joshydama
JF-Expert Member
- May 10, 2016
- 4,623
- 5,039
Wabunge wa Cha tawala sijui wanatumia nini kufikiria na kuchanganua mambo maana katika masuala ya kishenzi shenzi wanaunga mkono sana lakini katika ishu nyeti unakuta wamezubaa tu hata kuunga mkono hawataki....so sad!! Maana nashindwa kuelewa kama ni uoga au nini?Katika hali isiyo ya kawaida mbunge wa Karagwe (CCM) Mh Inocent Bashungwa ameomba uwanja wa Kayanga mjini Karagwe ujengwe kama kumbukumbu ya kitendo cha mgombea Urais kupiga push up jukwaani
Akijibu ombi hilo waziri anayehusika na Habari, michezo, utamaduni na sanaa Nape amesema mchakato wa kuenzi kumbukumbu hiyo unaweza kuanza maana kitendo kile kilionyesha ni jinsi gani mgombea wao angetengeneza serikali ya kazi tu na kwamba mgombe mwingine ingekuwa kazi kwake kufanya hivyo.
Hili suala la kuweka sijui ukumbusho wa push ups utasaidia nini wananchi? Sijui wanaipeleka wapi nchi yangu Tanzania.