Mtangoo
JF-Expert Member
- Oct 25, 2012
- 6,167
- 5,613
Uko sahihi. Lakini yeye kaleta maandiko gani zaidi ya anavyowaza au kuona (hisia zake).Ila kwa mfano tukisema Mungu hasemi uongo au Mungu hafi ni vitu ambavyo vimeelezwa kwenye biblia, kwa sababu hatuwezi kumjua Mungu kwa kutumia akili au hisia zetu bali lazima tumjue kupitia maandiko. Kwahiyo lazima ufikirie kuwa wanaosema Mungu hawezi kufanya hivi au vile wanasema hivyo kutokana wamesoma huko maandiko.
Akili za binadamu ni ndogo mno kujaribu hata kuelewa Mungu alivyo. Ndio maana tunahitaji Mungu mwenyewe atuambie alivyo. Changamoto iliyopo ni kwa mtu kujua Mungu kasema kupitia maandiko gani, maana yapo maandiko mengi na yanapingana. Hili ni swali muhimu sana na lenye akili. Na linapendeza kulijadili kwa wale wanaopenda kujua Mungu amejifunua kwenye kitabu gani (hata kama sio cha imani yake). Ila ni swali lisilo na maana kwa wale wenye lengo la kubishana juu ya kila mmoja anachoamini.
Summary: Uko sahihi...!