DOKEZO Mbunge wa Ngorongoro (CCM): Maisha yangu yapo hatarini

DOKEZO Mbunge wa Ngorongoro (CCM): Maisha yangu yapo hatarini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Mbunge wa Ngorongoro (CCM) Emmanuel Lekishoni Ole Shangai ameandika kwamba maisha yake yapo hatarini na kwamba imeagizwa auwawe kwa amri kutoka kwa RC wa Arusha na DC wa Ngorongoro

“Naomba kuwasilisha kwenu, kama Kuna lolote litanitokea mjue kuwa ni maelekezo ya DC wa Ngorongoro na mkuu wa mkoa wa Arusha” - Emmanuel Lekishoni Ole Shangai

Shangai anaeleza kwamba hata mke wake na familia yake wanapokea vitisho vya kuuwawa na kwamba wamefika nyumbani kumkamata mkewe.

Emmanuel Lekishoni Ole Shangai anasema baada ya jeshi la polisi kuvamia nyumbani kwake na mitutu ya bunduki mama yake mzazi alizimia hadi sasa hajarudi katika hali yake.

Hii ni baada ya Emmanuel Lekishoni Shagai kuamua kukataa kabisa biashara ya kuwahamisha Maasai kutoka Ngorongoro kwa lazima.

Maji yamechemka sana. MaCCM yameamua kumalizana. Ukizoea kula nyama ya mtu huwezi kuacha. Sasa wanamshughulikia ndugu yao.
9cdbc136-fc10-42f2-b963-0e457cd6d95b.jpeg
 
Mbunge wa Ngorongoro (CCM) Emmanuel Lekishoni Ole Shangai ameandika kwamba maisha yake yapo hatarini na kwamba imeagizwa auwawe kwa amri kutoka kwa RC wa Arusha na DC wa Ngorongoro

“Naomba kuwasilisha kwenu, kama Kuna lolote litanitokea mjue kuwa ni maelekezo ya DC wa Ngorongoro na mkuu wa mkoa wa Arusha” - Emmanuel Lekishoni Ole Shangai

Shangai anaeleza kwamba hata mke wake na familia yake wanapokea vitisho vya kuuwawa na kwamba wamefika nyumbani kumkamata mkewe.

Emmanuel Lekishoni Ole Shangai anasema baada ya jeshi la polisi kuvamia nyumbani kwake na mitutu ya bunduki mama yake mzazi alizimia hadi sasa hajarudi katika hali yake.

Hii ni baada ya Emmanuel Lekishoni Shagai kuamua kukataa kabisa biashara ya kuwahamisha Maasai kutoka Ngorongoro kwa lazima.

Maji yamechemka sana. MaCCM yameamua kumalizana. Ukizoea kula nyama ya mtu huwezi kuacha. Sasa wanamshughulikia ndugu yao.View attachment 2723126
Wacha migambo waukesha na kukanyagana ndiyo furaha yetu wazalendo wa nchi hii.
 
Moto umeungua...
Baridi imeganda...
Naambiwa wamasai wanapitishiwa fedha haramu wasilete chokochoko siku ya ujio wa Mfalme wa Dubai!
Kuna Mzee Ole Kisongo ndiye dalali mgawa-fedha!
Fedha zigawanywa kwa vigezo vya rika na gender!
 
DPW inawachanganya, Ngorongoro kunawachanganya yote ili kumfurahisha mwarabu, tuna kiongozi mjinga sana, hawajali hata kama wazee wa wenzao wanazimia, wao wako busy kama watumwa wa mwarabu kuhakikisha wanamuandalia makao mema bosi wao.

Aibu kubwa sana hii.
 
DPW inawachanganya, Ngorongoro kunawachanganya yote kumfurahisha mwarabu, tuna kiongozi mjinga sana.
Yani mambo ya ajabu sana

Kuna jamaa yangu nilikuwa naongea nae akaniambia suala la Ngorongoro ni la moto sema tu halijapewa airtime kama DPW.

Unaambiwa habari za kusema wamasai wamehama kwa hiari ni uongo mtupu.

Hii nchi kazi kwelikweli
 
Nchi yetu sote ila kuna baadhi ya watu tuliowapa uongozi kujiona wao ndio kila kitu dhidi wananchi...

Wakumbeke upole una muda wake, watu watachoka, wasituone wametuweza na kufanya wanavyohitaji ila yana mwisho
 
Ni mpumbavu pekee ataamini wamasai wamehama kwa hiari. Tanzania tunafanyiana ukatili usiomithilika kwa uroho wa pesa na madaraka. Inasikitisha sana yani.

Back
Top Bottom