Tetesi: Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya kuhamia Chama cha Mapinduzi muda wowote kuanzia sasa

Tetesi: Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya kuhamia Chama cha Mapinduzi muda wowote kuanzia sasa

Write your reply...ni chizi pekee atafurahia upinzani ukifA
hamjui kuwa upinzani ndio unaishtua serikali kufanya mambo kwa wananchi? bila upinzani mngejua epa,Richmond ,kagoda,meremeta,escrow? mitahira duniani haiishi
 
Hii biashara haiwasaidi lakini kwa aibu hawawezi kuiacha maana watachekwa (wataulizwa imeleta tija gani) hivyo watajitutumua tu kuendelea nayo kuliko ku-surrender.

Eti hawa ndio watu wa kuipeleka Tanzania kufikia katika uchumi wa kati!!

Wabongo mtasubiri sana!!

SS hebu tafakari NA ujiangalie vizuri, unakurupuka kuchangia kitu hakina uhakika, hatujaona ukweli wa Milya kuhama chama.

Hata ikiwa lina ukweli, hebu kishauri chama chako kijichunguze na kujua mambo yanaharibikia wapi, pia waanze uchunguzi wa wabunge wao wanao onyesha ishara ama nia za kuhama, na kuwachukulia hatua. Iwapo watagundua mbunge anayetia mashaka ya kuvuka daraja, basi Chadema kimfukuze yeye kabla hajachukua hatua hiyo, hilo litaleta tija NA kumharibia huyu mbunge hata kuja kupata kura atakapo ingia chama kingine.

Lakini hizi kelele na kejeli wakati wewe ndiye uliyeachwa njia panda hazina faida kwenu.
 
Nadhani Sasa tukubali kabisa kuwa CCM ina madhaifu yake kwenye awamu zote.
Sina uhakika na suala la Kununuliwa kwa Wabunge au madiwani lakini wote kwa pamoja iwe ni CCM au Chadema au CUF tunakubaliana kuwa hawa wabunge wanaolisababishia hasara Taifa letu kwa makusudi ni Mafisadi kama mafisadi wengine waliolitia hasara taifa Letu.
Wananchi tuwakatae kwa kila namna. Ni aibu kusimama kabisa hadharani na kumshangilia mtu anayelitia Taifa letu hasara kwa ubinafsi wake.
Hivi Wabunge wote wakiwa ni wa CCM ndio pesa za Maendeleo zitaota tu kama uyoga?
Kwani hao Wabunge wa upinzani wanazuia vipi pesa za maendeleo kupatikana mpaka Pole pole awe anatumia nguvu kubwa kiasi hicho kushirikiana nao kulitia Taifa hasara ya gharama za kurudia uchaguzi ?

Tena Mimi nafikiri ni bora wale watu wengine waliotuhumiwa tu lakini walikua na manufaa na walifanya Mengi Makubwa kwa Taifa hili .Kwa Mfano Prof.Muhongo au Mama Tibaijuka . Ni watu ambao ukichunguza vizuri hicho kinachotajwa kwao kama Ufisadi ni mambo ya kukomaliana tu na kuchafuana lakini walikua ni watu Muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa na Kimataifa.

Sasa hebu tuangalie hawa wengeni wanaolitia hasara Taifa bila sababu yoyote.
Hivi CCM inahangaika kwabembeleza wa nini wakati idadi yao ya kupitisha bajeti inatosha kabisa bungeni?
Kwani bajetib isipopitishwa kwa 100% haipiti? Kwa nini tuingizwe hasara na watu kama akina Mtulia ,Moleli na wengine watu ambao hata kwenye kama za vikao vya harusi hawana influence yoyote . Watu ambao hata Kimataifa hawana tija wao kama wao.
Hivi wanakatwa kodi kiasi gani ili tuhangaike nao na kupoteza kodi za wananchi kwa kufanya uchaguzi?

Ukiangalia sana Ufisadi uliokua unafanywa ndani ya serikali ya CCM awamu zilizopita zilikua ni katika kutakeleza majukumu yao ya kimaendeleo japo tulikua tunaaminishwa kuwa hela zimepigwa sijui nini lakini tulikua hatuambiwi kuwa kuna kitu kimefanyika cha kimaendeleo .

Sasa huu Ufisadi wa miaka hii wa kulitia hasara Taifa unaofanywa na Wabunge na madiwani wanaojiuzulu ni janga lingine kwa Taifa.

Mshahara wa Mbunge wa CCM na yule wa Chadema yote inalipwa kwa kodi za wananchi na sio ruzuku za vyama vyao.

Hivi kama gharama za kumlipa mshahara na kufanya uchaguzi zingelipwa na kodi za WanaCCM pekee wangekubali kuona pesa zao zinachezewa hivyo?

Kwa nini Pole pole anathamini Chama ambacho ni taasisi ya watu wachache lakini anashindwa kuthamini Pesa za umma ambazo ni kodi za watanzania wote?
CCM ni baadhi ya watu katika nchi .Chadema ni baadhi ya watu katika nchi . Vyama vyote ni vinaundwa na baadhi ya watu.Hata wale wasio na vyama ni baadhi ya watu. Watanzania Wote kwa pamoja wanatoa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa sio maendeleo ya Chama kimoja wala viwili.

Sasa inaonekana serikali na Chama chake cha Mapinduzi wamejikita kwenye kujiwekea mazingira ya kupata kura 90% kwa kushirikiana au kulazimishwa na Maigizo ya Wabunge toka upinzani wenye ubinafsi uliopitiza ambao nawaona kuwa ni mafisadi walioibuka miaka hii kwa malengo yale yale ya mafisadi waliowahi kutokea yaani kujinufaisha kupitia fedha za umma.

Fisadi na adui wa Taifa hili ni lazima tumtaje kuwa ni mtu asiye na huruma na pesa za kodi za wananchi.
Mtu asiyejali pesa zinazotokana na kodi ya wananchi yote kwa maslahi binafsi.

Tunahangaika kutafuta pesa kwa ajili ya maendeleo lakini Mtu analipwa mshahara halali wa Ubunge au Udiwani halafu anaacha kwa makusudi Leo , halafu Kesho mtu huyo huyo ambaye ingewezekana apelekwe kwenye mahakama ya mafisadi anaomba tena nafasi hiyo hiyo aingie kwenye bunge lile lile!!

Hapana!!
Twaombe Wale wanaopiga kelele kusema fulani ni adui wa maendeleo kwa sababu anapinga, nawakumbusha kuwa wamesahau au wanafumba macho na midomo yao kwa hawa wanaolipa Taifa hasara ya mabilioni ya fedha kwa ubinafsi wao tu.

Ushauri wangu kwa Mh. Rais ambaye alianza kwa kudhibiti watu wanaochezea ofisi bila tija huku wakilisababishia Taifa hasara , asiwape nafsi ya kugombea kwenye chama Chake mpaka 2020 na wala asiwape nafsi za uteuzi mana hawa sio waaminifu .Hawa Wabunge ni sawa na watumishi wengine wanolipwa kwa kodi ya wananchi halafu wanachezea kazi waliyopewa .
Hawa ni watu wasio na huruma na kodi za wanyonge.

Au kama kweli CCM na serikali yake haijawanunua na Mimi siamini kama wote wamenunuliwa basi iache uchaguzi usimamiwe kwa haki ili kama kweli wananchi wanafurahishwa na tabia hiyo ya kuhama basi watawachagua.

Lakini kitendo cha wakurugenzi kukiuka Maagizo ya Rais anayoyatoa Mara kwa Mara wakati wakuwaapisha kuwa waende kwenye vituo vyao wakatende haki lakini wanashindwa kutimiza majukumu yao kwa makusudi ili Wagombea wale wale waliolitia Taifa hasara washinde tena badala ya kuwapa watanzania wengine waaminifu fursa za kuwatumikia wananchi , hakika tutakubaliana na wale wanaosema kuwa Wabunge hao wananuliwa na sasa Wakurugenzi wanatumika kuwapa ushindi ili waliowanunua wasipate hasara za kununua mtu na mtu huyo anashindwa.

Tuwakatae hawa mafisadi wapya wa kisiasa wanaojali maslahi na umaarufu wao tu huku Taifa likipata hasara.

Na pia tunawakumbusha Wakurugenzi Watende haki kama Mh. Rais alivyowaelekeza wakati wa kuapishwa. Mnalipwa na pesa za Kodi za watanzania wote bila kujali vyama hivyo watendeeni wananchi haki wakati wa uchaguzi ili kuepusha matatizo.Mukilijua hilo mtaacha kuwapa ushindi wale waliochezea pesa za umma kwa kukimbia ubunge huku wakiutaka kwa UDI na uvumba.
 
SS hebu tafakari NA ujiangalie vizuri, unakurupuka kuchangia kitu hakina uhakika, hatujaona ukweli wa Milya kuhama chama.

Hata ikiwa lina ukweli, hebu kishauri chama chako kijichunguze na kujua mambo yanaharibikia wapi, pia waanze uchunguzi wa wabunge wao wanao onyesha ishara ama nia za kuhama, na kuwachukulia hatua. Iwapo watagundua mbunge anayetia mashaka ya kuvuka daraja, basi Chadema kimfukuze yeye kabla hajachukua hatua hiyo, hilo litaleta tija NA kumharibia huyu mbunge hata kuja kupata kura atakapo ingia chama kingine.

Lakini hizi kelele na kejeli wakati wewe ndiye uliyeachwa njia panda hazina faida kwenu.
Wamfukuze ili mseme kaonewa?Endeleeni na biashara yenu ya utumwa!
 
Siku hizi mbona hamtoi habari za ujenzi wa viwanda??
 
Acha aendee tu itasaidia sheria za kwenye ukuta wa mererani kulegezwaaa
 
Huyo Slaa unaye sema aliuliza kama ni asset au liability, Je umejipa muda ukajiuliza yeye yuko wapi?
 
Hii biashara haiwasaidi lakini kwa aibu hawawezi kuiacha maana watachekwa (wataulizwa imeleta tija gani) hivyo watajitutumua tu kuendelea nayo kuliko ku-surrender.

Eti hawa ndio watu wa kuipeleka Tanzania kufikia katika uchumi wa kati!!

Wabongo mtasubiri sana!!


Pole, kwisha habari yako. Una invest katika watu usiowafahamu na kujiwekea tumaini kwao? Subiria magonjwa ya kujitakia yasiyo ya kuambukiza.
 
Swali la wapi ruzuku ya chama inaenda limekuwa gumu sana kwa mbowe .

Yupo tayari atumie mwezi mzima kuwaelezea bavicha namna ccm inavyonunua watu badala ya kutumia dakika moja kueleza kwa nini ruzuku ya chama haifiki wilayani.
Uliwahi musikia mwenyekiti wa ccm mpambana na rushwa mwanzisha mahakama za kifisadi akizungumzia 1.5 trilion? Ujue alizipiga sasa ndo anazitumia
 
Back
Top Bottom