Mbweni inapendelewa ujenzi wa barabara, Mbezi kwa miaka nenda rudi barabara hazijengwi

Mbweni inapendelewa ujenzi wa barabara, Mbezi kwa miaka nenda rudi barabara hazijengwi

Mkuu
Nakumbuka miaka ya mwisho ya 90s na mwanzo wa 2000s kuna wakazi kadhaa wa maeneo ya Kimara nyumba zao zilipigwa X kupisha ujenzi wa barabara serikali ikawapimia viwanja Mbweni kama fidia.

Wakapaona maporini hawakwenda kuviendeleza na wengine wakavitelekeza. Wachache sana walienda kishingo upande. Hao wachache walichekwa saaana. Magu alivyoingia madarakani na kuwabomolea ili kutanua barabara wakaanza kumchukia. Sasa hivi Mbweni pamekua hot cake! Kupanga ni kuchagua.
Mbezi inayo zungumziwa hapa ni Mbezi Beach na sio Mbezi ya Kimara au Mbezi Louis
 
Temeke,kino,magomeni mitaa kongwe
Ilijengwa kwa ramani,mitaa inaingia na inatoka
Ukisema upige mbezi beach yote lami hiyo haiwezekan hata mbweni yenyewe haiwezekani

Ova
Soma vizuri bandiko langu.
Mitaa mikuu nimeiainisha.
 
Nchi hii kuna ujinga mwingi sana pale Tembon kuna lami ilijengwa ikaishia mlangoni kwa boss wa Tanroads

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
Mkuu mchezo ulianzia Masaki.
Huko viongozi wamejiwekea lami mitaa kama yote.
Nyumba walizouziana Masaki sasa wamezipangisha na kuhamia Mbweni, mchezo ule ule!
 
Mkuu mchezo ulianzia Masaki.
Huko viongozi wamejiwekea lami mitaa kama yote.
Nyumba walizouziana Masaki sasa wamezipangisha na kuhamia Mbweni, mchezo ule ule!
Lami yenyewe si imeanza 2000
Kuweka lami eneo lote si masihara
Kwanza kutokana na watu walivyojenga....
Lamizimepigwa barabara zinazotoka na kuingia tu naona

Lami huko labda wangeanza huko miaka ya 80 ndy wangewezapiga sehemu kubwa
Wakati huo barabara zote vumbi tu

Ova
 
Halafu cha ajabu Mimi

Cha ajabu Mimi nimetokea kupachukia sana mbweni. Yaani sipapendi hata kidogo. Hasa kipindi cha MVUA. japo hata majira ya kiangazi Mbweni hovyoo sana, sijui ni kwanini wakubwa na watu kwenye hela wanapapenda sana Mbweni.

Kwa Dar sehemu ninayoipenda ni GOBA tu hata kama maji ni changamoto
Njoo kigamboni boss ubadili kauli yako
 
Majuzi nimepita Mbweni nikashangaa kabisa.

Barabara nyingi zilizokuwa hazipitiki sasa ni lami tupu.

Najua huu ni mkakati wa viongozi wengi kujipendelea maana wengi wamejenga huko.

Nimepata tetesi kuwa hata kwa Katibu Mkuu Kiongozi, watu wameamriwa barabara iendayo kwake iwekwe lami.

Tofauti na Mbweni, huku Mbezi Beach barabara za kwenda makazi ya watu hazijashughulikiwa kabisa.
Barabara za NSSF Flats
Barabara za Jogoo Cotex
Barabara za Mbezi Tangi Bovu
Barabara ya Mbezi 5 Star
Barabara ya Ndumbwi-Baraza la Mitihani
Barabara za chini Kwa Lukuvi

Ila barabara ya kwenda kwa Kikwete Kawe Beach ilijengwa chap chap!

Huu upundeleo dhahiri wa viongozi kujinufaisha Awamu hii!
Sasa kama Mwenyewe umeshasema kuwa Mbweni kunajengwa sana kwakuwa wanaishi Wakubwa unacholalamika hapa ni nini?
 
Na katika kitu Halmashauri ya jiji upande wa mainjinia wa ujenzi wamelala ni kuisafisha mbezi beach na jiji kwa ujumla.

Kuna watu kwa makusudi kabisa wanajenga nje ya mipaka ya viwanja vyao wengine wanaziba njia lakini jiji halichukui hatua ya kuwabomolea. Kwa mfano kuna kigogo mmoja wa makaunda suti pale bahari beach njia panda ya kwenda tegeta nyuki anajenga nyumba za kupangisha appartment nje kabisa ya mawe ya kiwanja yaani kazidisha kiwanja mpaka road reserve kaimaliza wahusika wapo na wanafanyaga doria lakini naona wanamuogopa mmiliki.

Pale Jogoo kuna mwingine kuelekea kanisa la TAG besides Art Gallery huyu alishapigiwa X lakini habomoi na amaefinya mtaa mzima.
Hata mimi nilishangaa yule jamaa kajenga barabaran kabisa
 
Back
Top Bottom