TANZIA Mbunge wa Newala Vijijini, Ajali Rashid akutwa amefariki katika Gesti ya Mingoyo

TANZIA Mbunge wa Newala Vijijini, Ajali Rashid akutwa amefariki katika Gesti ya Mingoyo

Dogo nyie watu wa upinzani kazi yenu kwa awamu ya tano baada ya CCm kuwabana kila kona hadi kuishiwa pumzi,mmekuwa na mikakati ya kutaka kuiaminisha jamii kuwa mauaji yote yanayofanywa au kutokea katika hali ya sintofahamu yanafanywa na Government,kwa dhana hii huyu Mh .angekuwa ni wa upande ule, kelele zingesikika sana tu,

naomba nikuambie kuwa licha ya juhudi zenu za kutaka kuichafua government kwa wananchi hii haisaidii na wala haitakuwa mbinu mbadala ya ninyi upinzani kuchukua uongozi wa nchi hii.

Kitakacho wanusuru japo kwa uchaguzi wa oktoba muwe hata na wabunge wawili na madiwani japo watano ni kubadili Sera zenu kitoka kwenye chama cha ushirika na kuwa chama cha siasa chenye mlengo wa kutaka kutatua changamoto za wananchi kama ambavyo serikali yangu ya CCM inavyo shughulikia matatizo ya Raia wake.
Ungesikia mengi gani we dogo? Unataka kuleta mambo ya majitaka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amepata hasara kubwa kufia ndani ya CCM!!
Mbunge wa Newala vijijini, AJALI RASHIDI AKBAR amekutwa amefariki katika gesti ya Mingoyo - Mnazi Mmoja - Lindi, inaelezwa kuwa yeye ndio mmiliki wa gesti hiyo mpaka sasa bado chanzo cha kifo chake hakijafahamika na mwili wake umepelekwa hospitali ya Sokoine kwa uchunguzi.

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, ameeleza kusikitishwa kwa taarifa za kifo cha Mbunge wa Newala Vijijini, Rashid Akbar, kilichotokea leo Januari 15, 2020 mkoani Lindi, na kueleza ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia watatoa taarifa ya mazishi ya Mbunge huyo.

Wakati akiwa hai akichangia mjadala Bungeni
View attachment 1324208

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dogo nyie watu wa upinzani kazi yenu kwa awamu ya tano baada ya CCm kuwabana kila kona hadi kuishiwa pumzi,mmekuwa na mikakati ya kutaka kuiaminisha jamii kuwa mauaji yote yanayofanywa au kutokea katika hali ya sintofahamu yanafanywa na Government,kwa dhana hii huyu Mh .angekuwa ni wa upande ule, kelele zingesikika sana tu,

naomba nikuambie kuwa licha ya juhudi zenu za kutaka kuichafua government kwa wananchi hii haisaidii na wala haitakuwa mbinu mbadala ya ninyi upinzani kuchukua uongozi wa nchi hii.

Kitakacho wanusuru japo kwa uchaguzi wa oktoba muwe hata na wabunge wawili na madiwani japo watano ni kubadili Sera zenu kitoka kwenye chama cha ushirika na kuwa chama cha siasa chenye mlengo wa kutaka kutatua changamoto za wananchi kama ambavyo serikali yangu ya CCM inavyo shughulikia matatizo ya Raia wake.

Sent using Jamii Forums mobile app

Narudia tena dogo, maovu yote yenye utata, uminywaji wa haki za watu wenye itakadi tofauti na rais aliye madarakani una baraka zake, na hilo halihitaji uwe na degree kulijua. Hakuna mtu yoyote anapoteza muda wake kuichafua serikali kwakuwa sio safi, bali watu wanapigia tu mstari mambo hayo.

Wapinzani wako vizuri na sera zao zinaeleweka, lakini kupitia madaraka ya urais ndio tumejionea chaguzi za kishenzi zilizojaa uhayawani wa wazi. Sasa hivi tunaona vyombo vya dola na tume ya uchaguzi vikipokea amri toka juu, ya kuvuruga na kunajisi uchaguzi ili wagombea toka chama cha rais watangazwe washindi bila ridhaa ya umma! Uzuri wananchi nao walikuwa wameshamka, hivyo walisusia kushiriki chaguzi za kishenzi. Rejea idadi ndogo ya wapiga kura iliyojiandikisha uchaguzi serikali za mitaa, tena hilo lilifanyika bila ushawishi wa chama chochote cha siasa. Na huo uchaguzi wa Oktoba kwa mwenendo wa awamu hii bila tume huru ya uchaguzi, itakuwa sio uchaguzi bali ni maonyesho ya kipimo halisi cha ujinga wa mtu mweusi, linapokuja suala la kupata madaraka.

Iwepo tume huru ya uchaguzi kisha uje ulete mrejesho hapa jukwaani, sio hiyo tume ya uchaguzi + vyombo vya dola kuchukua maagizo toka kwa rais ili wawatangaze wagombea wa chama chake, kwa hofu ya kupoteza ajira zao. Hivyo huo uchaguzi wa Oktoba sio wa ushawishi wala kukubalika kwa sera, bali utakuwa uchaguzi wa kudhibitisha madaraka ya rais yanayotumika vibaya.
 
Back
Top Bottom