Mbunge wa zamani wa Ndanda Cecil Mwambe amesema ameitwa jijini Dodoma na Spika Ndugai

Diwani ambaye anatambuliwa na chama chake anakataliwa kwa barua ya kufoji, mbunge ambaye hatambuliwi na chama tena kautangazia umma kuwa yeye siyo Chadema tena anaitwa mbungeni kwa mbwembwe, shame on them.
 
Ni dharau kubwa sn kwa wananchi
 
Ikiwa tuna viongozi wanaotegemewa kufanya maamuzi katika nchi hii ambao ndio wanaofanya haya >>tukubaliane tu, hatutakaa hata siku moja tupige hatua katika nyanja yoyote ya maisha. Hawa watafanya maamuzi ya kuwanufaisha wao wenyewe hata kama kwa kufanya hivyo inamaanisha kuliingiza taifa hasara.
 
Ahaaaaa. Ameweka na ilani ya chama kwapani.
 
Kuna watu wanashangilia matendo haya ya uvunjifu wa waziwazi wa Katiba na sheria za nchi. Hawajui madhara yake kwa nchi. Kuna siku watakuja kujuta na itakuwa tumechelewa kutatua tatizo. Tutabaki kuomba watu wa nje watusaidie kulitatua. Utawala usiofuata Katiba na shetia mliojiwekea una athari kubwa. Inafikia mahali hata wao (wanaovunja sheria) wanaogopa kutoka madarakani. Tuombe Mungu tusifike huko.
 
Mambo mengine yanatia aibu sana! Huyu mzee kajitoa ufahamu kabisa....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kukuta akilini mwao wanadhani wanawakomoa CDM kumbe wanawaumiza wapiga kura wao, lazima iwe rais anayabariki haya maujinga.
Ukweli ni kua waTanzania wanaowapigia akina Magufuli kura ndiyo wapumbavu wenyewe, ngoja kodi zetu zichezewe.
 
BANANA REPUBLIK...................!!
 
Hivi Sheria na kanuni za uendeeshaji wa Bunge huwa zinawahusu kina nani?Zilitungwa kwa maana gani kama hazikuwa na kazi?
 
Mbunge wa Ndanda kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Cecil Mwambe, amesema kuwa kwa sasa amerejea Bungeni rasmi kumalizia muda wake wa Ubunge kwa kipindi kilichobaki na kwamba yeye ni mwanachama halali wa CCM, hivyo uchaguzi ujao atagombea kupitia tiketi ya CCM Darmpya Blog on Twitter
 
Hii nchi inahitaji MABADILIKO ya haraka ya kiutawala. Hii mambo ya Fisiemu ya kutufanya Watanzania wote hatuna akili, ifikie wakati tuseme INATOSHA!
 
Aisee UKISIKIA dunia imebeba miguu kichwani na inatembelea mikono ndio hii sasa

Jr[emoji769]
 
Aisee UKISIKIA dunia imebeba miguu kichwani na inatembelea mikono ndio hii sasa

Jr[emoji769]
Mnapigwa kwa technicalities za kipuuzi kabisa, hakuna barua yoyote ofisini kwa spika ya huyo mtu kuhama chama hivyo ofisi bado inamtambua.
 
Kwa hivyo Bunge sasa litalipa posho na Mshahara kwa Mbunge hewa!!

Katiba hairuhusu..

Magu ameharibu sana hii Nchi.

Eti tunapambana na ufisadiii..Nyokoooo..

Haya ni maagizo yake 100%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…