Mbwa aina ya Bulldog wajeruhi familia

Mbwa aina ya Bulldog wajeruhi familia

Haya si ndiyo yalimwua mwanasoka wa zamani wa Zambia kule South Africa? Mnafuga madude gani haya? Bwana mdogo naye liliwahi kumgeuka bahati yake mafunzo ya kijeshi yakamwokoa akalidhibiti kama anadhibiti gaidi kwenye vita! Ilikuwa hatari sana!
Sio south Africa ni Zimbabwe. Yule jamaa ndio hawa hawa wasiojua kukaa na haya maumbwa alikuwa anaishi nayo kwa namna za hovyo sana.

Alikuwa analeta nayo mizaha ya hovyo na kuyafunza kiburi yakamrudia. Mfano alikuwa na tabia ya kuleta wanyama kama mbuzi halafu anayafungulia yakamate yule mbuzi yamuue in cold blood yaani ile kumrarua mbuzi kiroho mbaya.

Sasa michezo kama ile unayafunza kufanya fujo, kutokuwa na adabu,kuwa makatili, kutokuwa na mipaka na kukosa utii.

Ndio maana hiyo siku alikuwa anayazingua yenyewe yakageuza mchezo kuwa jambo serious yakamrukia na kumuangusha chini yakakamata shingo yakauma hadi alipokata roho.
 
Ndugu sio hao sijui Bulldog/pitbull. Hao ni mbwa wa hovyo kabisa kufuga na anayefuga huwa namshangaa sana. Yaani huwa sijui wanapataga wazimu maana kikinuka hata wewe mfugaji mwenyewe wanakujeruhi kama sio kukuua kabisa. Nikijua una hao mbwa kwako hautaniona milele hata uwe ndugu yangu wa damu siji kabisa. Mbwa gani ukikaa na mwenyeji anakuwa mpole kabisa anachezesha tu mkia kama rafiki subiri sasa mwenyeji ajisahau aingine ndani labda kuchukua simu yake inaita wee akirudi anakuta unavuja damu.
Tena ndani ya dakika tano tu anakuchenjia.
 
Nilipokua.kijana mdogo kwetu nimefuga sana mbwa hawa wa kawaida.Sasa hivi nimekua baba wa familia nimefuga Germany Shephard...jike..ana miaka 2 sasa.Nimekuja kugundua kuna utofauti mkubwa sana nikilinganisha na hawa wengine....yuko composed, hapanick, habweki ovyo ovyo, royal.muda wote anakuangalia straight machoni kama vile anasubiri umwambie kitu.Akibweka mishindo miwili tu mtu wa kawaida lazima a-feel.
Nawaza nitafute Rotweiler dume, nimix
Achana na hiyo takataka pia, huyo Rottweiler ndio binamu na hawa pitbull sio majibwa mazuri. Achana na hiyo breed utakuja jutia. Juzi hapa kamrarua demu wa Master wake sababu ya wivu.
 
Hawa hapa
FB_IMG_17049270810589900.jpg
 
Sio south Africa ni Zimbabwe. Yule jamaa ndio hawa hawa wasiojua kukaa na haya maumbwa alikuwa anaishi nayo kwa namna za hovyo sana.
Basi wewe labda utakuwa unamfahamu mwingine tofauti na huyu wa kwangu ninayemzungumzia. Philemon Mulala alikuwa anaishi South Africa. Soma hicho kipande.
 

Attachments

  • Screenshot_20240111-054927_Chrome.jpg
    Screenshot_20240111-054927_Chrome.jpg
    169.8 KB · Views: 11
Back
Top Bottom