TANZIA Mbunge wa zamani, Nimrod Mkono amefariki dunia nchini Marekani


Hao wanawake wawili hawana watoto wa marehemu?
 
Hiyo Familia naijua kwa 100% na yaliyokuwa yakiendelea nayo nayajua kwa 100% vile vile na ndani ya hilo Jumba nimeishi sana na Kucheza mno na Mwanae Mkono Junior au Walter ( wenyewe Watu wa Oysterbay na Masaki ) enzi hizo tulikuwa tukimuita Mkono Mental.

Na hata hao Wadogo wa Marehemu Mzee Zadock Mkono na Dokta Japhet Mkono ni Watu wangu wa Karibu, hivyo ukiona nadondosha tu Comment hapa ichukue na iamini tena kwa 100% sawa Mkuu?

Mimi ndiyo MINOCYCLINE The Great!

Cc: Bujibuji Simba Nyamaume na Dr Matola PhD
 
Nilishangaaga sana niliposikiaga mkono analelewa kwenye kituo cha
Wazee huko marekani,nkajiulizaga hivi watoto wake,familia waliridhia...au ndiyo ilikuwa style tu mkakati

Ova
 
Hao wanawake wawili hawana watoto wa marehemu?
Alizaa nao na kuna Mmoja namuona anazurula sana Mitaa ya Mbezi Beach Corner Bar Kijiwe cha Rafiki yake mkubwa GENTAMYCINE hapa JamiiForums aitwae Bujibuji Simba Nyamaume na kuna muda anaonekana Kawe na Msasani.

Huyu Mtoto kwa Sasa ukimtizama Kisaikolojia ni kama vile Ameshadata na nakumbuka kila nikionana nae anachokisema ni kwanini Watoto wa Marehemu Mzee Mkono walikuwa hawamtambui na hawamjali na kwamba Siku Mzee Mkono akifa ( kama hivi sasa ) atauwasha Moto.

Na hapatani kweli kweli na Leah.

Cc: Dr Matola PhD
 
Nilishangaaga sana niliposikiaga mkono analelewa kwenye kituo cha
Wazee huko marekani,nkajiulizaga hivi watoto wake,familia waliridhia...au ndiyo ilikuwa style tu mkakati

Ova
Mwanzoni alikuwa akiishi kwa Bintiye Mirembe huko nchini Marekani na muda mwingine Bintiye mwingine Dokta Wambura aishie nchini Uingereza nae akawa anaenda Kumtumza na Kumuona Baba yake.

Cha Kushangaza Leah na Mama yake na Kushirikiana na huyo Mbunge ( EK ) aliyezaa Kimkakati na Leah wakaamua Mzee Mkono akatunzwe Kimasikini katika Kambi ya Wazee Wasiojiweza ili wapate Urahisi wa Kupiga Fedha zake ambazo Leah alifoji baadhi ya Nyaraka na Kudanganya Watendaji baadhi wa Serikali na Fedha zote zikawa zinaingia Kwake na anazifuja tu hovyo mpaka sasa Amefilisika na anahaha kutaka Kuuza Mali za Baba yake ambazo zingine hata hivyo hazijui na najua baada ya wanaozijua kusikia Mzee Mkono Kafariki kuanzia leo Watajimilikisha rasmi.

Cc: Dr Matola PhD
 
Huyo L anaonekana mbinafsi na kaingiwa na tamaa

Ova
 
Pole sana ndugu , najua ni kiasi gani huu msiba umekuumiza , nitamkumbuka huyu mzee leo na kesho maana nina mengi ya kumshukuru .
 
Duh,ila hiyo ya mkono kuwekwa kituo cha kulelea wazee marekani iliniacha
Hoi,na hyo nlisikiaga muda sana kutoka kwa wazee fulani wanazungumza,wao wenyewe walikuwa wanashangaa

Ova
 
Huyu mwamba mwaka 2005 wakati HELB inaanza alikopesha wanafunzi wooote nchi nzima akiwa mwenyekiti wa Board. Mi nikiwa 1st yr😇😇😇.



Ufu 14:13 SUV

Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

pumzika kwa amani umechangia mi kuwa hapa.
 
Kwa tunaomfahamu Mkono tunapatwa na maswali zaidi kuliko majibu.

Kwa mtu msomi na Wakili nguli kama Nimrod Mkono inawezekana vipi asiwe na willing ya Mali zake kwa advocate wake? Kumbuka hata Lisu ni Wakili nguli lakini ana Wakili wake.

Kuna sintofahamu nyingi sana ya maisha ya mwisho ya Mzee Mkono, otherwise mniambie basi kuna uchawi wa Gambia wameutumia mama na bintiye kumgeuza msukule Mzee Mkono.

Lakini swali linabaki, je inawezekana vipi kwa wakili nguli kama Nimrod Mkono hana willing ya Mali zake?

Brother Pascal Mayalla hebu tusaidie hapa views zako, Mimi Niko confused.
 
Butiama hii hii au? maendeleo gani yapo Butiama uanze kumsifia mtu?
 
Nimekomaa nasoma kwa umakini kumbe ni wewe Gentamycine ndio umeandika hapa? Huyo binti Leah licha ya kuwa mke wa mbunge ana nguvu gani nyingine kiasi che kuweza kuwaweka wakubwa wa serikali,ndugu zake na vyombo vya dola mfukoni? Huyo Leah ni nani haswa aweze kupanga mambo makubwa hivi dhidi ya baba ake katika dunia hii ya utandawazi na akakosa mtu wa kumchallange?
 
Butiama hii hii au? maendeleo gani yapo Butiama uanze kumsifia mtu?
Inategemea kwako maendeleo ni nini?

Wengine mkipewa ubwabwa na kofia ni maendeleo tosha kabisa.

Mkono ameongoza jimbo la Musoma vijijini na baadaye likazaliwa jimbo jipya la Butiama Mkono akabaki Butiama Profesa Sospeter Muhongo akachukuwa Musoma vijijini.

Sasa majimbo yote haya mawili wakazi wake ni wakulima na wafugaji, je unayaelewa mahitaji yao ni nini? Je Mkono alifanya au hakufanya?

Njoo kwa takwimu nione kama una akili, usidhani maendeleo ni maukumbi ya disko na mahotel ya kisiasa, hiyo siyo kazi ya mbunge, hilo ni jukumu la wazawa kuwekeza kwao.

Na ukitafuta tatizo la Wazanaki kutowekeza kwao source ni Nyerere hakupenda maendeleo na hakutaka asili ya vijiji ibadirike lakini yeye Butiama alijenga ghorofa siku nyingi tu Mwitongo.

Na hapa ndipo kwenye source kwa nini mbuga ya Serengeti ipo mkoa wa Mara zaidi lakini manufaa makubwa wananufaika Arusha.

Hawa watu maarufu unaowasikia, Wassira, Warioba, Butiku, Musuguri na wengine wengi wote wana nyumba tu za kawaida za makazi maeneo yao mkoani Mara, Hakuna hata mmoja aliyewekeza chochote wote waliufyata kwa Nyerere wakaishi maisha ya kawaida.
 
Mkuu sijisikii kuandika sana tafadhali,nipo Butiama wakati naandika comment hii,tuna miezi mitatu maji hayapatikani bombani. Kama hali hii ninayoona butiama inakufanya umsifie Mbunge aliyepita kwa maendeleo tuishie hapa. Sina takwimu. Na-Edit kuongeza comment..
Mkuu Butiama sio tena ya wakulima na wafugaji kama ulivyosema. Chuo cha kilimo kitaleta wanafunzi hapa mwaka huu,kuna wafanyakazi wa halmashauri,hospital ya wilaya na zahanati za pembeni,shule za msingi na sekondari,kambi za jeshi,vituo vya polisi na magereza,hizi taasisi zote zinaleta wafanyakazi Butiama,je unadhani mahitaji ya wakulima na wafugaji yanawatosheleza na kundi hili?
 
Mkuu sijisikii kuandika sana tafadhali,nipo Butiama wakati naandika comment hii,tuna miezi mitatu maji hayapatikani bombani. Kama hali hii ninayoona butiama inakufanya umsifie Mbunge aliyepita kwa maendeleo tuishie hapa. Sina takwimu.
Mkono ameondoka Tanzania akiwa mgonjwa mwaka 2018, hujui unachokiandika, sasa hivi kuna mbunge mwingine tangu mwaka 2020, huyo ndivyo yupo responsible kwa hicho unacholalamikia.

Pita Kwa wanavijiji waulize Mkono alikuwa mtu wa aina gani watakwambia siyo wewe wakuja uliyepata ajira ya halmashauri mpya ya Butiama umekwenda hapo kikazi, huwezi kumjuwa Mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…