Elections 2015 Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (CHADEMA), ajiuzulu na kuhamia CCM

Elections 2015 Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (CHADEMA), ajiuzulu na kuhamia CCM

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Mkoa wa Arusha zinasema Mbunge wa Jimbo la Monduli Juliasi Kalanga kuhamia CCM kesho majira ya saa nne asubuhi.

======

UPDATES; 00:15HRS
View attachment 823188
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Monduli kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Mhe. Julius Kalanga amejiuzulu na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM muda huu kwa kile alichoeleza kuwa ni kuunga mkono juhudi rais Magufuli. Amepokelewa na katibu mwenezi wa CCM ndugu Humphrey Polepole.

Siasa za uhasama, malumbano na chuki zimeniondoa CHADEMA. Nimeamua kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwa maslahi ya taifa... Kwa sababu huwezi kufanya hivyo ukiwa upande wa pili, lazima utaonekana msaliti tu... Wana Monduli naombeni mnielewe, nitakuja kuzungunza nanyi," Julius Kalanga Laizer, aliyekuwa Mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CHADEMA.

Julius Kalanga aliwahi kuwa diwani kupitia CCM, kabla ya kuhamia Chadema 2015
Human beings by nature are selfish or egoistic and if left free to pursue their will they can use all resources at their disposal to satisfy their egoistic tendencies to the point that the world can be become the most unpleasant place to live. Let it be a special duty for all of us to dissolve our animal nature and transmute it into divine nature- the ultimate goal of creation.
 
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Mkoa wa Arusha zinasema Mbunge wa Jimbo la Monduli Juliasi Kalanga kuhamia CCM kesho majira ya saa nne asubuhi.

======

UPDATES; 00:15HRS
View attachment 823188
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Monduli kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Mhe. Julius Kalanga amejiuzulu na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM muda huu kwa kile alichoeleza kuwa ni kuunga mkono juhudi rais Magufuli. Amepokelewa na katibu mwenezi wa CCM ndugu Humphrey Polepole.

Siasa za uhasama, malumbano na chuki zimeniondoa CHADEMA. Nimeamua kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwa maslahi ya taifa... Kwa sababu huwezi kufanya hivyo ukiwa upande wa pili, lazima utaonekana msaliti tu... Wana Monduli naombeni mnielewe, nitakuja kuzungunza nanyi," Julius Kalanga Laizer, aliyekuwa Mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CHADEMA.

Julius Kalanga aliwahi kuwa diwani kupitia CCM, kabla ya kuhamia Chadema 2015
Good news kwa CCM
Bad News kwa Chadema
 
Sidhani kama kuna usahihi maana yule mlezi wake ni Lowassa. Hawezi kuhama hivi hivi maana Lowassa ataonekana ameshindwa kisiasa.

Yaani hiyo ndio itakuwa pigilia msumari kabisa kwa uhai wa kisiasa wa Mzee Lowassa. Yaani amekufa kisiasa; maanake hakuna lolote analoonekana kulifanya aonekane bado yungali hai kisiasa. Hakuna lolote alilofanya kuleta ushawishi ndani ya chama au kwake binafsi aonekane yungali hai. Pole yake.
 
Wamewatenga Lowasa na Sumaye kwenye maandalizi ya mapokezi ya Lissu, wafuasi wao ndani ya chama wameona isiwe nongwa.
 
CCM kwisha kazi na bado mtanunua sana tu. Watanzania tumeshawachoka.
 
Viongozi wa upinzani hasa Chadema wanajisahau kuwa wao sio sawa na mwenyekiti wa CCM.
Mwenyekiti wa CCM na wale wa vyama vya upinzani ni kama mbingu na ardhi.
Mwenyekiti wa CCM akiwalazimisha wanachama wake kupigia kura bajeti analenga kutimiza malengo ya serikali yake.
Lakini wale wapinzani kila mwaka wanalazimishwa kupinga bajeti bila kutuambia wanataka ipitishwe ipi ?
Yani wanataka nchi isiwe na bajeti au wanataka nini na uchache wao?

Mwenyekiti wa Chadema akimbana Mwanachama wake wakati mwingine mtu anaona isiwe tabu naweka maisha yangu rehani halafu bado nabughudhiwa na kutishwa tishwa na mtu asiye na teuzi zaidi ya viti maalum.
Mwenyekiti wa CCM akimtishia mtu ujue kweli mtu anapata tabu sana mana fursa zote za nchi hii zipo mikoni mwake. Sasa mwenyekiti wa Chadama ana nini cha kumtishia mtu mpaka mtu aufyate?

Mbowe ajaribu sasa kusikiliza watu wa maeneo mengine nje ya wale wa waliomzunguka ambao wanaangalia maslahi yao kwanza.
Vinginevyo chama kitapukutika kabisa.
Watanzania hawana uelewa huo wanaoufikiria wapinzani.
Wengi wanaamini kuwa juhudi za Mh. Rais zinavunja nguvu ya vyama vya upinzani. Watapinzani wamejisaha kabisa.
Ngoja wabunge wao waishe ili wajipange upya.
Pumba. Unataka kutuambia ******** ndio menye akili kuliko wote hapo ccm? Acheni upumbavu nyie majitu ya ccm
 
Maendeleo hayana Chama,hii kauli ya Mheshimiwa naona ipo kisiasa.
 
Tumeshindwa kupata Ushahidi wa zilipo elekea 1.5 Trillion ,wenye Mamlaka na Pesa wanaamua tu sasa kutu geuza geuza kama Samaki.
 
Siasa bana..
Mbunge / anahama chama kwa madai kwamba wabunge wa upinzani wanalazimishwa kupinga bajeti na wakifanya vingine wanaonekana wasaliti alafu unahamia chama ambacho wabunge wanalazimishwa kupitisha bajeti na wakifanya vingine wanaonekana wasaliti vilevile
HAPO NDIPO UNAPOONA MASLAHI BINAFSI YANAHUSIKA
 
Back
Top Bottom