Ilongailunga
JF-Expert Member
- Jan 18, 2012
- 1,388
- 896
R.I.P Mch mtikila.
Barabara za mkoa wa pwani ni chanzo cha ajali nyingi. Barabara inateleza kama imepakwa mlenda.
Waziri husika awajibishwe haraka
Hii ndio propaganda ya mwisho ya kumchafua Lowassa? Nayo itabuma, mark my words!Nadhani sasa mmejione umafya wa LOWASSA
Chinembe ni Mungu yupi huyo????? Mungu ni wa rehema na hataki hata mmoja apotee.
Kama huyo Mungu wa Lowasa anaua kila atakayemsema basi atauwa watu wengi sana. Lile kusudi la kazi ya msalaba litakuwa limefitinika.
Bwana wetu Yesu Kristo alifanyiwa kila namna ya uovu akasema Baba wasamehe hawajui wafanyalo. Huyo Mungu wa kulipiza papo kwa papo !!!!!!! Mh!!!!! Wapi kazi ya MSALABA???
Damu zilizomwagika hata sasa kama ni mapenzi ya Mungu zitaenda kwa AMANI. Kama ni umafya na ushirikina basi tegemeeni KISASI cha Bwana.
Queen Esther
Tunajua nguvu ya mafisadi inavyofanya kazi ...lakini itashindwa tu
Kabla ya kuchangia uwe unatumia ubongo kufikiria kwanza na sio kutumia "Masaburi" kwenye kufikiria.
Hahaha, sasa wafanyaje na maisha ni magumu!! Hata kama alikuwa na vichenji chenji vimebaki mfukoni wanachukua kwenda kununulia mboga!!hizo nyanya wananchi walivyo wakatili itakuwa walizibeba kwenda kuungia mboga
Lete ushahidi Kwamba Lowassa Amemuua Mch: Mtikila? Endeleeni Kumsema Lowassa Hata wewe Mungu Atakushugulikia, Mungu Yupo upande wa Lowassa. Ndiyo Mjue Afanyaye Mtu Kuwa Mzima Au Mgonjwa Au Kuua Ni Mungu Chungeni Midomo yenu. Wambie na wenzako. Mtafinywa sana.
Tatizo mkuu, uko mbali kwenye siasa za Tanzania ndio maana unashangaa kuwa hapa Mungu anaingiaje. Ni miongoni mwa wanasiasa waliomdhihaki sana Mungu juu ya afya EL hivi karibuni. Kama ni kweli Mungu awatie nguvu wafiwa. Na sisi twaendelea kujifunza kwamba kuumwa sio kufa. Anaweza kuondoka mzima mgonjwa anabaki, haya yote yanatokea ktk jamii zetu.
Rest in peace mchungaji .acheni dhihaka kila mtu ataondoka wakati ukifika.
Ni kweli kabisa ukiwa unaendesha gari bara bara Hiyo ni vema kuwa makini inateleza na INA mawimbi sana. Sote njia yetu ni moja R.I.P mchungaji Mtikila.
Kila mtu ana uhuru wa kuongea anachotaka kuongea. Semeni Lowasa mgonjwa semeni chochote mtakacho. Lakini mimi na nyumba yangu na jirani zangu wote tunampa kura zetu Lowasa pamoja na ugonjwa wake akafie ikulu.