Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea atangaza kujiuzulu Ubunge na uanachama wa CUF

Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea atangaza kujiuzulu Ubunge na uanachama wa CUF

Kwa wale amabo huwa mnapitapita vijij vya ndani ndani huko (vijiji vya Chato inclusive) ukaona jinsi binadamu anavyogombania maji na ng'ombe/mbuzi kwenye madimbwi halafu unasikia pesa inatumika kuonga wapuuzi fulani na kurudia uchaguzi kwa upuuzi fulani tu....Wakati mwingine unatamani hata kujitoa muhanga ila ukifikiria kuna wanaokutegemea unasonya tu na kukaa kimya...Inatia hasira sana basi tu...
 
Eti hawa akina Mtulia ndio watanzania wanawategemea kama Think Tanks wa kuleta fikra mpya ili nchi ijitegemee. Bogus and Hopeless.
 
Tutakutana 2020 hawa wanacheza na Wananchi..

Watu walikupambania mpaka ukafika Mjengoni leo unakuja na hoja dhaifu namna hiyo.

Wakati Mwingine ni ujuha tu na uzuzu kuchezea pesa za walipa kodi.
 
hakutakuwa na dirisha dogo la usajili?
wafikirie kuwa ktk usajili kuna fursa ya dirisha dogo
 
Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdallah Mtolea wa Chama cha CUF ametangaza rasmi kujivua uanachama wa chama hicho pamoja na kuachia nafasi yake ya Ubunge kuanzia hivi sasa.

Mtolea ametangaza uamuzi huo bungeni jijini Dodoma hii leo Novemba 15, 2018 ikiwa ndio tarehe ya mwisho iliyowekwa na CCM kwa viongozi wa vyama vingine wanaotaka kuhamia CCM na kupewa dhamana ya kutetea udiwani na ubunge wao kwa tiketi ya chama.

View attachment 935115
Abdallah Mtolea akitoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kutangaza kujiuzulu Ubunge​

Soma pia: CCM yatangaza leo ni siku rasmi kufunga milango kwa wanaotaka kuhamia kutoka vyama vya upinzani - JamiiForums

For the English Audience ​

Temeke Constituency Member of Parliament, Abdalla Mtolea has announced his resignation from his leadership posts within the Civic United Front(CUF) citing that he is not impressed by the internal dispute that has torn the party into two.

Today, November 15th is the deadline for those who want to join CCM and get nominated to represent the party in by-elections as stated by CCM's National Executive Committee in October.

Mtolea becomes the 8th Opposition Member of Parliament to resign from his post since the 2015 General Elections.

Kuna nini kwenye siasa? Kila anaeaminiwa na wananchi anawatelekeza kama makinda ya njiwa
 
Nashangaa watu wanaona hili ni jipya! Mbona siku nyingi tumeieleza hii 'biashara'

Wanaohama hawana sababu, wana visingizio tu.

Mtolea siku zote hakuona tatizo ndani ya chama chake, eti ameliona baada ya Deadline ya CCM ya tarehe 15 November! Bado watu wanaamini matatizo ndani ya vyama ndiyo sababu

Yeye haku-photocopy ile barua 'standard' yenye neno ''Kujiuzuru' iliyotumiwa na kila mmoja

Manunuzi yana namna zake , Pascal Mayalla umeamini sasa!

JokaKuu
 
Nashangaa watu wanaona hili ni jipya! Mbona siku nyingi tumeieleza hii 'biashara'

Wanaohama hawana sababu, wana visingizio tu.

Mtolea siku zote hakuona tatizo ndani ya chama chake, eti ameliona baada ya Deadline ya CCM ya tarehe 15 November! Bado watu wanaamini matatizo ndani ya vyama ndiyo sababu

Yeye haku-photocopy ile barua 'standard' yenye neno ''Kujiuzuru' iliyotumiwa na kila mmoja

Manunuzi yana namna zake , Pascal Mayalla umeamini sasa!

JokaKuu
Mkuu Nguruvi3, mimi bado ninaamini, kila anayehama ana sababu, hata kama sababu yenyewe ni ile rushwa tuu ya ahadi ya kusimamishwa tena, nayo ni sababu tosha. Hata kama ni fear of unknown kwa hatma ya upinzani 2020 ni sababu.
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums

Ila pia kuna wahamiaji wengine ni very genuine, wakati wanahana wanaandika barua kwa vyama vyao na wanatoa sababu, nilishauri, hawa wasipuuzwe wana hoja za msingi.
CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike - JamiiForums
P
 
Amechelewa sana ata hivyo hongera sana kwake ila bado hamtutoi kwenye koroshow maana tunabanana mpaka tujue korosho jiwe ataziuza wapi kwa bajeti ipi?
Kasema tutazibangua zote na kugawia wananchi milioni 30 takirbani kilo mbili mbili kama atakosa mnunuzi.
Magu katika ubora wake atakuwa anatengezea lishe wananchi ni muhimu kuliko hata kuziuza
 
Ukawa ndio umeshasambaratika
Hao kina mnyika na kubenea wanasukuma siku ziende tu
 
"Pascal Mayalla, post: 29224648, member: 17813"]Mkuu Nguruvi3, mimi bado ninaamini, kila anayehama ana sababu, hata kama sababu yenyewe ni ile rushwa tuu ya ahadi ya kusimamishwa tena, nayo ni sababu tosha. Hata kama ni fear of unknown kwa hatma ya upinzani 2020 ni sababu.
Nakubaliana nawe kuhusu uwepo wa sababu za aina yoyote ile.
Mkuu P

Sikubaliani nawe pale wanapofanya matatizo ya vyama kama ndiyo sababu.
Huu ni uongo, usemwe na usivumiliwe.

Wao ni raia huru wanaweza kuhama bila kusema lolote na hawana kosa

Leo Mtolea aliyeishi na CUF kuanzia inaparaganyika , inagawanyika, account zina matatizo, wabunge wanafukuzwa na kupandikizwa, makao makuu hayajulikani, kwa muda wote huo hakuona tatizo na kulisema ndani ya chama chake. Alichukua upande kulinda ubunge wake

Leo tena baada ya deadline ya CCM anatangaza kuhama eti kwasababu za CUF

Huu upuuzi usiendekezwe hata kidogo.
Tutakuwa na taifa la watu wajinga wajinga, wakilifanya taifa lote ni la wajinga.

Mtolea ahame tu ana haki zake za kisheria. Ana haki za kuitisha mikutano na kueleza, ana haki za kutosema. Hana haki ya kupandikiza uongo unaotokana na masilahi yake kama suala la kitaifa
Ila pia kuna wahamiaji wengine ni very genuine, wakati wanahana wanaandika barua kwa vyama vyao na wanatoa sababu, nilishauri, hawa wasipuuzwe wana hoja za msingi.
Katika waliondoka hakuna genuine hata mmoja.

Kiongozi genuine ni yule anayesimama kuhesabiwa wakati akiwa ndani ya chama chake.
Hata kama anafukuzwa, lakini kama ana anachosimamia huyo ni genuine

Hawa wengine wanaoandika barua mbili, ya kwanza kulaani vyama vyao na ya pili ni ile iliyoandikwa Lumumba 'standard letter' yenye maneno ya ''kujiuzuru' si genuine hata kidogo

Hakuna anayejiuzulu na kukaa pembeni, wakijiuzulu wanaomba, wanateuliwa wanarudi Bungeni kutetea kile walichoaminisha hakikuwa sawa. Yaani siku moja mtu anakuwa si yule

Mku Pasco kijiko ni kijiko tusiite kijiko kama beleshi au chepeo, ni kijiko tu

Kwa upande mwingine, hili ni jambo lenye faraja.
Ni heri ya wapinzani watatu wanaosimamia na kuamini wanachokisema kuliko kundi lisilojielewa linaloishi kwa kutegemea allowance. Kundi lisilo na masilahi na nchi bali masilahi yao binafsi
 
Back
Top Bottom