DOKEZO Mbunge wa Ngorongoro (CCM): Maisha yangu yapo hatarini

DOKEZO Mbunge wa Ngorongoro (CCM): Maisha yangu yapo hatarini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ni mpumbavu pekee ataamini wamasai wamehama kwa hiari. Tanzania tunafanyiana ukatili usiomithilika kwa uroho wa pesa na madaraka. Inasikitisha sana yani.
Mno yani mimi baada ya kusikia hilo nilisikitika sana halafu juzi nikaona uongo mwingine wakidai wamasai wanamuomba sa100 wahame wameshikishwa na mabango feki kesho yake naona waandishi wa habari wameshambuliwa na mikuki na mishale hakika niliendelea kudhibitisha hii nchi viongozi wetu ni wahuni na wako kwa ajili ya matumbo yao
 
Mbunge wa Ngorongoro (CCM) Emmanuel Lekishoni Ole Shangai ameandika kwamba maisha yake yapo hatarini na kwamba imeagizwa auwawe kwa amri kutoka kwa RC wa Arusha na DC wa Ngorongoro

“Naomba kuwasilisha kwenu, kama Kuna lolote litanitokea mjue kuwa ni maelekezo ya DC wa Ngorongoro na mkuu wa mkoa wa Arusha” - Emmanuel Lekishoni Ole Shangai

Shangai anaeleza kwamba hata mke wake na familia yake wanapokea vitisho vya kuuwawa na kwamba wamefika nyumbani kumkamata mkewe.

Emmanuel Lekishoni Ole Shangai anasema baada ya jeshi la polisi kuvamia nyumbani kwake na mitutu ya bunduki mama yake mzazi alizimia hadi sasa hajarudi katika hali yake.

Hii ni baada ya Emmanuel Lekishoni Shagai kuamua kukataa kabisa biashara ya kuwahamisha Maasai kutoka Ngorongoro kwa lazima.

Maji yamechemka sana. MaCCM yameamua kumalizana. Ukizoea kula nyama ya mtu huwezi kuacha. Sasa wanamshughulikia ndugu yao.View attachment 2723126
Yangu macho
 
Yani mambo ya ajabu sana

Kuna jamaa yangu nilikuwa naongea nae akaniambia suala la Ngorongoro ni la moto sema tu halijapewa airtime kama DPW.

Unaambiwa habari za kusema wamasai wamehama kwa hiari ni uongo mtupu.

Hii nchi kazi kwelikweli
Kwa taarifa ya awali ya mwananchi paper ni asilimia tatu tu! Waliohamishwa kwenda msomera.
Na kinachofanyika sasa ni hujuma za wazi wazi Kwa Jamii ya wamasai ili wagive up waombe kuondoka! Serikali na NCCA wameacha kupelekea fedha zozote Kwa ajili ya huduma za afya maji na soda elimu na wamewazuia wadau wowote Kutoa huduma hizo!
Kilichotokea ndio hiki sasa wanamwinda Mbunge Kwa kuwatetea wananchi wake wasihame!

Kitenge et al wiki iliyopita walitaka kulianzisha tena eti Wamasai Loliondo wamwangukia mama Samia awahamishe! Wakajikuta swala la DP weld linawaelemea na pesa wamekula
 
Samia anayowafanyia wamasai huko Ngorongoro kuna siku yatawekwa wazi. Mambo ya ajabu kabisa.
Mh. Rais kazungukwa na genge la waharifu, nenda Tanzanite na mkoa wa manyara kwa ujumla kuna bonge la ujambazi wa vitalu vya kuwindia unaendelea, Tanzanite mapato ni mwendo wa kugawana wamejazwa Wazanzibar mpaka balaa na wilaya yenye mkakati kamuweka mkuu wa wilaya balaa.
 
Mnakandana wenyewe kwa wenyewe tena

Ova
 
Mh. Rais kazungukwa na genge la waharifu, nenda Tanzanite na mkoa wa manyara kwa ujumla kuna bonge la ujambazi wa vitalu vya kuwindia unaendelea, Tanzanite mapato ni mwendo wa kugawana wamejazwa Wazanzibar mpaka balaa na wilaya yenye mkakati kamuweka mkuu wa wilaya balaa.
Siyo kwamba na yeye ni jambazi mmoja wao?
 
Yani taratibu tutakuja kufika walipo Congo DRC. Huwa hayaanzagi ghafla tu. Wamasai watakapochoka zitaanza ambush kama za Kibiti ndio tutaheshimiana.
Mno yani mimi baada ya kusikia hilo nilisikitika sana halafu juzi nikaona uongo mwingine wakidai wamasai wanamuomba sa100 wahame wameshikishwa na mabango feki kesho yake naona waandishi wa habari wameshambuliwa na mikuki na mishale hakika niliendelea kudhibitisha hii nchi viongozi wetu ni wahuni na wako kwa ajili ya matumbo yao
 
Siyo kwamba na yeye ni jambazi mmoja wao?
Hapana Rais Dkt Samia hajui vitu vingi kwa sababu walimfanyia kama alivyofanyia Papa Yohana wa II, yaani walimtenegenezea na bado wanamtengenezea safari nyingi nyingi sana yaani matukio kila kukicha kiasi kwamba hana kabisa muda na wanaoendesha serikali ni genge fulani lipo Kule kunani. Yaani Rais Samia ni mzalendo sana tena sana.
 
Acheni mama aifungue nchi 👏👏😁

JamiiForums934640752.jpeg
 
Back
Top Bottom