R.I.P Mtikila!
Tuliobaki tuna la kujifunza, hasa tulio na dhamana ya kuelimisha juu ya Imani, uadilifu, unyenyekevu, heshima na Ibada bora kwa Mwenyezi Mungu.
Tumwombe Mungu atujarie angalau hekima kidogo tu kama punje ya haradali tutambue mipaka yetu linapokuja swala la utu wa mtu na hadhi ya Mwenyezi Mungu.
Tunakashifu au kumdhiaki mtu; tutambue Ugonjwa na Afya ni kudra ya Mwenyezi Mungu pekee hali kadhalika Umauti na Uzima ni vyake yeye...... UTUKUFU HUU HATUHUSTAHILI HATA CHEMBE.
Tumheshimu Mungu na Tujiheshimu na kuwaheshimu waja wake wengine tujiepushe na KIBURI CHA UZIMA.
Nitamkumbuka sana Mtikila kama mpambanaji hasa kwa mambo mawili:-
1. Mgombea Binafsi
2. Kudai Tanganyika
Zaidi, tukumbuke hadithi ya Miriamu na Musa (Hesabu 12:1-11).
R.I.P Mtikila.
Ni shujaa uliyeondoka kwa staili ya Goliathi.
Tuliobaki, TUJIFUNZE