TANZIA Mbunge wa zamani, Nimrod Mkono amefariki dunia nchini Marekani

Mbona Chuki / Usununu hivi? Alikudhulumu chochote kile labda ili Wanawe ( hasa Uncle's ) wake tukurejeshee?
 
Masahihisho kidogo siyo zote zina Majina ya Machifu kwa mfano ile ya Oswald Mang'ombe ( Baba yake Mkubwa mwana JamiiForums mkubwa, machachari na maarufu mno hapa ) hakuwa Mtemi ila alikuwa ni Mtoto wa Mtemi wa Watuguri Mang'ombe ( Omary ) Isyesya.

Huyu Oswald Mang'ombe ndiyo alikuwa Rafiki mkubwa wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere mpaka kufikia Kuamua kuwa na Undugu wa Kuchanja Damu na ndiyo maana hata huyo Member maarufu, mkubwa na mtata hapa JamiiForums ameishi mno Ikulu na Msasani enzi za Mwalimu Nyerere kutokana na hii Historia ya huu Undugu.

Na huyu Oswald Mang'ombe ( Archtecturer by Profession ) ndiyo alikuwa Mkuu wa Mkoa ( zamani Area Commissioner ) wa Mbeya.

Marehemu Mzee Mkono aliamua kuiita Jina lake hiyo Shule kwakuwa tokea Yeye ( Mkono ) akiwa Mdogo alikuwa akiona Utendaji mkubwa wa Oswald Mang'ombe na alivyokuwa akipambana Kuwaendeleza hasa Kielimu Wazanaki wa Butuguri, Busegwe ( Kwao Mzee Mkono ) na hata Butiama kwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

Cc: Bujibuji Simba Nyamaume
 

Nimrod Elirehema Mkono tutamkumbuka kwa mema yake mengi, apumzike kwa amani mahala pema peponi
 
Nimrood Elirehema Mkono
Mkono Kwa Mkono
Mbunge Wangu 2000-2015 Mpka alipokuja Prof Muhongo 2015-2020
2005 nikiwa namaliza la 7 aliitembea shule yetu ... Alikua anaongea Sauti yake ndogo sana afu kama Ina kimkwaruzo anavalia tarbush na kaunda au Kisela tu jinsi na magari ya kutosha afu ana macho mekundu sana ....
Ila anatoa misaada sana hasa kwenye upande wa Elimu miundo mbinu na Afya ...

Alikua na Hela Nyingi Sana
Anatoa pale pale bila Mbamba Mbamba
Next time akaja na Mh Jakaya...
Amefanya Mengi sana Mkoa wa Mara ( Nchini)
Aliupenda sana mkoa wa Mara hasa wakati akiwa Mbunge alipenda kulitembea Jimbo lake la Musoma vijijini ( Butiama)
Rest Easy Home Boy .
 
Rest well Mzee Mkono
Pole kwa familia na wote walioguswa na msiba huu
Umesoma kwa makini comments za pacha wa Gentamycine?

Sasa rudi kwenye thread ya Le Mutuz na Neema Ngwilulupi hivi ndivyo alivyotaka kumalizwa Baharia akastukia mchezo mapema.

Hivi tajiri kama Mkono ni wa kwenda kutunzwa nyumba za wazee?

Aisee wanawake mnaupiga mwingi mpaka unamwagika aisee, nimeogopa sana.

Cc: MINOCYCLINE
 

Umeandika nini hapo!?
Halafu tusipangiane vya kuandika
 
R.i.p taikon wewe ni jabali la siasa za bongo....
Japo wew ni CCM ila uliona potentiality za wanasiasa wa upinzani na uliwapa TAG...
NIMROD MKONO JUHUDI ZAKO ZA KUWAPAMBANIA WATANZANIA NA WANA MUSOMA HAZIWEZI SAHAULIKA DAIMA.....
Pumzika Baba sote safar yetu ni Moja.....
UFUNUO 14:13 tunapata faraja kupitia hili andiko.....

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
Licha ya maradhi, kwa mwaka huo, isijekuwa pia alimkibia bwana yule.
Yule shetani alikuwa na uwezo wa kufanya ushetani wake wote lakini siyo kumgusa Mkono ambaye ana mahusiano ya moja kwa moja na familia ya Mwalimu.

Huwezi kuiongelea Musoma vijijini/ Butiama bila Mkono, hiyo ni vita angekuwa anaitafuta, na unajuwa vizuri ule siyo ukanda wa wazaramo au walugulu, wale watu hawajaribiwi.
 
kweli hapa Nimrod Amenishangaza shule hata moja haina jina lake kama mafisadi na wanasiasa makanjanja wapendavyo kuandika majina yao katika taasisi. kwa Advocate Mkono ni tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha, eti Hadi mrisho Gambo fisadi wa juzi tuu, kawaibia wahindi kina Tanga general na bulk mavifaa ya ujenzi, nae ana shule inaitwa mrisho Gambo tena ya government
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…