MC Pilipili afungua Kanisa

MC Pilipili afungua Kanisa

Ila kwa mfano tukisema Mungu hasemi uongo au Mungu hafi ni vitu ambavyo vimeelezwa kwenye biblia, kwa sababu hatuwezi kumjua Mungu kwa kutumia akili au hisia zetu bali lazima tumjue kupitia maandiko. Kwahiyo lazima ufikirie kuwa wanaosema Mungu hawezi kufanya hivi au vile wanasema hivyo kutokana wamesoma huko maandiko.
Uko sahihi. Lakini yeye kaleta maandiko gani zaidi ya anavyowaza au kuona (hisia zake).
Akili za binadamu ni ndogo mno kujaribu hata kuelewa Mungu alivyo. Ndio maana tunahitaji Mungu mwenyewe atuambie alivyo. Changamoto iliyopo ni kwa mtu kujua Mungu kasema kupitia maandiko gani, maana yapo maandiko mengi na yanapingana. Hili ni swali muhimu sana na lenye akili. Na linapendeza kulijadili kwa wale wanaopenda kujua Mungu amejifunua kwenye kitabu gani (hata kama sio cha imani yake). Ila ni swali lisilo na maana kwa wale wenye lengo la kubishana juu ya kila mmoja anachoamini.

Summary: Uko sahihi...!
 
Maandiko uliyokuwa unayatumia yalikuwa yanatoka kwenye biblia na mimi nakusudia biblia hiyohiyo.
 
Acha ujinga, wewe sio Mungu wa kuchagua nani achunge kondoo wake. Mungu ameita majambazi, na wauaji akawabadilisha na kuwapa kazi ya kuchunga kondoo wake. Paulo akiwa Sauli alikuwa muuaji na alihusika katika mauaji ya Stefano. Hata njiani alikopigwa dafrau na Yesu alikuwa ameenda kuwakama Wakristo. Lakini Sauli ndio mwandishi wa citabu vingi vya agano jipya.

Kwa hiyo Mungu hapimi mtu kwa maisha ya nyuma bali ya sasa. Kama kuna kitu mtu kafanya na hakimpasi mchungaji useme hicho sio kuangalia kazi ya mtu tena halali kabisa!

Wamepewa uhuru na Mungu acha wautumie. Kila mtu atajibu kivyake.
Ok
 
Nilishangaa sana
Nikahitimisha pengine ndio sababu

Hivi kweli yule MC maarufu na yeye ana miliki kondoo sasa hivi?

Na yeye anaombea watu??

Ndio maana watu wana badili gia angani

🤔😷🙅🏽🙅🏽
Lakini hushangai SAULI muuaji kuwa muhubiri mashuhuri na baba wa kwanza wa Kanisa
 
Mnakaririshwa asee mnatamka maneno ya kiarabu na hata hamjui maana yake
Mkuu kiarabu ni lugha kama lugha zengine ndio maana kuna hadi wazungu wapo waliyojifunza kiarabu, sasa ukisema wanakaririshwa wasichojua unakuwa na maana gani? Pengine wewe unaona ni lugha ya ajabu ajabu ila ndio kama nilivyokwambia kuwa kiarabu ni lugha tu kama zengine na inafundishika tu na kueleweka.
 
Sisi wote tulipewa kibali cha kuzaliwa duniani tumetumwa kufanya kazi kwa sifa na utukufu wa Mungu; yaani sisi sote ni mitume wa Mungu.

Mungu huwa anachagua mtu
"kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo" - Waefeso 4:11-13

Na utaratibu wake wa Mungu katika kuwachagua watu hauratibiwi na mtu ndio maana Musa aliitwa na Mungu mwenyewe na kupewa jukumu lakini Daudi alipakwa mafuta/ailtawadhwa na Samueli baada ya Samuel kupokea maagizo toka kwa Mungu.

Hii ya Pilipili kufungua kanisa ili uweze kumtumikia Mungu anajua yeye na Mungu wake na tumwache. Hii ya kufanya uzinduzi Kebbys nayo tumwachie yeye na Mungu wake
Mungu hawezi kutumia Tapeli kama huyu
 
Una miaka mingap Kwan mn unaongea kitoto Sana ,,wamechalengiwa na nan wakachinja watu ,hebu weka huo ushaid ,na nan sasa awachalenj Kama wakristo wenyew kitabu Chao hawawez kukichalenj na kumejaa madudu wataweza Qur'an ?
Wanachalenjiwa na hao wanaotoka kwenye hiyo dini, na wala sio hao wakristo unaosema. Consequences zake wanaishia kukimbia nchi na kwenda magharibi kutafuta hifadhi.

Ukiwekewa ushahidi utaukubali hapa wakati utaishia kusema ni propaganda kama kawaida yenu.

Tafiti fupi ni ya hapa hapa Jf Atheist karibia wote asili yao wametokea kwenye Ukristo kuna mifano rahisi ;

1.Kuna member kaanzisha uzi Freemason ndani ya makanisa na katika uzi ule ukifuatilia reply unagundua wengi wana mashaka na Imani yao

2.Kuna member alianzisha uzi wa kufuta bible

3.Bujibuji Mzee wetu alianzisha uzi wa kuacha kwenda kanisani na usanii wa wachungaji

4.@KENZY naye mkristo kaanzisha mada juzi juzi inayoashiria kuwa naye anaingia kwenye chama la Kiranga

5.@Darmian naye mkristo naye kaanzisha uzi unaoashiria anaona kama yuko chaka

6.nk
Mimi nilikuwa muislam, lakini sasa hivi ni atheist... na sina haja ya kuweka bandiko.
 
ukimaanisha Waislam ndio maana atheist waliokuwa Waislam hwaonekani?
Wote wote, kuna watu wanahofia siku wakijitambulisha ni atheist watatengwa na jamii zao... wanahofu hawatazikwa au kupewa msaada wowote wa kijamii na jamaa zao.

Lakini matendo ya watu tu, yanakwambia hawaamini wanayosema. Kuna watu humu utawaona wanakosoa sana watu waliokacha dini zao, na kujfanya wema sana, lakini behind the scene ndio wanaodanga, ndio wanaofanya mambo ya kishenzi kabisa.
 
Kile ni kimondo kilichokua kimedondika Toka angani .
Wapagani wakawa wanakiabudu wakijua ni kimbe kilichotoka mbinguni.
Dini kwenye vitabu ziko sahihi ila zimeathiriwa na Mila na tamaduni za watu wa kale ,yaani wahenga wa zilipoasisiswa.
Ukristo umeathiriwa na upagani wa Kirumi.
Uislamu umeathiriwa na upagani wa Babeli pamoja na uchawi wa zama za Babiloni.
Watu wanapaswa wasome vitabu vyote vya dini ili watumie akili kupambanua mema na mabaya na kujua kuwa Mungu yupo mahali pote na hafungamani na Tamaduni za watu ila anahitaji watu wawe watakatifu ili wauone ufalme wake na waishi kwenye ufalme huo milele kuanzia hapa Duniani mpaka we atakapokufa na kufufuka Tena au kuwa na miili ya kiriho isiyokufa Tena.

Mungu ni Roho nao wamwabudio imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli.
Watu hawapaswi wasome, kwasababu ingekuwa ni lazima ingekuja in built .... vitu vya lazima vyote ni in built na vya hiari ni hiari....

Kuna watu tangu kuzaliwa kwao mpaka kufa kwao hawajawahi kujua kusoma au kuandika kutokana generation walizoishi, hii kwangu mimi inaniambia kusoma sio jambo la lazima.

Naomba nijihami, sorry kama nimekukera na maoni yangu.
 
Kufungua kanisa sio dhambi, sasa mnataka afungue nani jamani? Mungu akitaka mtu anachagua yeye anayeona anafaa sio binadamu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi wote tulipewa kibali cha kuzaliwa duniani tumetumwa kufanya kazi kwa sifa na utukufu wa Mungu; yaani sisi sote ni mitume wa Mungu.

Mungu huwa anachagua mtu
"kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo" - Waefeso 4:11-13

Na utaratibu wake wa Mungu katika kuwachagua watu hauratibiwi na mtu ndio maana Musa aliitwa na Mungu mwenyewe na kupewa jukumu lakini Daudi alipakwa mafuta/ailtawadhwa na Samueli baada ya Samuel kupokea maagizo toka kwa Mungu.

Hii ya Pilipili kufungua kanisa ili uweze kumtumikia Mungu anajua yeye na Mungu wake na tumwache. Hii ya kufanya uzinduzi Kebbys nayo tumwachie yeye na Mungu wake
Kebby ni ukumbi, Tena hapo kebby marehemu Mchungaji Mitimingi alikuwa hapo kabla hajahamia kule mbezi beach barabara ya tegeta, sasa nashangaa shida ni nini kama mtu na MUNGU wake wameongea mtu mwingine huwezi jua ni yakwao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom