Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara(CHADEMA) ajiuzulu na kuhamia CCM

Zitto leo anamkosoa Mwita Waitara,amesahau na yeye alihama Chama na kuanzisha Chama chake cha ACT kwa sababu kama hizohizo alizozisema Waitara,yeye aligombana hivohivo na Mbowe kisa tuu kutaka kugombea Uenyekiti leo anamponda Waitara kweliiiii!???.
 
Hongera zake
 
Mimi naona kichekesho hapa. Unapokuwa Upinzani maana yake unaamini itikadi ya chama chako ni bora kuliko chama tawala. Sasa kukosana na viongozi wenzio, kunageuzaje itikadi ya chama tawala kuwa bora mara moja hadi kuhamia na kugombea nafasi hiyo hiyo ya Ubunge?
 
Tanzania ya kiwanda cha ajira ni Chadema. Tulikuwa tunaambiwa Tanzania ya viwanda itatuletea ajira. Kumbe nimegundua kiwanda cha ajira Tanzania ni kimoja tu, ni Chadema. Ukiwa ndani ya kiwanda hiki utapewa ajira yoyote uitakayo. Shahidi ni Katambi na wenzake lundo. Sasa wanakula kuku kwa mrija. Hongera walioanzisha kiwanda hiki kikubwa cha ajira Tanzania.
 
huyu huaga ni kichaa..alipo shindwa uchaguzi huku tarime alichangisha kwa wananchi pesa kwa ajili kufungua kesi...alitoroka nazo ndipo tulipo mjua huaga hazimo na hata yeye alijua wananchi wamemjua huku ndo kuhamia huko aliko...ni goodplyer wa siasa hata nyie ccm mumuangalie kwa jicho la upande
 
Sio lazima watu wafuate maono yk
 
Huyu jamaa nimemsikiliza ........... is TOO NAIVE.
 
Siyo jambo jema kwa binadamu kuwa na bei,hasara ni kubwa kwa taifa kwa ulilofanya,2020 tuonane,huo ndiyo mwisho wako kuonekana kwenye ubunge au udiwani,unaota uwaziri,ukuu wa mkoa/wilaya labda
 
Kila ka kheri huko unakokuita kwa ukweli. Umewaangusha wananchi wako. Tunaamini watu wa kabila lako ni majasiri lakini wewe umekubali kuwa bidhaa ununuliwe.
 
Watabaki watu OG tu, then hapo ndipo mambo yatakapoanza kuwa mazuri. Kwahyo wanafiki wote wakisepa wakijidai eti ruzuku sjui uenyekiti haina shida. Kama yeye kahama akiwa mbunge hata angekuwa mwenyekiti si angehama hvyohvyo tuuu. Na tusidanganyike hakuna mtu atakaye acha mshahara wake mkubwa kila mwezi af ajidai anamuunga fulani mkono
 
Any way Ngoja tusubiri aweke sababu why kafanya Hivyo,nakumbuka huyu alihamia chadema akitokea CCM na akimlaimu makamba na Chimbi,tena alihama CCM katikati ya uchaguzi mdogo jimbo la Tarime.
Aanzishe tu chama chake kama vipi, mana Leo sisiem hawafai bora chadema kesho chadema nao hawafai... sasa ukirudi unaelewekaje kama sio mfia tumbo

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…