Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea atangaza kujiuzulu Ubunge na uanachama wa CUF

Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea atangaza kujiuzulu Ubunge na uanachama wa CUF

Makubaliano mwisho ni kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo hilo. 2020 kila jicho litajililia, hakuna namna
Mkuu,ingekuwa hivo wasinge hama.. kumbuka mbunge wa upinzani kurud bungeni 2020 ni muujiza. ..

Hivo anaye hamia huko ana uhakika wa kugombea hilo jimbo 2020,
Pia asipo pewa hyo nafasi kuna fursa nyingi za teuzi,.

Hakuna kinacho itwa CCM asilia saiv,labda siku za nyuma.kura ya maoni hakuna saivi ndani ya CCM.

Magu ndo Final
 
Magu ndio final wakati huu wa kujiuzulu lakini kipindi cha uchaguzi mkuu wote walio tokea upinzani kwa kujiuzulu watalia na kusaga meno. Kwani watamfanya nini hata asipo warejesha bungeni kwa nguvu(na itakua hivyo)
 
Endelea kuota
 
Poleni watumishi,hakika fanyeni hujuma indirect dhidi ya serikali hii onevu kwenu.
 
Mbunge wa Temeke kwa tiketi wa Chama cha Wananchi (CUF) Abdallah Mtolea ametangaza kujiuzulu ubunge na nafasi zake zote za uongozi ndani ya chama hicho kuanzia leo Novemba 15, 2018.
MTOLEAPIC-730x375%402x.jpg

Akiyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma, Mtolea ameeleza kuwa, kwa muda mrefu sasa ndani ya chama hicho kumekuwa na mgogoro wa kiungozi ambao haufikii mwisho.

Baada ya kutangaza uamuzi huo, Mtolea alitoka nje ya ukumbi wa Bunge.

Kujiuzulu huko kwa Mtolea kunakuja ikiwa leo ni siku ya mwisho iliyotangazwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa, ni mwisho wa kuwapokea wabunge na madiwani kutoka upinzani ambao watapewa nafasi za kugombea tena.

Uamuzi huo ulifikiwa katika Kikao cha Kamati Kuu Maalum jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti Rais John Magufuli.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, baada ya leo (Novemba 15) wabunge na madiwani watakaoomba kujiunga na CCM watapokelewa na kubaki kuwa wanachama wa kawaida.

“NEC imeelekeza kuwa tarehe 15 Novemba ndio itakuwa mwisho wa kupokea maombi ya uanachama wa CCM na kupewa dhamana ya uwakilishi kupitia tiketi ya CCM kwa wabunge na madiwani kutoka vyama vingine,” alisema Polepole na kuongeza:

Lakini tofauti na wabunge wengine wa upinzani waliojiuzulu, Abdallah Mtolea hakueleza kama atajiunga CCM ama la.

-swahiliTIMES
 
Hata mimi nangoja kununuliwa ndio nihame, lakini yaonekana bei yangu wamesidwa, maana mimi nataka foreing currency sio hizi hela zetu , mimi nataka mamilioni ya dola, na ndio jiwe amesidwa kuninunua
 
Hii inaitwa Win Win Situation 😀 . Niliisha sema Atakae bakia Upinzani basi akili yake sio timamu .
 
Wakati leo ni tarehe ya mwisho kwa wanaotaka kuhamia CCM, huku kwingine dirisha dogo la usajili limefunguliwa rasmi leo. Sijajua Yanga wanamsajili mchezaji gani mwingine, maana nasikia Ajibu anasepa zake!
 
Ata hivo Cuf ina mgogoro wa muda mrefu ila Kwa nn ahame Leo Kwann asihame kesho
 
Nachukua nafasi hii kuwapongeza wabunge wote wa upinzani walioipa umuhimu taarifa ya dirisha dogo la usajiri kufungwa leo na wengine kuhakikisha wanajiuzulu wakiwa ndani ya Bunge waki "abandon" majukumu ambayo walikabidhiwa na wananchi.

Nina imani kwa wale ambao bado hawajaonyesha "uzalendo" wa kuhamia CCM watafanya hivyo kufikia saa tano na dakika tisini na tisa usiku wa leo. Kuanzia kesho tutasubiria wale watakaoonyesha "uzalendo" wa kweli kwa kuhamia CCM bila kuhakikishiwa kugombea tena nafasi hiyo hiyo waliyoikataa.

Bwana Apewe Sifa!
 
Back
Top Bottom