Mbunge wa Uganda, Brian Kipyagon, amezua mjadala baada ya kuonekana kwenye video akimfanyia kampeni Rais William Ruto kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Kenya wa 2027.
Katika video hiyo, Kipyagon anawasihi wananchi kumuunga mkono Ruto na hata kudai kuwa Waganda wanaweza kuvuka mpaka kuja Kenya kumpigia kura.
Kauli hiyo imeibua maswali kuhusu ushiriki wa viongozi wa kigeni katika siasa za Kenya pamoja na masharti ya kisheria yanayowabainisha watu wanaostahili kupiga kura nchini.
Huku uchaguzi wa 2027 ukikaribia, shughuli za kisiasa na kampeni za mapema zimeanza kushika kasi.
Una maoni gani kuhusu mbunge wa Uganda kumfanyia kampeni mgombea wa urais nchini Kenya