Pre GE2025 Mbunge wa Moshi mjini, ⁨Priscus Tarimo amekuwa mtu wa mwanzo kuleta maajabu ya maendeleo Moshi mjini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Joined
Jul 27, 2024
Posts
26
Reaction score
12
Mbunge wa Moshi mjini MH.PRISCUS TARIMO @⁨Priscus Tarimo B⁩ amekuwa mtu wa mwanzo kuleta maajabu ya maendeleo Moshi mjini...

Haikuwa rahisi kwa chama kumpa ridhaa mtu ambaye hajawahi kuwa kiongozi wa kada yoyote ndani ya CCM na ambaye walitazama sifa zake wakaona ni mbovu hazifai kuwa mbunge....

Tabia njema na uzoefu katika Uongozi ndio chanzo kikubwa Cha mwanaccm kupewa ridhaa na CCM hainaga kujaribu mtu kwenye uongozi Bali inateuwa Wana CCM makini na haswa wabunge lazima Chama kitazame sifa stahiki na historia za tabia kwa muombaji...

CCM ikikunyima nafasi basi fahamu wewe haufai na ndio maana yule wa 2020 aliponyimwa akageuka kuwa msaliti wa CCM na hata baada ya kampeni aliendelea kuwa msaliti kwa kupinga maendeleo yanayoletwa na CCM na kutukana CCM na viongozi mpaka kufikia kuisemea vibaya ilani ya Mama Samia Rais wetu...

CCM inateuwa kwa misingi madhubuti sana kutazama nani ANAFAA na Kumpa ridhaa ya kugombea haswa wabunge wamekuwa watu wenye kutegemewa na TAIFA kutunga Sheria na kupitisha hoja mbalimbali hivyo lazima watu hao wawe watu imara KITABIA na ELIMU na UZOEFU wa kiuongozi sio kumpa Mtu asiye na sifa na hiko ndio kichujio Cha 2020 na mwaka huu ndio hiko hiko kitatumika kuchuja Wapotoshaji na waongo na watukanaji walio dhihiri Moshi hii kwa nafasi mbalimbali haswa ubunge...

Pongezi nyingi sana kwa mbunge kwa kutekeleza majukumu yake kwa ukubwa wa Hali ya juu na tunaona ila kwa vipofu waliofungwa macho kwa gundi ya malafi wa madaraka.

2025 PRISCUS TARIMO BINGWAA ANAFAA HATUMUACHI TUNA YEYE IMETIKI NJE NDANI✅✅✅✅

By ✍🏾Mwandishi Bora
 
Weka picha tuone Kazi zake alizofanya .


Mwambie safari hii uchaguzi utakuwa wa ushindani na mgumu hivyo awekeze katika Kazi na sio Kama hivi
 
Priscus acha kujipigia krosi, hebu tuambie ni maendeleo gani umeyaleta hapo Moshi kwa kipndi chako cha ubunge.

Baada ya Ndesamburo kuondoka, mji wa Moshi umeporomoka sana kimaendeleo
 
Watu wa Kilimanjaro mnapenda sana kujianzishia nyuzi za kujifagilia.

Hata Kamanda wa CHADEMA Henry Kilewo alishawahi kufanya hivi hivi kwa kutumia ID fake kujisifia yeye mwenyewe na aliyekuwa mke wake Joyce Kiria! Ila mwisho wa siku aliishi tu kuumbuka baada ya ID yake kuwekwa wazi.
 
Uchaguzi umekaribia. Tutaona kila rangi.
Nitarudi
KAZI ni kipimo cha utu
 
Unaweza kutueleza alichofanya au tukakushtaki mahakamani kwa kosa la kumdhalilisha mbunge na kumchafua kwa kuandika maneno ya uongo kuhusu priscuss??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…