Kwasababu ya imani ya kikristo kuwaaminisha yesu ni mungu wakikaa vizuri akili ikitulia wakijiuliza je kabla ya kuzaliwa yesu dunia haikua na Mungu? Ndo hapo hapo wanaanza kuona wanatapeliwa wanasema Mungu hayupo
Hahahaaa! Na wewe umeona umeandika bonge la argument? Okay nita assume hujawahi kujua ambacho Wakristo wanaamini. Kama ndivyo acha nikusaidie.
Wakristo hawaamini ulichokiandika. Ngoja nikuletee mstari mmojawapo unaoelezea hiki kitu.
Isaya 9:6
"Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani"
Huu unabii juu ya Yesu (Mtoto aliyezaliwa)
Mtoto amezaliwa lakini mtoto tumepewa. Unapewa kitu ambacho kipo tayari. Kwa hiyo huyu mtoto mwanaume alikuwepo, tukapewa na akazaliwa. Kukurahisishia na wale wasiojua Ukristo ni kwamba Mungu katika Nafsi ya Mwana, aliutwaa mwili akawa Mwanadamu bila kuacha kuwa Mungu. Ndio maana huyo mtoto ni mshauri wa ajabu na ni Mungu mwenye nguvu...
Kama mstari huu unakupa kizunguzungu acha nikupe mwingine.
Mika 5:2
"Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele"
Bado huu ni unabii wa Masihi Yesu. Note kiwa toka Bethlehemu atatokea mtawala. Atazaliwa kwao mtu ambaye atakuwa mtawala. Lakini matokeo yake (His going forth) ni milele. Hakuna mwanadamu ambaye amekuwepo tangu milele. Huyu ni Mungu akiuvaa mwili na kuongeza ubinadamu katika Uungu wake.
Kwa hiyo Wakristo hawaamini kuwa Mungu alianza Yesu alipozaliwa. Wakristo tunaamini kuwa Mungu katika nafsi ya Mwana, akaongeza asili ya mwanadamu katika asili ya uungu wake kwa hiyo Yesu ni mwanadamu kamili na Mungu kamili.
Wengi hulalamika hii haiwezekani Mungu hawezi kufanya hivi blah blah, as if wao ni wazazi wa Mungu kumpangia anachoweza na asichowrza kufanya. Absurd! Mungu anafanya anachotaka na achoona ni sawa. Na sisi mavumbi ya udongo hatuna mamlaka ya kumpangia.
Kama hukubaliani na theolojia ya Wakristo usi misrepresent. Ni akili mbovu kufanya hivyo