Tetesi: Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya kuhamia Chama cha Mapinduzi muda wowote kuanzia sasa

Tetesi: Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya kuhamia Chama cha Mapinduzi muda wowote kuanzia sasa

We unashangaza kweli!!Wakati wanakuja CHADEMA walikuwa wanajiuzulu nafasi zao na kupelekea nchi kuingia kwenye uchaguzi?
Wewe una matatizo kwenye mtindio. Yaani hujui wanachokifanya kama ni Uhuru wa kikatiba? Jitafakari.

Wewe hutakiwi kubeza uamuzi wao bali kupitia mbunge wako mwambie aandae hoja binafsi apeleke bunge lijalo ili sheria hiyo ndani ya katiba ifanyiwe marekebisho. Ila kwa sasa unakuwa kituko kwani mtu yupo huru kuamua
 
Hii biashara haiwasaidi lakini kwa aibu hawawezi kuiacha maana watachekwa (wataulizwa imeleta tija gani) hivyo watajitutumua tu kuendelea nayo kuliko ku-surrender.

Eti hawa ndio watu wa kuipeleka Tanzania kufikia katika uchumi wa kati!!

Wabongo mtasubiri sana!!
Machadema kumbe siyo ya kuaminiwa kabisa!

Kwamba yanajiuza na kununulika kirahisi hivi?
 
Hawa madalali wa hii biashara wamewaaminisha wabunge wa upinzani wanaowahitaji kuwa watawateu kugombea na ushindi ni wa hakika kwa sababu si kazi ya wapiga kura kuamua nani awe mwakilishi wao; ni kazi ya NEC isiyo huru.

Faida wanayoipata ni kupunguza upinzani bungeni kama sehemu ya mchakato wa kuua upinzani kabisa. Elimu ya uraia kwa watanzania inahitajika sana vinginevyo awamu hii ya tano upinzani utarajie anguko kuu.

Ushauri: upinzani usishiriki kwenye chaguzi ndogo zote zijazo isipokuwa kwa ajili ya kupata fursa ya kuzungumza na wananchi kwa ajili ya kuwaelimisha na kujipatia wanachama wengi.
 
Si huwa mnajisifu humu kwamba watu wa kaskazini mnajitambua.
Sasa haya yanayotokea yanawavua nguo.

Kuna mzee mmoja aliniambia wafrika wote akili zao zinafanana. Uende west east north au south wote sawa tu.
Hao wale wachache wachumia tumbo wanaangalia maslahi ya matumbo yao yao. Hakuna mtu anayejitambua anayeuza thamani ya utu wake
 
Hii biashara haiwasaidi lakini kwa aibu hawawezi kuiacha maana watachekwa (wataulizwa imeleta tija gani) hivyo watajitutumua tu kuendelea nayo kuliko ku-surrender.

Eti hawa ndio watu wa kuipeleka Tanzania kufikia katika uchumi wa kati!!

Wabongo mtasubiri sana!!
Kweli mkuu mabenki yanafilisika wao wako kwenye soko ka wabunge na madiwani wa cdm
 
Teh mkuu mbona unaumia kusikia watanzania tupo imara na chadema? Vumilia tu mkuu chadema inapendwa hutaki jiue kununua viongozi haitasaidia kuitenga na sisi wananchi.
Chadema ndo inazidi kumairika wachumia tumbo wataondoka wote
 
Back
Top Bottom