The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, Ummy Ally Mwalimu, amejiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika tarehe 27/11/2024.
Ummy ametekeleza haki yake hiyo ya kikatiba katika mtaa wake wa Suji, uliopo kata ya Mzingani, ambapo pia ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wakazi wa Jiji la Tanga kujitokeza kujiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura ili waweze kupata haki ya kushiriki katika uchaguzi wa viongozi wa mitaa yao.