Kushindwa sio kama hujui, mbona wachezaji kibao washawahi kukataliwa na club kubwa ila leo hii wanatamba Mfano Martinelli,hata huyo Nonda Shabani husizani kama ilikuwa directly.
Mfano kwenye mziki Diamond ndiye msanii mkubwa na mwenye mafanikio sababu alijiongeza mapema, anajua soko la ndani na nje linataka nini ,anajua kuubrand mziki wake ,amewekeza ,anajituma nk.Ila haimanishi kwamba anajua kuimba kuliko wote walio tangulia. Ndio maana nikakwambia Samatta aliwahi kujiongeza na si kwamba anatalent kubwa kuliko waliopita ,sometimes kujitambua ndio kila kitu.Hebu mtizame Hajibu leo hii angekuwa anajitambua nahisi hata Chama angeanzia nje, tatizo wachezaji wabongo hawajiogezi na hawajitambui.
Haruna Moshi Boban,Kapombe nk hizi ni talent kubwa sana zilizopata chance ya kucheza nje ila zili shindwa kujiongeza na kujitambua.Hawa wachezaji wa Africa Magharibi unawaona leo na ukubwa wao wamefanyiwa trial nyingi sana na mpaka wametoboa kushindwa trial haimaanishi hujui.