MC acheni kuposti video za harusi na sendoff bila idhini

Niliendaga harusi ya mwamba mmoja
Humo ndani ilikuwa marufuku mtu kupiga picha au kurecord video
Kulikuwa na mtu maalum wao wa shuguli hiyo

Ova
Kwamba simu zinakusanywa ama wanafanyaje kuzuia watu wasirekodi

Yani nikuchangie Laki halafu unikataze nisirekodi utarudisha mchango wangu
 
Bahati mbaya sana walengwa hasa ma bibi harusi wanapenda sana,Kuna harusi nilihudhuria nikashangaa baada ya siku kadhaa bidada kanitumia picha zao ili nipost status, sikupost maana huwa sipost chochote
 
Yaani, kuna kabinti katulivu tu, ila kwenye harusi moja kakajiachia kaka nyonga nyonga zake basi baada ya hapo kila mtu anakatongoza, wahuni walijua kana gawa gawa tu. kenyewe kalifurahi tu kwenye harusi ya mjomba wake.
 
Bahati mbaya sana walengwa hasa ma bibi harusi wanapenda sana,Kuna harusi nilihudhuria nikashangaa baada ya siku kadhaa bidada kanitumia picha zao ili nipost status, sikupost maana huwa sipost chochote
Siujui ukaribu wenu, ila sidhani kama alikutumia upost..

Mm pia rafiki angu alinitumia, alituma akaweka na ka sms β€˜our dress’ Nadhani alinitumia sbb tulikuwa bega kwa bega kwenye ile dress yake.
 
Kumbe suala hapa siyo kuwa videos zinazopostiwa na mc zinadhalilisha, bali ni kwamba wahusika wanataka kuepuka kujulikana maovu yao??
 
Kumbe suala hapa siyo kuwa videos zinazopostiwa na mc zinadhalilisha, bali ni kwamba wahusika wanataka kuepuka kujulikana maovu yao??
Kuna hiyo. Na nyingine zinamuelekeo wa udhalilishaji. Kwenye sherehe watu wanajiachia,, kumbe mtaani ni walokole tu wazuri.
Sasa mkipost sio nzuri
 
Hii inajitokeza zaidi katika siku za karibuni kutokana na maendeleo makubwa ya mtandao.
hili halijaanza siku za karibuni kutokana na maendeleo ya mtandao, labda wewe ndio umeshtukia jana au umepata mtandao jana

tatizo ni biashara za kienyeji enyeji zisizo na mikataba

unampa mtu kazi ya milioni tano (MC, Mziki, n.k.), hamna mkataba, hamna risiti, hamna cheki, hamna nothing..... unategemea afanyeje?

Nini ku post, kuna siku mtakuta wamezi photoshop mko uchi uchi...
dawa yao ni mikataba, mikataba inayoshitakika mahakamani
 
Nisiku za karibuni baada ya smartphone revolution 2011 sijui unabisha nini
 
Kweli mkuu
 
Wengi wanapenda clips kuwekwa mtandaoni na ndiyo inekuwa kawaida. Labda sasa unapomfuata MC inabidi umuonye asiweke picha zako mitandaoni.

Lakini kama wewe ni raia unayeishi kwa maadili mimi sioni ubaya mtu akiweka clip. Ku comment watu wana comment vizuri na wengine vibaya na hiyo ndiyo social media ilivyo. Ila social media haiwezi kubadili vile ulivyo
 
Nikitaka kucheka naangalia hii video οΏ½ kumbe huku ukumbini kuna mambo sanaπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 

Attachments

  • VID_22761015_030632_662.mp4
    18.1 MB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…