Mbwa aina ya Bulldog wajeruhi familia

Mbwa aina ya Bulldog wajeruhi familia

Usiku wa kuamkia leo Tarehe 8/1/2024 majira ya saa Nne usiku Familia ya Ndugu Nicholaus Kunju ilishambuliwa na Mbwa na kuisababishia madhara Kwenye sehemu mbalimbali za miili yao,walio shambuliwa ni Mke wake pamoja na watoto.

View attachment 2865985
View attachment 2867418
Walikuwa Mbwa aina ya Bull dog ambao anawafuga kwa ajili ya ulinzi nyumbani kwake Usagara, Mbwa hao walimshambulia binti yake wakati ametoka nje usiku huo wa saa Nne akiwa amesindikizwa na kaka yake, mara baada ya uvamizi huo kijana mwingine na mama yao walitoka kutoa msaada lakini Mbwa hawakuwatii na kuwashambulia wote.

Wote walioshambuliwa na Mbwa sio wageni kwa Mbwa hao kwani wamekuwa wakiwahudumia kwa chakula, baada Familia hiyo kujinusuru na kukimbilia ndani Mbwa waliendelea kuwa wakali na hapakuwa na uwezekano wa kuwapatia huduma majeruhi kwani hakuna alieweza kuingia wala kutoka ndani ya uzio.

Wakati haya yanatokea Kunju alikuwa kazini zamu ya usiku na alipigiwa simu kujulishwa juu ya tukio huku na kuambiwa mmoja wa majeruhi ana hali mbaya, Tulibahatika kufanya mawasiliano na Polisi kituo cha Misungwi ili waweze kufika eneo la tukio waue Mbwa ili msaada kwa majeruhi Upatikane.

Kwa ushirikiano na Zombwe na Lenox tulifanikisha kumtoa Kunju Kazini ili akashiriki uokoaji. Polisi walifika Nyumbani kwa Kunju majira ya saa saba usiku wakitanguliwa na watu wa Maliasili na wafanikiwa kuwapiga risasi Mbwa wote wawili na Majeruhi wakapelekwa Hospilali ya Cf kwa Matibabu.

Majeruhi wote wanaendelea vizuri, Shukrani kwa wote walioshiriki Kwenye utatuzi bila kumsahau Sheik Abdallah Omari.
Pole sana.
Nimeiona video nyingine kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha mbwa wa aina hiyo wakimshambulia mwanafamilia na ndugu wakijaribu kumnasua bila mafanikio na jamaa kachakazwa balaa.
 
Kibongo bongo tafuta gs wako mfuge haya mambwa mengine ni hatari yanahitaji mtu makini na asie na mambo mengi tunaiga sana vitu ila uwezo hatuna siongelei uwezo wa fedha ila hata mafunzo hatuna sasa balaa kama hilo ni hatari...... Mbwa wazuri sana ila hatari...
 
Mim hawa mbwa koko tu nawaogopa,familia yny mbwa hata km ni rafik zng sana,siitembelei ,naogopa mbwa mno ,sasa sembuse hayo ma bulldog cjui ingekuaje,ningekimbia nyumba,mme angenifata kwetu na watoto
 
Wale ni loaded gun, na Wana wivu sana sana ...na Wana visasi kuliko binadamu. Na hawarudi nyuma kwenye visasi Hata ikipita miaka mingapi watalipiza tu!!! Hawana kitu msamaha!!!
Hii ya wivu nshaiski mahala, kuna jamaa alikuwa analifuga tena sio kwa kulifungia bandani kashalizoea huwa anacheza nalo, sasa maisha yanaendelea akabahatika kupata mtoto hivyo muda mwingi ye akawa anatumia kucheza na mtoto mbwa akawa kampotezea kwa mbali.
Kumbe jibwa linaona wivu lishammaindi mtoto siku wamejiachia limemlia timing likamtafuna mtoto mpaka akafa.
Jamaa akaingia ndani akachukua cha moto akalitwangaa za kichwa likafa.
 
Sikushauri Mkuu Rottweiler sio mbwa wa kutegemea kiusalama ni aggresive sana, likitokea jambo hawezi kufikiri sawa sawa yeye ni kukamata na kurarua, tofauti na German shepherd au Belgian Malinois.

Ushaona wapi jeshi likitumia Rottweiler na ndugu zake kina pitbull, boureboule na bulldog. Marekani na South Africa alijaribu watumia miaka ya 1960/70s ikabuma.

Ni sawa na utumie Chihuahua kwa ulinzi [emoji23][emoji23][emoji23] ni mbwa sawa ila sio mbwa mlinzi.
Hahaha...nimesoma sehemu hawa Rottweiler miaka ya nyuma majeshi-polisi..walijaribu kuwatumia changamoto
1.Ni wakubwa sana na wazito.
2.Bitting force kubwa..walikua wakikamata mualifu..wakiuma mkono.wanavunja mpaka mfupa..damage zikawa kubwa sana..

Kwa michango ya humu naachana na Rott..nabaki na GS....
 
Back
Top Bottom