyo ukiwa upande wa pili, lazima utaonekana msaliti tu... Wana Monduli naombeni mnielewe, nitakuja kuzungunza nanyi," Julius Kalanga Laizer, aliyekuwa Mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CHADEMA.

Julius Kalanga aliwahi kuwa diwani kupitia CCM, kabla ya kuhamia Chadema 2015
Wala c kweli ni kununuliwa na kurudishwa bungeni kwa nguvu lkn iko siku watajua nn maana yake ni sawa na mtu akiua nafsi yake humsuta mpaka mauti na wala hao c wapinzani bali wapinzani ni wale wapga Kula ila kwakuwa wameahdiwa iwe isiwe watarudishwa bungeni iwe kwa vyovyote vile lkn iko siku watajua nn maana yake.
 
Kama hawa bora wandetu maana hata bungeni sikuwai kumsikia
Siku wakihama hawa
(1) mboe
(2)Lisu
(3) heche
(4) msigwa
(5)Sugu
(6)selasini
(7)Lema
(8) mdee
(9)Silinde
(10)Nasari
Kati yahawa akihama mmoja wao hata mm nitahama .
 
Chadema ifanye kama mbeya, taarifa zikivuja tu jamaa anataka kuhama unafukuza mapema ili asipate umaarufu wa kisiasa. Huku kumwacha mtu hadi anaita waandishi wa habari ni kumpa mtu kiki. Labda kama wanafanya kusudi
Hakuna sababu ya kushindana na wajinga hawaondoki chadema bahati mbaya.huu ni mchezo mchafu wa ccm.
 
Kweli hii ni Karne ya 21 miongoni mwa makabila yenye watu walio na misimamo isiyo yumba ni wamasai na wakulyaa lakini kinacho tokea kina waondolea heshima yao ya miaka mingi
Wamasai unawajua? Wanafiki kama wabena
 
Usije ukamuamini mwanasiasa hata siku moja yani hata kama akikwambia usiku mwema we toka nje kahakikishe kama kweli kuna giza
 
*BREAKING NEWS.*

Tarehe 30 Julai 2018

*CCM IMEFAGIA UPINZANI KWA LOWASSA*

Bwana Julius Kalanga Laizer Mbunge wa Jimbo la Monduli kupitia Chadema, leo amejivua uanachama wa Chadema, amejiuzulu nafasi yake ya Ubunge na vyeo vyake vyote ndani ya Chadema na Kujiunga na CCM.

Bwana Julius Kalanga Laizer amepokelewa na Kamaradi Humphrey Polepole Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.

Imetolewa na,

*IDARA YA ITIKADI NA UENEZI*
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM
 
Ndio sababu najiuliza mkuu,inawezekana kuna kitu wamefanyiwa,kuna nguvu nyuma ya kuhama kwao.

Ulishawahi kuona mtu anaambiwa fanya jambo fulani,kama hutaki nakuharibia.

Sio akili ya kawaida hii.

Ni kitu gani hicho Mkuu na ni kwa nini wawe na Uoga namna hiyo ?..Au hawakuwa wasafi wanaogopa kuharibiwa Biashara zao ?
 
Yanayoendelea sasa HV bongo,nayafananisha na matukio katika filamu ya COLONY,ambapo kuna viumbe viliivamia dunia(USA),vikaweka utawala wao,wale ambao walishirikiana navyo kutawala,wakawa salama,waliopingana navyo wakakiona cha mtema kuni,kupotezwa/kupelekwa kwenye forced labour,nk,
Sasa HV bongo ni kama vile imeingiliwa na roho Fulani,ukienda kinyume,unatwangwa,(Tundu lissu,Saanane,Mwandishi wa Mwananchi),na ukikubaliana nao,mambo yako yanakunyookea,mfano wabunge wanaojiuzuru na kujiunga CCM,
 
Tatizo sababu wanazozitoa kwa kuhama kwao huwa hazina mashiko yoyote yale na badala yake zinawavua nguo na kuonesha ni kwa vipi hawawezi kutumia baraka waliyopewa na Mwenyezi Mungu za kuwa binadamu badala ya Ng'ombe!!
.....wakirudi huku wanaitwa ng'ombe waliokatwa mkia ! Isikuumize kichwa saana.
 
Back
Top Bottom