Mbwana Samatta uwezo wake wa kawaida Mno, Anabebwa na bahati tu!

Mbwana Samatta uwezo wake wa kawaida Mno, Anabebwa na bahati tu!

Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa Mbwana Samatta Tangu alivyotua katika Club ya KRC Genk ya Belgium akitokea TP Mazembe ya DRC.​
Kiukweli jamaa kiwango chake ni cha kawaida sana na anabebwa sana na bahati kubwa aliyonayo kwani performance yake haitishi sana.​
Ukiangalia magoli anayofunga asilimia kubwa ni ya kawaida sana yasiyo na ufundi (hufunga zaidi kwa kichwa na asilimia kidogo kwa mguu na setpieces).​
Kwa namna soka la Ulaya lilivyokuwa na ushindani hasa kwa mabeki wakatili (kama akina Pepe) sioni Samatta akifanya lolote mbele yao, kwani mbinu zake mguuni hazitishi mabeki na ni za kawaida sana.​
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.....Jamaa some how Anajitahidi na anaendelea kujitahidi kwani ameonesha ujasiri na amekuwa Idol kwa Vijana wengi wenye ndoto za mafanikio kwenye soka kama ya Samatta.​
Kama ataweza kuuona uzi huu au aambiwe na mtu wake wa karibu aliyeko humu basi nimwombe ndugu yangu Samatta, aongeze zaidi juhudi na ajifunze mbinu nyingi za kufunga kwani yeye kama forward kazi yake uwanjani ni magoli tu na si vinginevyo. Bila kisahau Kujisahau na Kuvimba kichwa akuepuke sana kwani magazeti ya bongo yanapamba wachezaji hadi wanakuwa under pressure na mwishowe huharibu carrier yao.​
Mkuu wenzio wamebadilika ila we bado una roho ya kwanini!

Mtapata tabu sana

Kwa hiyo Mumpeleke AJIBU basi[emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lukaku anafunga magoli ya ufundi?... Mwisho wa siku kinachotakiwa ni magoli...haijalishi hata kama yamefungwa kwa mkono au kiuno
Umesema vizuri sana,90 minutes haiangalii ulifunga kwa mkono au kwa mguu,kinachotakiwa ni magoli,tena mfungaji anaefunga goli nyingi zaidi ndio mchezaji bora zaidi,that is football.Genk ni timu kubwa Belgium, yenye mameneja tena waliosomea na kubobea hawatakuwa wajinga watupe pesa kumlipa mchezaji wakati wanajua kuwa ni mtu wa kubahatisha,the guy is talented tuache wivu wa kizamani bana...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NAOMBA KUJUA IVI BIG MATCH ZA LIGI YAO HUWA ANAFUNGA?????????
 
Kwasababu wewe sio kocha wa Genk au timu yoyote ya soka ndio maana umemuona wa kawaida na utaendelea kumuona wa kawaida.
Halafu unaomuona wa kawaida sana na hatishi ukimlinganisha labda na nani anayetisha au ulitaka atishe kwenye nini zaid ili ufikie uamuzi wa kumuona anatisha?
Aliyemsajili anaijua kazi yake na ndiye ayemtuma afanye hayo unayoyaona miguuni mwake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Critical views...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NAOMBA KUJUA IVI BIG MATCH ZA LIGI YAO HUWA ANAFUNGA?????????
huwa anafunga ila kwa kubahatisha yaani timu kama Anderlecht, Na Clube Brugge huwa zinawapa shida sana. yeye anazionea timu kama vile Eupen, Oostende, kortrijk, na Waasland Beveren....ila hapo kwa Anderlecht, Clube Brugge, Standard Liege na Gent huwa wanapata matokeo kwa tabu saana
 
Mleta Uzi ambae unajipambanua kama mfuatiliaji wa match za Samatta me nakuja kukujibu na vitu live maana hiyo Genk wote tunaiangalia na kama kweli unaifuatilia Genk utakuwa ulikuwa unamfahamu Niko Kalleris ambae yeye ndio alikuwa anagombea namba na Samatta amehama msimu huu kaenda PAOK anako kaa benchi,mchezaji mwingine alikuwa akicheza cheza kipindi Samatta yuko bench ni Puzuelo mspain huyu na hao wote nawengine wengi Samatta kawakalisha katika list ya wachezaji waliowahi kucheza Genk na kufunga magoli mengi.Samatta anamagoli mengi kuliko Kevin De Bruyne na Benteke kwa kipindi walichocheza Genk ifuatayo ni jedwali la vielelezo ili ujue why wazungu wanaimba Samagoal.

View attachment 855948View attachment 855951View attachment 855949View attachment 855950
Safi sana, tunataka evidence kama hivyo. Siyo mtu anaeleza hisia tupu bila kuweka facts mezani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom