MC Pilipili amlilia mkewe kwenye kipindi cha Zamaradi | Ni sahihi Mwanaume kumlilia mkeo hadharani?

MC Pilipili amlilia mkewe kwenye kipindi cha Zamaradi | Ni sahihi Mwanaume kumlilia mkeo hadharani?

CONTROLA,
Wanawake wa namna hiyo wameshakufaga kwenye WW1, zimebaki copy kwenye movie tu hasa za bongo. Kulia mbele za watu hasa mwanaume unaonyesha, you are weak enough kushindwa ku control hisia zako otherwise tuseme yalikuwa maigizo, chochote kinawezekana mbele ya camera.
 
Mc Pilipili kila siku zinavyokwenda unazidi kutuaibisha wagogo
Inakuwaje mwanaume unalia mbele ya mkeo tena mbele ya media
Ilitokea ulizuzuka wakat unamtambulisha
Hata baada ya kumuoa bado unadeka tu
Kaaaa,sisi wagogo tunaomba tuwauzie wachaga na wahaya huyu mtu maana kajaa sifa
 
These are the type of niggas when they nut the whole neighbourhood gon know as niggas be shouting, cursing and shit.

It's all perfect tho
 
Mpaka mwanangu nae kalia kikuda kweli
istockphoto-151557041-612x612.jpg
 
Tangu hiki kipindi kimeanza nimeona zamaradi akiita zaidi wanawake na si mke na mume, isije kuwa pilipili alitaka kuongozana na mkewe kutokana na mahaba ya kihindi .

Katika machozi hayahaya kuna mmoja hapo anateseka sana na staili ya maisha ya mwenzie ndo maana inawagharimu mno kudhirisha upendo binafsi naona elements za Toxic relationship no matter how much they cry.

Kwenye macho yao mmoja anadai kuheshimiwa na mwengine anataka kutambulika kwa uzuri alionao anyway still is life kila Baharia anapambana na alichonacho.

Pia relation ship hii ni kama ina maigizo mengi kuliko uhalisia mambo ya mbelembele....

Mwamba punguza kulia only men in Philippines cry often in audience hii kitu ipo kwenye filamu za ufilpino na chache mataifa mengine.

Ila nampa angalizo mke wa pilipili machozi ya mwanaume mara nyingi ni yakuchunguza mda mwingine hayana tofauti na machozi ya mamba (crocodile tears) kwanza jamaa kaanza kudondosha machozi ghafla baada ya Zama kurecommend maongezi ya wife wake.
 
Hivi mbona JF ni kama hamuoni kinachoendelea kwa MC mwenye chombo yakee.

Hivi ni sahihi Mwanaume kumililia Mwanamke hadharani kama alivyofanya jamaa?

Daah! Kulia hadharani nimeshindwà kukubaliana nayo. Kama kulia, nitajiliza faragha, chumbani hukoo tena baada ya kujiliza inafata show ya haja.

View attachment 1278759
Huyu ni fala numba moja Tanzania, kwanza hakuwahi kuwa mwanachama wa chama cha Mabaharia
 
Nasema hiviiiii tena naandika vitu kutoka ndani ya Moyo wangu wala sio unafiki wowote

MC PILIPILI ana haki ya kulia (narudia tena ana haki) acheni nyie haya maisha watu tunapitia mambo mengi sana,watu tumetengwa na wazazi,watu tumetengwa na ndugu,tumetengwa na jamii,tumetengwa na hadi wanyama pori.

inafika wakati mtu unaamua kuingia porini ili uliwe na simba au mnyama yeyote mkali ili tu UFE uliwe upotee katika hii dunia,lakini ajabu unaingia porini unapishana na simba face to face hakugusi,unapishana na Chui face to face hakugusi.

Unalia sana sana unamuuliza Mungu kwanini sasa sifi kama hata hawa wanyama wakali hawanimalizi wananipita kama hawanioni,Mungu kimya,unafuta machozi unarudi uraiani kuendelea na ratiba zako kwa hali ya kutengwa hivyo hivyo.

From nowhere anatokea MWANAMKE anakwambia CONTROLA nakupenda, CONTROLA nimekuchagua wewe pamoja na yote hayo,nipo tayari kuonekana wa ajabu kukusaidia,nipo tayari kuonekana nisiefaa kukusaidia,nipo tayari kufanya lolote na chochote CONTROLA nakupenda from deep inside my heart.

Aseee mimi kama CONTROLA kilio nitakachoangusha hiyo siku hamna wakuweza kuninyamazisha,ntaomba mniache nilie na kweli ntalia,narudia tena ntaliaa😭😭, ntalia sana.Wingi wa machozi yatakayonitoka hiyo siku hakuna mtu yeyote duniani kawahi kulia hivyo.

Acheni MC PILIPILI alie acheni kabisa, nasema acheni jamani maisha haya tunapopita hapaelezeki,maisha haya majaribu tunayopita hayasimuliki,ugumu wake hamna njia nyepesi nitakayoweza wasimulia mkaielewa, halafu anatokea mtu hajulikani hata katokea wapi tena MWANAMKE pamoja na kujua historia yangu halafu anatamka maneno aliyotamka mke wa mc pilipili.

Tena sio tu anayatamka kimoyomoyo ila anayatamka wazi na peupe kwenye media Aseee mc pilipili ni nani asitoe chozi😭😭,ninapoandika huu ujumbe nimevaa uhusika wa mc pilipili kanirudisha nyuma sana (nimedondosha machozi) yes nasema hivi muacheni MC PILIPILI hamna anaemjua kuliko yeye ajijuavyo.

Muacheni Muacheni he is a real Gentleman tena nasema he is one among Few of his Type. Pole pilipili,Pole sana.

Mkuu mimi naomba nibishane na wewe kabisaa.
Kwanza kabisa, hayo matatizo unayoyataja, asilimia kubwa ya watu tunaoishi kwenye hizi nchi masikini tunayapitia. Na hata kama ni kweli jamaa kayapitia lakini sisi kama wanaume tumekuzwa kuji control na kupambana kiume! Mwanaume umeumbwa kubeba mambo mazito, kuteseka, kunyanyasika, kupigana na hata kufa lakini kamwe hutakiwi kuonyesha udhaifu mbele za watu, hasahasa mkeo. Ndio maana hata kwenye misiba huwezi kukuta mwanaume analia na kugalagala chini hata kama umeumia kiasi gani!!

Mwanaume unapooa, yule mwanamke anakutegemea wewe kwamba ndio utakua nguzo yake na ulinzi wake. Kama hujui hili nenda kasome au uliza ni kwanini kwenye ndoa mwanamke anakaa upande wa kushoto? Hivi wewe ukiwa na mlinzi au bodyguard halafu uone anaanza kulia hata kabla maadui hawajatokezea utaona kuna mlinzi hapo?

Wanawake by nature ni "control freaks" mwanamke akishajua una weakness kwake aisee atakuendesha kama gari bovu tena ukicheza atakulamba vibao mbele za watu. Huyu dogo ajiangalie sana.
 
Back
Top Bottom