Mbunge wangu Mwigulu umeshindwa kabisa!


Ndio maana sisi wengine tunasema huo uwanja wa ndege wa Chato ni matumizi mabovu ya pesa za umma, kwani atakapotoka madarakani ndio itakuwa mwisho wa huo uwanja. Miradi mingi iliyoanzishwa na viongozi kutokana na nafasi zao kimadaraka, mingi ya miradi au biashara hizo za upendeleo, husuasia ama hata huanguka pindi tu viongozi hao wakitoka kwenye nafasi hizo.
 
Aliwahi kuchana bajeti mbadala ya wapinzani bungeni maccm wenzake wakamshangilia sana akajiona boonge moja la genius kumbe ugoro mtupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
in contrary wapinzani kibao wanapita ubunge bila magufuli...

Magu ana bahati kuwa na big name[emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app

Nitajie mpinzani yoyote aliyepata ubunge ama udiwani kwenye chaguzi yoyote iliyofanyika toka Magufuli amekuwa rais. Chini yake ndio tumeona kwa macho yetu mabox ya kura yakitolewa vituoni mbele ya polisi na wasimamizi wa uchaguzi kwenda kujazwa kura za ccm, kisha msimamizi wa uchaguzi kutangaza mshindi aliyepatikana katika mazingira hayo! Chini ya utawala wake ndio tumeshuhudia ofisi zikifungwa ili wapinzani wasirejeshe fomu ofisini ili ccm wapite bila kupingwa. Chini ya utawala wake, ndio tumeona uchaguzi wa nchi nzima viongozi wakipatikana bila kupigiwa kura, na yote ni maagizo yenye baraka zake. Kibaya zaidi ushindi huo wa mezani, umeshangiliwa kuliko hata chaguzi ambazo ccm walikuwa wakishinda kwa kura kabla yake.
 
Ni mbumbumbu tu huyu hana lolote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Education wise he is brilliant, ana 1st class ya Economics from UDSM na aliajiriwa BOT.

P
 
Ni mbumbumbu tu huyu hana lolote

Sent using Jamii Forums mobile app
No Mwigulu sio mbumbumbu ni kichwa sana
P
 

Paskali hapa ni kama unacheza tu na maneno, sio mara moja au 2 umekuwa ukileta hizo trend readings zako kama utabiri. Hilo la kwamba uchaguzi wa mwaka huu wapinzani wanaenda kuwa dumped umelichomeka ili kuupa utetezi wako nguvu.
 
Achana nae alikuwa na jeuri sana alipokuwa anavaa mabendera anakula alichopanda
 

Paskali nimetumia neno competent sio kwa bahati mbaya, najua kuna tofauti ya kupata first class ya hapo UDSM tena wakati ukiwa waziri, na first class ukiwa huna madaraka. Aliajiriwa BoT kweli, lakini hakuwa gavana bali alikuwa staff wa kawaida. Na isitoshe katika mazingira ya hizi taasisi zetu ambazo watu wanapata kazi kwa mbeleko huwezi kupima uwezo wa mtu kwa uhalisia. Nimesema competent kwenye taasisi za kimataifa, nikijua fika huko uwezo ndio nguzo halisi kuliko hizi blabla za hapa nyumbani. Huyo Mwigulu ana uwezo huo au ana vyeti tu?
 
Sawa Mkuu Paskali. Ingawa unakataa unachoandika sio utabiri lkn kwa uelewa wangu naona ni utabiri.
Mtabiri ni sheikh Yahaya, watabiri wanatumia nyota, au ramli etc, mimi ni msoma trends, kusoma trends ni kuangalia tuu mielekeo, mfano leo ni January uchaguzi ni October, nikikuambia kuna uwezekano hakuna hata Mbunge mmoja wa Chedema atakayerudi Bungeni, ikitokea utasema ni utabiri?. No sio utabiri ni trends tuu.

P
 
Nadhana mtoa mada jibu analo.
Mkuu wa Inchi hawako vizuri na Mbunge wetu.
Mkuu wa Inchi ndiye mwenye mamlaka ya mwisho ya Kiserikali kuhusu kuendeleza miradi ya maendeleo.
Mbunge Mwigulu ana conflict of interest na Mkuu wa Inchi kwa sababu Mwigulu bado anautaka Urais kama sio 2020 basi 2025.
Bado kuna maandishi yaliyoandikwa juu ya majabali mengi kando kando ya bara bara za Singida Arusha na Singida Dar kuwa Mwigulu ni Rais 2015. Mwandiko unafanana kwenye majabali yote na hadi leo takriban miaka 4 hayajafutwa.
Kwenye BASI la Timu ya Singida United kwa nyuma kuna picha kubwa ya Mwigulu ambayo inamtangaza Inchi nzima bila kuwekwa wazi kuwa yeye ni mfadhili au mlezi.
Wengi wanatafasiri kuwa hizi nazo ni Kampeini za kuutafuta Urais 2025.
Katika haya yote tumwombee afanikishe ndoto yake ya kuupata Urais ili mradi havunji kanuni na Sheria za Inchi.
Itakuwa ni Heshima kubwa kwa Wana Singida kama Rais atakuwa Mwigulu kwa mwaka 2025.
Kwa mwaka 2020 aungane na Rais wetu wa sasa katika kumfanyia kampeini ili ashinde kwa kishindo katika nafasi yake ya kikatiba ya kugombea Urais kwa awamu ya pili.
 
Kuhusu uwanja wa Chato, I'd like to disagree, kinachofanyika sasa baada ya uwanja ni kuweka sustainability strategies ili kuwa sustainable, utalii ni moja ya mipango hiyo.

Mimi naunga mkono uwanja huu.
P
 

Paskali bana huwa unanichekesha sana, kichwa wa nini, alikuwa mfadhili sijui mdhamini wa Singida United, wakati akiwa waziri hiyo timu ilikuwa vizuri, kapoteza uwaziri timu iko hoi! Yeye kama mchumi anashindajwe kuifanya timu isimame kama timu kwa kutumia elimu yake ya uchumi, bali timu inafanya vizuri anapokuwa tu na madaraka!? Hapa ndio hoja yangu ya kuwa competent inaposimama. Hiyo elimu yake ni kwa faida yake na mkewe. Mimi nimeishia darasa la saba la ukweli, lakini nipe milioni 200, kisha mpe Mwigulu 2b, kisha njoo baada ya miaka miwili uchukue mrejesho. Ili mradi wote tuwe kwenye uwanja sawa wa biashara.
 
Kwa hiyo Zitto amewaiga hao 90% ya wabunge wa CCM wasioonekana majimboni kwao?

Vichwa vya hawa vijana wa ufipa nadhani ubongo wao umechanywa na maji ya ndimu. Huwezi kuhalalisha uhalifu wako eti kwa sababu tu na mwenzio anafanya aina hiyo hiyo ya uhalifu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Paskali inaonekana unazungumza jambo usilolijua au unazungumza kwa matamanio. Jaribu kufanya utafiti wa mapato wa hivyo vivutio vyetu vya utalii kisha utakuja na jibu sahihi badala ya matamanio. Kuwa na vivutio vya utalii ni jambo moja, kuwa na watalii ni jambo jingine. Kama kuwa na vivutio vya utalii ni hoja, Kenya au Rwanda wasingetusogelea kwenye mapato ya utalii. Kama mbuga ya utalii ndio inachangia kuwa na uwanja wa ndege wa 39b, basi huko Selous kulitakiwa kuwa na uwanja wa ndege wa 300b. Paskali tuombe uzima 2030 tuwe hai, miaka mitano baada ya Magufuli kutoka madarakani, iwapo atachaguliwa tena mitano hii, kisha unipe mrejesho wa kitakachokuwa kinaendelea huko Chato.
 
Wamekazania kuyanyima miradi ya maendeleo majimbo ya upinzani.

Hahahaa karma ni hap hapa.

Akina mwigulu hawana uwezo wowote wa kiuongozi wanabebana tu ndani ya chama.
 
Kwahiyo Pasco unataka kusemaje hapa??
 
tindo
Upumbavu uliojitokeza wakati ule kuanzia Lowassa na wafuasi wake na maumivu yake sidhani kama kuna mtu ndani ya Chadema anaweza kuurudia na hata kuuzungumzia tena.
Lakini yote in yote, hakuna kuzungumzia sijui uchaguzi utakuaje au nini, habari iwe tume huru ya uchaguzi tuu. Viongozi wasipotumia nguvu zao kwa hiyo agenda nasi kuwaunga mkono basi nchi imekwisha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…