Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi (CCM) mbaroni kwa kukutwa na Silaha 16 na risasi 536

Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi (CCM) mbaroni kwa kukutwa na Silaha 16 na risasi 536

To hide their gross incompetence in handling covid 19 pandemic na kuficha takwimu… they'll do anything to change the narrative kuanzia Mwigulu kuteuliwa tena, kelele za Bungeni, kiazi kukamatwa na bunduki na marisasi zote hizi ni mbinu za kuficha uzembe na kukwepa uwajibikaji.
 
Eti wa chama gani huyu??
Kadoji bunge, anawinda nyara za Kigwa??😀😀
Daah tumeipenda wenyewe, wacha tuisome namba eeh......mbele kwa mbele, atalipa faini keshi ya kama milioni 250...

Tukumbushane kwann Rostam aliunga juhudi mkono..

Jela za wezi wa kuku siyo hao...

Everyday is Saturday.........................😎
 
Oooh huyo nae hafai hata kuwa mbunge ni zero
Hakuna maendeleo yoyote aliyofanya Wilaya ya kishapu ,mpaka leo barabara ya vumbi tu



Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kumbe bado Kuna majimbo yenye wabunge wa ccm na bado hayana barabara za lami? Huku penye wabunge wa upinzani tunaambiwa tulikosea kuchagua,je na huko kwenu shida ni Nini au unaweza ukachagua ccm na bado ukawa umekosea kuchagua?
 
sasa hii ndio sabotage..,unaeza kuta wamegombana kidogo kwenye lichama lao huko wameamua kupandikiziana silaha majumbani na kupeana kesi maccm hayaaminiki hata kidogo


Sent from my iPhone using JamiiForums
Hakuna kesi hapo Hizo nyama Bunduki ataziruka atakana hazijui na kusingizia anaishi Dsm hajui ni nani alipeleka Bunduki kwake
 
View attachment 1441653

Polisi mkoani Shinyanga wanamshikilia Mbunge wa Kishapu (CCM) Suleiman Nchambi kwa tuhuma za kukutwa na silaha 16, risasi 536 pamoja na nyara za Serikali
==

Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Suleiman Masoud Suleiman maarufu Suleiman Nchambi (CCM) kwa tuhuma za kupatikana na silaha 10, risasi 536 na nyama zinazodhaniwa kuwa ni za wanyawapori kinyume cha sheria.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatano Mei 6,2020, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Mei 3,2020 majira ya saa sita kasoro usiku katika mtaa wa Lubaga kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

“Mei 3,2020 majira ya sita kasoro usiku Kikosi kazi cha askari wa upelelezi kikiongozwa na Kaimu Mkuu wa upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi kwa kushirikiana na Afisa wa Wanyamapori mkoa wa Shinyanga Perfect Mbwambo walifanya upekuzi kwenye makazi ya Mbunge wa Jimbo la Kishapu baada ya kupata taarifa za kiintelejensia kuwa Mheshimiwa huyo alikuwa akifanya uwindaji haramu kwenye eneo la Negezi wilayani Kishapu akiwa na gari yenye namba za ujasili T760 DSD Nissan Hard Body”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

“Katika upekuzi huo walifanikiwa kukamata nyama iliyodhaniwa kuwa ni wanyamapori yenye uzito wa kilogramu 35 zikiwa zimehifadhiwa kwenye jokofu lililokuwa jikoni,jingine sehemu ya mazoezi na nyama nyingine ilikutwa kwenye gari hilo likiwa limeegeshwa nyumbani kwake ndani ya uzio wa nyumba hiyo”,amesema Kamanda Magiligimba.

“Katika gari hilo kulikutwa silaha moja aina ya shortgunWakati askari hao wakiendelea na upekuzi ndani ya chumba chake cha kulala zilipatikana silaha zingine za aina mbalimbali na kufanya jumla ya silaha zilizokamatwa kuwa 16 ambazo ni Airgun 3, Shortgun 3,Rifle 8, Pistol 1 na Mark IV 1 pamoja na risasi 536 zikiwa kwenye kabati la nguo",anaeleza Kamanda.

“Baada ya uchunguzi wa awali iligundulika kuwa silaha 10 ambazo ni Airgun 2, Rifle 5, Shortgun 2 na Mark IV 1 kati ya 16 anazimiliki isivyo halali”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

Kamanda Magiligimba amesema nyama hizo zimepelekwa maabara ya mkemia mkuu wa Serikali kwa uchunguzi zaidi na gari husika limekamatwa.

“Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika. Natoa onyo kali kwa yeyote atakayejihusisha na vitendo vya kumiliki silaha isivyo kihalali hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake”,amesema Kamanda Magiligimba.


Waniletee mimi huyu kijana.
 
Amini nawaambia Huu Ni mchezo wa CCM na Jeshi la polisi kuondoa watu kwenye issue ya covid na Chadema kutoka Bungeni. Kumbukeni Leo pia imeachiwa clip ya makonda akitaka wabunge wa upinzani kurudi Bungeni ...



Watanzania acheni kuchezewa na x
" cheap politics".. Endeleeni na mapambano ya corona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
6 May 2020
Shinyanga, Tanzania

Polisi wanamshikilia Mbunge wa Kishapu (CCM)

Polisi mkoani Shinyanga wanamshikilia Mbunge wa Kishapu (CCM) Suleiman Nchambi kwa tuhuma za kukutwa na silaha 16, risasi 536 pamoja na nyara za Serikali. Mbunge huyo alionekana akifanya ujangili kufuatana na taarifa za kiintelejensia na hivyo Jumapili tarehe 3, May 2020 kikosi kazi maalum kilikwenda nyumbani kwa mbunge na kumkuta akiwa na silaha hizo na nyara chumbani kwake hivyo akakamatwa na kutiwa nguvuni.



Source : Mwananchi digital
Hiki chama cha CCM hakiachi asili yake ya ujangili wa kila namna.
 
Hii itakuwa ni mtego,kama siyo njama wasingemtangaza kwenye vyombo vya habari maana hata tbc wamemtangaza
Huyu ni mwenzetu hivyo hii kesi itakuwa nyepesi sana... Tutakachofanya ni kusubiri kelele za mitandaoni zipoe

Jr[emoji769]
 
Toka maktaba/ archives online
6 Aug 2018
Biharamulo, Kagera
Tanzania

Mbunge wa CCM Suleiman Nchambi na wenzake 10 mahakamani kwa tuhuma za rushwa



Mbunge wa Kishapu kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Suleiman Nchambi pamoja na wenzake kumi wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Biharamuro Mkoani Kagera wakikabiliwa kwa kosa la kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Source : Azam TV

Soma zaidi : https://www.mwananchi.co.tz/habari/...1597578-4699380-view-asAMP-cnve5gz/index.html

Mbunge CCM anaswa kwa tuhuma za rushwa - KUSAGA NEWS
6 Aug 2018 · Mbunge wa Kishapu (CCM), Suleiman Nchambi na viongozi watatu wa mgodi wa Stamigold ulioko Tulawaka wilayani Biharamulo mkoani
 
Hivi ni vijimambo,huyu mwenzetu tutamaliza ndani ya chama dola.
 
Hakuna kesi hapo Hizo nyama Bunduki ataziruka atakana hazijui na kusingizia anaishi Dsm hajui ni nani alipeleka Bunduki kwake
Angekuwa ni wa upinzani nadhani msajili angeshakifuta chama chake long huku mhusika ashakabidhiwa wasiojulikana.
 
Back
Top Bottom