Hapana mkubwa,wapo Wanakagera wengi sana wanaojitambua,kuwaweka wote kwenye kapu moja kwa sababu ya "uhalo" wa mtu mmoja ni kuwakosea heshima Wanakagera makini.
Jambo la msingi ambalo tunaweza kujifunza kupitia hoja mfu za wanaCCM ni namna wanavyojionesha jinsi walivyo watupu kifikra.Huwa nasema mara kadhaa,hivi hao viongozi wa ccm wanajisikiaje kama nafasi walizonazo wamezipata baada ya kuchaguliwa na watu wasiojitambua?Hivi zile kura milioni 8 alizopata mheshimiwa ndiyo alizipata toka kwa watu wa aina hiyo?Kama ndivyo,basi sina sababu ya kuhoji nchi inavyoendeshwa,ngoja tuburuzwe tu Maana hakuna namna.
Tunapofikia hatua ya kupokea kofia,kanga t-shirts,chumvi na viberiti,kisha tukakubali kusombwa kwa maroli na mikokoteni ya punda kwenda mikutanoni,halafu tukashangilia push-ups na ahadi za kuleta Kilimo cha umwagiliaji wa ubuyu,unatarajia nini toka kwa watu wa aina hiyo?
Jamii iliyoparaganyika kifikra haiwezi kuwa serious kwenye mambo ya msingi.Tutaishia kuwa nashabiki wa upuuzi na kuishia kutumiwa kama wanasesere.Wako wapi wanaCCM makini,je kati ya hao milioni 8, waliyoichagua CCM,hakuna Mwenye uthubutu wa kukemea futuhi hizi zinazokidharirisha chama,au wote ni mapoyoyo na wanakubaliana na huu utumbo unaoendelea huko mjengoni?
Sasa tumefahamu kwa nini ilikuwa ni lazima bunge lisionekane live,Kidumu CHAMA CHA MWENDOKASI(CCM).