MC Pilipili amlilia mkewe kwenye kipindi cha Zamaradi | Ni sahihi Mwanaume kumlilia mkeo hadharani?

MC Pilipili amlilia mkewe kwenye kipindi cha Zamaradi | Ni sahihi Mwanaume kumlilia mkeo hadharani?

Mwache afanye mazoezi, naona anautangazia umma alivyo na machozi mengi kwa mdada.

Hapa wala haihitajiki nguvu kutambua KICHWA CHA NYUMBA ni kipi. Bidada anajieleza bila tashwishwi jamaa linalia? Huyu jamaa hawajui wanawake aisee atapata taabu sana. Nakumbuka hata siku ya send off jamaa alimwaga michozi kama yote.
Kwa jinsi ninavyowajua wanawake wanavyopenda ku control, huyu jamaa kuna kipindi kitafika ataiona ndoa chungu.
 
Nasema hiviiiii tena naandika vitu kutoka ndani ya Moyo wangu wala sio unafiki wowote

MC PILIPILI ana haki ya kulia (narudia tena ana haki) acheni nyie haya maisha watu tunapitia mambo mengi sana,watu tumetengwa na wazazi,watu tumetengwa na ndugu,tumetengwa na jamii,tumetengwa na hadi wanyama pori.

inafika wakati mtu unaamua kuingia porini ili uliwe na simba au mnyama yeyote mkali ili tu UFE uliwe upotee katika hii dunia,lakini ajabu unaingia porini unapishana na simba face to face hakugusi,unapishana na Chui face to face hakugusi.

Unalia sana sana unamuuliza Mungu kwanini sasa sifi kama hata hawa wanyama wakali hawanimalizi wananipita kama hawanioni,Mungu kimya,unafuta machozi unarudi uraiani kuendelea na ratiba zako kwa hali ya kutengwa hivyo hivyo.

From nowhere anatokea MWANAMKE anakwambia CONTROLA nakupenda, CONTROLA nimekuchagua wewe pamoja na yote hayo,nipo tayari kuonekana wa ajabu kukusaidia,nipo tayari kuonekana nisiefaa kukusaidia,nipo tayari kufanya lolote na chochote CONTROLA nakupenda from deep inside my heart.

Aseee mimi kama CONTROLA kilio nitakachoangusha hiyo siku hamna wakuweza kuninyamazisha,ntaomba mniache nilie na kweli ntalia,narudia tena ntaliaa😭😭, ntalia sana.Wingi wa machozi yatakayonitoka hiyo siku hakuna mtu yeyote duniani kawahi kulia hivyo.

Acheni MC PILIPILI alie acheni kabisa, nasema acheni jamani maisha haya tunapopita hapaelezeki,maisha haya majaribu tunayopita hayasimuliki,ugumu wake hamna njia nyepesi nitakayoweza wasimulia mkaielewa, halafu anatokea mtu hajulikani hata katokea wapi tena MWANAMKE pamoja na kujua historia yangu halafu anatamka maneno aliyotamka mke wa mc pilipili.

Tena sio tu anayatamka kimoyomoyo ila anayatamka wazi na peupe kwenye media Aseee mc pilipili ni nani asitoe chozi😭😭,ninapoandika huu ujumbe nimevaa uhusika wa mc pilipili kanirudisha nyuma sana (nimedondosha machozi) yes nasema hivi muacheni MC PILIPILI hamna anaemjua kuliko yeye ajijuavyo.

Muacheni Muacheni he is a real Gentleman tena nasema he is one among Few of his Type. Pole pilipili,Pole sana.
 
CONTROLA,

Kwani kusema ndiyo kumaanisha toka moyoni?
Kwani kusema ndiyo kutenda?

Wengi wanaishia kusema mdomoni lakini kwenye matendo ni tofauti kabisa!

Mtu anakufokea mbele ya watu hajui kujustahi na imeandikwa kabisa “mke asiache kumstahi mume wake”

Hapo utasema aliposema nakupenda alimasnisha toka moyoni?

Mwingine anakosa uaminifu anakuwa na michepuko huyo utasema anakupenda?

Safari ndo kwanza imeanza !
 
Mnao ona cha ajabu sana napenda tu kuwapa taarifa kuwa "mnamtukana mamba kabla hamjavuka mto" (hasa wanaume)

nimesema hasa wanaume kwa sababu ipo siku 1 leo hii unajiona mzima unatype una record voice note,una move from hapa to pale,Yes ni haki yako sana "kumuona mc pilipili wa ajabu,haki yako".

ila itafika siku 1 haya maisha its like a circle yana rotate taratiibuu itafika time yatakukuta yaliyomkuta mc pilipili,yatakukuta yalio wakuta watu walio paralyse,utakua umelala kitandani unatoa haja zote hapo hapo,miguu ina vidonda vinaoza,maisha yako ni ya shda, mama baba wamekukimbia, ndugu majirani wamekukimbia,Umebaki peke yako kitandani unaugua.


Atatokea mwanamke kama huyo mwanamke wa mc pili pili atakwambia Njopino nakupenda, Saoka nakupenda Kizzy Wizzy nakupenda kwa hali yako hiyo hiyo,nitakupenda na ntahakikisha unainuka tena kitandani,mwanamke huyo atapambana kufa na kupona hadi utasimama tena juu,utaanza kutembea.

Then baada ya kupona Mungu si athumani utaitwa mahali utaambiwa bwana flani sema kitu kuhusu mke wako,nakuhakikishia wewe unae mcheka mcpilipili leo ukiambiwa sema kitu kuhusu mke wako,kabla hujasema "A" machozi yataanza kushuka yenyewe😭,na yatashuka kuliko yaliyomshuka MC PILIPILI.

Nawambia hivi ndugu zanguni wote mnao muona mc pilipili wa ajabu hapaswi kulia Mnakosea,Mnakosea na nipende tu kuwambia kuwa THIS IS LIFE (tupo sana tuombe uzima).
 
CONTROLA,


Sasa huko kwenye media si ndiko watu wanako pretend kwa sana na show off?!

Yani ulitegemea iwe kinyume chake?!

Siyo kila yanayofanyuka kwenye media wanamaanisha , fahamu hivyo.

Wengine kwenye macho ya watu wanajidai kupendana lakini wakiingia ndani ya nyumba kulala kila mtu na chumba chake [emoji108][emoji108][emoji108]

Kuwa uyaone mdogo wangu!

Wala usijilinganishe na mtu mwingine au ku admire life style ya mtu au watu fulani siku ukija kuujua ukweli wa maisha yao utachoka mwenyewe!

Tafuta kumjua Mungu , soma au fanya kazi kwa bidii, heshimu watu wote, jifunze kuwa na tabia njema itakayo kuwezesha kuishi popote na mtu au watu wowote .

Kuwa tayari kukiri makosa unapokosolewa na kuwa tayari kujifunza kubadilika ndipo utakapopata kibali machoni pa Mungu na wanadamu.
 
Kajamaa kanaulizwa swali badala kajiweke kama kidume ajibu kanajiinamia kanajishika nacho kanalia halafu mwanamke anainuka kukabembeleza. Huyu jamaa akijivua huo upilipili akamvisha mwingine then ashuhudie hivyo vituko angejikana!
 
nakuuliza swali 1, ondoa maigizo ondoa comedy za mc pilipili

Kama kulia kule kwa mke wake kumetoka moyoni na ni halisi,

Je,kwako unaona pilipili yupo sahihi au hayupo sahihi? nijibu kabla sijaendelea.

Akilinjema


Kwa mujibu wa maelezo yako ni kuwa huenda Mc pilipili alikosaga upendo hapo awali , na kwamba sasa amepata mwanamke anaenpenda ambae anathubutu kumtamkia kumpenda hadi mbele ya media.

Wewe ukasema hata ungekuwa ni wewe ungelia sana zaidi yake!

Sasa mimi nikasema mwanamke kumwambia nakupenda , nitakulinda, nitakushimu, nitakutunza n.k peke yake haitoshi kuthibitisha kwamba hayo yanayoka moyoni mwake.

Uzoefu unaonesha ni fix tu zile!

Sasa nikijibu swali lako;

Yule jamaa kulia kwake kunaweza sababishwa na sababu nyingi wala siyo kwamba eti sababu ya upendo tu [emoji108][emoji108]

Mimi nilitaka kumnanga lakini nilipotafakali nikaacha kumnanga na kuanza kumhurumia kwa kuzani pengine anamatatizo ambayo akiwaza yanamchanganya tu.

Hujawahi ona wanandoa ambao wakiwa hadharani wana pretend kupendana sana lakini kumbe mmoja ni Mtumwa kwa mwenzie kiasi cha kukosa raha ya nafsi?

Yule huenda analia kwa kupima mbele kwamba ikitokea kuachwa kwa sababu moja ama nyingine jamii inamuelewaje na mashauzi yake?

Au analia jinsi anavyopelekeshwa mwendo kasi kwa mahitaji na kuchoka wakati hadharani anamwambia anampenda?!

Sometimes better to expect less or nothing ili kuepuka disappointments in life!
 
Akilinjema,

maelezo ni mengi nahitaji simpo and clear answer "achana na maelezo yangu" fanya kama hamna nilipoelezea chochote kisha jibu hili swali in a single sentence. 👇👇

CONTROLA, post: 33649145,

Akilinjema sitaki maelezo marefu wala insha nahitaji jibu 1 tu,sitaki sjui "kama" sjui "hivi" sjui "vile" hapa tunaongelea kilio cha mc pilipili kwa mke wake Je kwako jibu ni "Yes,he is right" au "No,he is wrong"
 
CONTROLA,


Mimi sinaga majibu mepesi sababu nimejifunza kuangalia nje ya box always!
Sasa kama unataka jibu la ndiyo hapana kwangu siyo rahisi saababu naangalia na nje ya box siishii kuangalia ndani peke yake!

Labda nianze kuweka assumptions kwa kuzingatia other factors kitu ambacho nitaandika zaidi na wewe unaona ni insha!
 
Back
Top Bottom