TANZIA Mch. Christopher Mtikila afariki baada ya kupata ajali, Msolwa - Chalinze mkoani Pwani

TANZIA Mch. Christopher Mtikila afariki baada ya kupata ajali, Msolwa - Chalinze mkoani Pwani

Jamani si alimsema sana Lowasa juzi juzi hapa kwamba ni mgonjwa sana. Jamani haujafa haujaumbika..
 
Dhambi zote zitasamehewa hata ukiua utasamehewa ila Dhabi ya kumkufuru roho Mtakatifu haitasamehewa kamwe!
 
acheni kuingiza propaganda mpaka kwenye vifo n yie eboo,RIP REV.MTIKILA,tutakukumbuka kwa kauli yako ya saa ya ukombozi ni sasa.

Hawa ndio ukawa damu.
 
Pumzika kwa Amani Mtikila ...

Umeondoka bila kuiona Tanganyika yako.
 
Wakuu,

Kuna taarifa kwamba Mchungaji Christopher Mtikila amepata ajali ya gari mkoani Pwani alfajiri ya leo, taarifa zaidi tunasubiria kutoka kwa Kamanda wa Polisi mkoani humo.

=====
UPDATE:

JamiiForums imeongea na Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema amefariki saa 12 kasorobo asubuhi katika kijiji cha Msolwa, Chalinze.

Amesema gari lililokuwa limempakia lilikuwa linatokea Morogoro na kwamba walikuwa watu wanne ambapo wengine watatu wamejeruhiwa vibaya.

Majeruhi wamekimbizwa katika Hospitali ya Tumbi.

MGONJWA WETU NA Rais WETU Mtarajiwa Ndugu Edward Ngoyai Lowasa BADO ANADUNDA TU, YU HAI, NI MZIMA.
 
Basi naanza kumwogopa Mungu wa Lowassa, anaelipa visasi badala ya kusamehe.
Hakulipa kisasi bali ameitwa kwa mahojiano: Swali la kwanza atakaloulizwa ni "wewe si mchungaji? kwa nini ukafanya kazi ya kulaani badala ya kuombea roho za watu zibadilike kunifuata mimi? La pili, je unajua Mimi ni I AM? Ninatoa na ninachukua na pia ninaponya? Aliyekupa mamlaka ya kuwanyanyasa watu wangu ni nani? Jamaa ana hali ngumu kweli kweli!
 
Lowassa kila a anakwambia wewe ni mgonjwa unamfanyia hivi utaondoa wangapi. Rip Mtikila rip Mtoi rip kombani
 
Kwa hiyo kumbe Lowasa siyo mgonjwa? Kwa hiyo wewe unataka tumpeleke ikulu ili akapate nafuu ya kujitibia kwa fedha zetu na mfululizo wa ruhusa za mapumziko ya ugonjwa? Hivi unajua kuwa ikulu kulala ni bahati na kazi ni nyingi kuliko muda? Kama Mtikila atakuwa amekufa ujue hajafa na hoja hii. Swali liko pale pale. Ikulu siyo chaka la wagonjwa. Bora aende mtu mzima ugonjwa uanzie akiwa tayari ikulu na siyo aende nao eti tunamsindikiza sisi watanzania.

Pole ndugu yangu, ujinga huondolewa kwa Elimu, ila Upumbavu ni mzigo utakaoondolewa na Kifo tu! Kwa ugonjwa wa Lowassa bado anatibiwa kwa hiyo hela ya Serikali ambayo unadhani utaiokoa kwa Lowassa kutokuwa Ikulu. Pili, kila mtu ni Mgonjwa na Marehemu mtarajiwa, kumwita Mwenzako Marehemu au kusema anatarajia kufa, ilihali nawe upo kwenye foleni hiyohiyo ni dhihaka kwa Mungu ambaye anajua nani ni nani katika listi, na anaweza ifanyia orodha yake marekebisho!
Kwa upofu wako, umesahau tuna mgonjwa Ikulu,hujasikia tukimtabiria kifo, push ups hazimaanishi Uzima hata kidogo! Siasa zisiondoe UTU, mwombe Mungu akurehemu!
 
Watu wa lowasa wanatutoa njea ya hoja. Hoja ni kwamba afya ya lowasa hatoweza kumudu majukumu urais ipasavyo haijalishi kuna wazima wanakufa kabla ya lowasa. Ebo!

na huo ndo ukweli, anaweza kuishi mda mrefu but kwa mikikimikiki ya urais kwa ile afya ni BIG NOOO!
 
Back
Top Bottom