Mbwa hao ni hatari sana tena sana. Hao ni Pitbull.
Mwenyewe anajuwa kawawekea ulinzi familia yake kumbe ndiyo kawawekea hatari.
Inasikitisha sana.
Kuna jamaa yangu mmoja anao, lakini yeye ana uwezo kifedha, kawawekea watu wa kuwatazama mwanzo mwisho, kuanzia usafi wao, kula yao, mazoezi yao na mafunzo yao.
Anao hao pitbull kama wanane kwake, akitoka au kurudi mtu wa nyumbani kwake wana banda lao la chuma wahudumu wao wanapigiwa simu wawafungie ndiyo atoke au aingie ndani kukatiza yadi yao.
Bila kuwa na pesa za maana iusijaribu kuwafuga hao, kuna siku watakugeukia.
Hao mbwa ni wehu kabisa. Kula kwa wakati wake, kukojowa kwao kwa wakati wake, kunya kwao kwa wakati wake, kukogeshwa kwao kwa wakati wake.
Ukibadili ratiba yao, ushakuwa adui kwao, hawana sijuwi nilisahau. Utakoma kusahau.
Watanzania awashauri msiwafuge hao kabisa, hawana ujanja wala mazowea ya kudumu hao.