TANZIA Mbunge wa Muhambwe(Kigoma), Atashasta Nditiye afariki dunia baada ya kupata ajali ya gari Februari 10

TANZIA Mbunge wa Muhambwe(Kigoma), Atashasta Nditiye afariki dunia baada ya kupata ajali ya gari Februari 10

Huu uhamisho wa Dodoma una baraka zote kweli? mbona unatuteketeza hivi na kutezitesa familia zetu jmn !!
 
Ina maana hata bungeni haikutangazwa kwamba kuna mbunge kapata ajali?

Au kuna mbunge kalazwa?

Acha urongo King Kong!

Ina maana hata bungeni haikutangazwa kwamba kuna mbunge kapata ajali?

Au kuna mbunge kalazwa?

Acha urongo King Kong!
Bwashee saa mbili zimepita bila kuweka link iliyoelezea hiyo ajali ,haujaweka hata audio clip kutoka kwa Ndugai,Tulia au Mwenyekiti....Inawezekanaje mtu mzito kama Nditiye apate ajali halafu hakuna mtu yeyote aliyereport??
 
Mbona hakuna taarifa ya ajali toka hiyo juzi hadi anakufa ndio taarifa zinatoka. Wangeendelea tu kuficha hata mazishi yake. Mtakumbuka sana

Hatuwezi kutatua matatizo kwa kujidanganya kwamba hayapo - JK Nyerere 1922-1999.
 
Kwa comment hii wewe ni kilaza square uchaguzi upi bila tume huru
Sisi ndio vilaza zaidi, tunashiriki uchaguzi ambao tunajua tunakwenda kupoteza? Tunachangishwa pesa wakati wanajua tunakwenda kipoteza, tunatupa pesa na wakati, ni bora hizo pesa zaidi ya bilioni zinge jenga ofisi mpya na kuhama makaburini Ufipa. Yaani wamekosa kitu cha kufanya vilaza.
 
Rest in peace rafiki. Alikuwa ni mmoja kati ya mawaziri wenye akili kubwa wanaojielewa. Nilitegemea atakuwa waziri kamili baada ya uchaguzi
 
Hawa wazurumati hawafai kuendelea kuishi hapa Tanzania


Eeeh Mungu kamchukue na bwana yule ....
 
Kuna ajali mbali mbali, hata ajali za mfumo wa upumuaji, mtu anaweza ukapaliwa na chakula ukashindwa kupumua. Cha msingi tufuate maelekezo ya wataalamu wa afya.
OK, nimeelewa mkuu. SO huyu mhe bila shaka nae alipatwa na ajali za namna hi ulioieleza hapa!?
 
Alishinda kihalali kwenye kura? Kama alishinda kihalali RIP, lakini kama ni hawa walioshinda kwa maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura, basi apambane na hali yake.
Baadhi ya hawa watu tusiwalaumu bure. Wengi wao ni 'mateka' tu kama tulivyo waTanzania wengine wote.
Inawezekana hata hakujua kura zimetoka wapi, yeye katangazwa tu kwamba ameshinda.
 
Ajali ya gari!! Huo ni uwongo. Ilikuwa ajali ya namna gani ambaye imetokea Dodoma, halafu hata isisikike kwa ntu hata mmoja au kwa chombo chochote cha habari?

Jamani kifo siyo tendo la aibu. Tuweni wakweli.

Hizi fikra kuwa mtu kufariki kwa corona ni aibu au laana, ni kufifisha jitihada za kupambana na adui ambaye anatuandama.

Sina imani kuwa amefariki kwaajili, na sisemi amefariki kwa corona maana sina uthibutisho.

Kama kuna uthibitisho wa kutokea ajali juzi tuletewa (najua hautakuwepo maana hakukuwa na ajali).

Pole sana wafiwa. Mungu mwenye uweza awapeni nguvu ya kuyapokea mapenzi yake.
Ni kweli juzi tarehe 10 majira ya asubuhi eneo la Nzuguni (Nanenane) mkabala na stendi kuu ya Mabasi kulitokea ajali ya kugongana uso kwa uso kati ya gari moja hivi ya kisasa yenye rangi nyeusi na coaster yenye rangi nyeupe.

Kwa namna ile gari ilivyo haribika upande wa mbele, ingekuwa ni vigumu sana dereva kutoka salama. Huenda hiyo gari ndiyo ilikuwa ni ya huyo Mheshimiwa. Nilipita hilo eneo mida flani nikiwa kwenye Shabiby!

Apumzike kwa amani Mheshimiwa Nditiye. Kimsingi hakuwa mtu mbaya sana enzi za uhai wake.
 
Back
Top Bottom