Mbwa wangu anakuwa mkali bila sababu; nataka kumpiga risasi

Mbwa wangu anakuwa mkali bila sababu; nataka kumpiga risasi

Usimuue mpeleke kwa doctor anaweza kuwa na stress . Hali ya uchumi imekuwa ngumu hata vyakula vya mbwa tunAwabadilishia ghafla jamani nao wana hisia kutoka Pedigree hadi pumba na madagaa unadhani atakosa msongo wa mawazo ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Mimi wangu nawafungulia kila siku wakajitafutie chakula wanarudi jioni kama kuku wa kienyeji ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ™๐Ÿฝ
Free range system ๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜‚
 
Pamoja na hayo si haki kutoa uhai wa kiumbe pasipo sababu za msingi,anachopaswa atafute suluhu ya mbwa wake kuliko kumuua,mbwa hawezi kumshinda binadamu
 
Jirani yangu ana mbwa wake amezeeka vibaya mno,amebaki ngozi tu mwili mzima ,hana yale manyoya,na jicho moja limepofuka kwa uzee.lakini jamaa bado anampenda sana mbwa wake ,anasema anangoja Mungu amchukue,hawezi kumuua.wewe una roho mbaya sana,usimuue
 
Naomba ushauri mbwa wangu anakuwa mkali bila sababu anabwekea wapangaji nahisi nitapata kesi kwa ukali wake nyumba yangu haijawahi kuibiwa ila Sasa ukali wake ni too much.

Nimempiga zile sindano tatu wapi bado hakomi (ant rabis) nyumba yangu ni kubwa inawapangaji wengi naogopa siku akikata mnyororo atakula watoto wawatu.

Anachoniudhi Sasa ananibwekea hata Mimi hii inanipandisha hasira mbaya zaidi nasikia mbwa Hali sumu hivyo napanga kumchapa chuma.

Naomba ushauri.

Superbug.
Hahaha aise lazima umpoteze maana mbwa ashajiona ni alpha male mwenye boma huna jinsi lazima apotee tu..
 
Roho mbaya inakusumbua umuue ili iweje?
Hafu nyie wenye nyumba kukaa na wapangaji huwa mna gubu Sana.
Huyo mbwa Hana shida ana tatizo la kisaikolojia inatakiwa umtaftie mtaalamu na huku. Bongo sidhani Kama wapo
uhali gani cariha
 
fanya namna kabla akaume watu bila shaka ni upweke bana
 
MVIZIE HALAFU MPIGE KABALI MOJA KABAMBE BAADA YA HAPO KUNA MAWILI.

1.AKIWA HAI ATAKUHESHIMU
2.ATAKUA MAREHEMU
3.UTAKUA KILEMA

NI HAYO TU NDUGU MTOA UZI
 
IMG_5393.jpg
 
Atakapokukula wewe ndo utajua.

Atakuwa na kichaaa huyo.

Mwenzio alibeba vijiumbwa toka sauzi vikaja mla baba yake.

Shauri zako usije sema hatukukuambia.

by the way........ hicho chuma kinaazimika?
 
Back
Top Bottom