Mbweni inapendelewa ujenzi wa barabara, Mbezi kwa miaka nenda rudi barabara hazijengwi

Mbweni inapendelewa ujenzi wa barabara, Mbezi kwa miaka nenda rudi barabara hazijengwi

Baada ya kupokea kiinua mgongo cha buku saba zangu nampango wa kuhamia mbweni.

Hivyo acha wafanye maandalizi kwanza, wakimaliza tu nitahamia.
Unafikiri lami zitapigwa mitaa yote
Sana sana barabara zinatoingia na kutoka tu

Ova
 
Sehem kubwa ya ukonga haijapimwa. Unataka serikali iingie gharama ya kuvunja nyumba za watu mje kulalamika hapa kuwa mnaonewa. Anzeni kuvunja nyumba zenu tengeni sehem ya barabara alafu iteni serikali muone kama hamtajengewa lami.
Wewe kweli kukumdogo na ndio maana uwezo wako wa kufikiri ni mdogo pia!
 
Majuzi nimepita Mbweni nikashangaa kabisa.

Barabara nyingi zilizokuwa hazipitiki sasa ni lami tupu.

Najua huu ni mkakati wa viongozi wengi kujipendelea maana wengi wamejenga huko.

Nimepeta tetesi kuwa hata kwa Katinu mkuu Kiongozi, watu wameamriwa barabara iendayo kwake iwekwe lami.

Tofauti na Mbweni, huku Mbezi Beach barabara za kwenda makazi ya watu hazijashughulikiwa kabisa.
Barabara za NSSF Flats
Barabara za Jogoo Cotex
B arabara za Mbezi Tangi Bovu
Barabara ya Mbezi 5 Star
Barabara ya Ndumbwi-Baraza la Mitihani
Barabara za chini Kwa Lukuvi

Ila barabara ya kwenda kwa Kikwete Kawe Beach ilikengwa chap chap!

Huu upundeleo dhahiri wa viongozi kujinufaisha!
Usisahau kuwa Mbweni ni kwa Hangaya mkuu, Hangaya amefumua bonge la mjengo
 
Halafu cha ajabu Mimi
Acha Mbweni ijengwe sana. Kule ndio kioo cha nchi. Tena wanatakiwa kuweka lami kila mtaa. Watu wa kule wamestaarabika sana kulinganisha na sehem zingine. Wanastahili kuwekewa lami na taa za barabarani.
Cha ajabu Mimi nimetokea kupachukia sana mbweni. Yaani sipapendi hata kidogo. Hasa kipindi cha MVUA. japo hata majira ya kiangazi Mbweni hovyoo sana, sijui ni kwanini wakubwa na watu kwenye hela wanapapenda sana Mbweni.

Kwa Dar sehemu ninayoipenda ni GOBA tu hata kama maji ni changamoto
 
Sehem kubwa ya ukonga haijapimwa. Unataka serikali iingie gharama ya kuvunja nyumba za watu mje kulalamika hapa kuwa mnaonewa. Anzeni kuvunja nyumba zenu tengeni sehem ya barabara alafu iteni serikali muone kama hamtajengewa lami.
Kwa hiyo barabara ya bann-kitunda-msongola, au kitunda-magole/mwanagati,pugu majohe,mombasa kwa diwani-bombambili etc zinahitaji kuvunjwa nyumba?-nenda temeke uone mpaka vichochoro vina lami.
 
Obay yenyewe bado kuna barabara ziko ovyo..mfano ile haile selasie Road nk

Ova
ipo kwenye manunuzi mwaka huu wa fedha inarudiwa yote kama ile ya kuanzia coco-sea cliff - makutano ya haile selasie, itaanzia hapo makutano mpaka mataa ya st.peters dah
 
Obay yenyewe bado kuna barabara ziko ovyo..mfano ile haile selasie Road nk

Ova
Haile selassie ni mbovu sehemu walizoruhusu uswahili. Kile kipande chenye bar na vidukaduka kama sinza, kuanzia Puma mpaka kilima nyege ndio kubovu na kuchafu sana.
 
Kwani hujui nani ana makazi yake Mbweni? Kujipendekeza haukishi Tz hii,mwenyewe hata habari hana watu wanahangaika!
Kweli kabisa, lakini ninacho shangaa ni kwa nini hawatengenezi barabara zinazopitia Mbezi.
Old na New Bagamoyo road zinazopitia Mbezi zimejaa kabisa wakati wa rush-hour.
 
Halafu cha ajabu Mimi

Cha ajabu Mimi nimetokea kupachukia sana mbweni. Yaani sipapendi hata kidogo. Hasa kipindi cha MVUA. japo hata majira ya kiangazi Mbweni hovyoo sana, sijui ni kwanini wakubwa na watu kwenye hela wanapapenda sana Mbweni.

Kwa Dar sehemu ninayoipenda ni GOBA tu hata kama maji ni changamoto

Mbweni sehemu salama. Moja liko karibu na kambi za jeshi. Na eneo la mbweni jkt ambalo ndio hot cake lilikua eneo la jeshi wakauziwa viongozi wa kiserikali miaka iyo. Likasaidia kujengwa vizuri maana pesa walikua nazo

Kweli mbweni kipindi cha mvua ilikua inasumbua sana sababu ya kukosa mitaro ya maji. Ila sasa ujenzi wa hizi barabara utasaidia maji yote kushuka chini baharini kule.

Mbweni sahivi inafumuliwa yote na kuwekewa mifumo mipya ya maji. Wanaondoa ya zamani

Mbweni kuzuri anzia jkt kambini panda hadi makutano ya barabara ya kwenda mbweni kwa waswahili
 
Ukweli mbezi ya Kimara imeachwa sana sana pamoja na kuwa Wilaya, sijui kuna nini AU kwa sababu hakuna watu wanene kama huko Mbweni!
 
Mbweni sehemu salama. Moja liko karibu na kambi za jeshi. Na eneo la mbweni jkt ambalo ndio hot cake lilikua eneo la jeshi wakauziwa viongozi wa kiserikali miaka iyo. Likasaidia kujengwa vizuri maana pesa walikua nazo

Kweli mbweni kipindi cha mvua ilikua inasumbua sana sababu ya kukosa mitaro ya maji. Ila sasa ujenzi wa hizi barabara utasaidia maji yote kushuka chini baharini kule.

Mbweni sahivi inafumuliwa yote na kuwekewa mifumo mipya ya maji. Wanaondoa ya zamani

Mbweni kuzuri anzia jkt kambini panda hadi makutano ya barabara ya kwenda mbweni kwa waswahili
Hii Awamu ni ya kujipendelea na wabinafsi sana.
Walio Mbezi wengi wastaafu Awamu ya kwanza na ya Pili.
Mbona karibu na Mbezi kuna Lugalo na Makao Makuu ya JKT, na Range, lakini hakuna barabara za maana.
Tukubali tu kuwa ubinafsi umeruhusiwa Awamu hii
 
Back
Top Bottom