Mbwana Samatta ndio mchezaji bora wa soka wa muda wote Tanzania, GOAT

Mbwana Samatta ndio mchezaji bora wa soka wa muda wote Tanzania, GOAT

Mkuu hao wachezaji wote uliowataja ni average players kama Lunyamila ndio maana hata South Africa hawakuonekana. Samatta alipewa nafasi akaonesha uwezo.

Genk walikuwa wana wimbo maalum kabisa wa Sama goal.

Unaweza niambia Lunyamila kafanya nini kwenye soka? Au unaweza justify vipi Lunyamila ni mwanasoka bora wamuda wote? Chenga nyingi au?
Lunyamila kwa sie tuliomuona ni GOAT
 
Bongo hakuna goat labda wale mbuzi wa ilala.BADO SANA KUWA NA GOAT WETU HAPA BONGO TULIENI KWANZA
 
Story za lunyamila au sunday manara ni ubishi wa kutokubali ukweli. Hawana kikubwa walichofanya kwenye soka kumzidi Samatta.
Nashindwa kuelewa. Watu hawajaelewa thread inasema nini. Hata mimi nakubali kwa Tanzania huyu ndiye mchezaji pekee anayeongoza kwa mafanikio.
 
Poor justification,mbona wenzake walikiwasha
Una uhakika wachezaji wote walionunuliwa na villa wamekiwasha? Akina Shevchenko, Morata, Falcao, Minamino wameflop pale EPL lakini haimaanishi walikuwa au ni wachezaji wabovu na walikotoka walikuwa WA moto. Samatta ni mchezaji Bora WA muda wote Tz. Kathibitisha ubora akiwa Tp mazembe akimuweka benchi Tresor Mputu na kupata mafanikio kibao.Kathibitisha ubora Genk.
Yaani mnataka mchango wa Samatta akiwa taifa stars ufanane na akiwa Genk, Kwa wachezaji gani WA taifa stars?

Haaland ameipeleka wapi Norway? Lakini je ni mchezaji mbovu?
 
Back
Top Bottom