Mbwana Samatta ndio mchezaji bora wa soka wa muda wote Tanzania, GOAT

Lunyamila kwa sie tuliomuona ni GOAT
 
Bongo hakuna goat labda wale mbuzi wa ilala.BADO SANA KUWA NA GOAT WETU HAPA BONGO TULIENI KWANZA
 
makocha wanajinasibu ni bora kwa sasa epl wote kawatungua.

klopp
Liverpool vs Genk uefa champion league.

Pep Gurdiola
Man city vs Aston villa Carabao cup final Wembley.
Kocha bora kwa sasa, EPL ni Arteta
 
Story za lunyamila au sunday manara ni ubishi wa kutokubali ukweli. Hawana kikubwa walichofanya kwenye soka kumzidi Samatta.
Nashindwa kuelewa. Watu hawajaelewa thread inasema nini. Hata mimi nakubali kwa Tanzania huyu ndiye mchezaji pekee anayeongoza kwa mafanikio.
 
Poor justification,mbona wenzake walikiwasha
Una uhakika wachezaji wote walionunuliwa na villa wamekiwasha? Akina Shevchenko, Morata, Falcao, Minamino wameflop pale EPL lakini haimaanishi walikuwa au ni wachezaji wabovu na walikotoka walikuwa WA moto. Samatta ni mchezaji Bora WA muda wote Tz. Kathibitisha ubora akiwa Tp mazembe akimuweka benchi Tresor Mputu na kupata mafanikio kibao.Kathibitisha ubora Genk.
Yaani mnataka mchango wa Samatta akiwa taifa stars ufanane na akiwa Genk, Kwa wachezaji gani WA taifa stars?

Haaland ameipeleka wapi Norway? Lakini je ni mchezaji mbovu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…