TANZIA Mch. Christopher Mtikila afariki baada ya kupata ajali, Msolwa - Chalinze mkoani Pwani

TANZIA Mch. Christopher Mtikila afariki baada ya kupata ajali, Msolwa - Chalinze mkoani Pwani

Nacho jua pamoja na hayo yote ikulu haitaingiliwa na MTU machafu badala yake uchafu huo ni kwa vizazi vyake di vizazi,
We pumbv mtu kama wewe unatakiwa ukatupwe katikati baharini uliwe na papa...huna umuhimu wa kuishi duniani
 
Kuna watu ni wanafiki sana taarifa ya polisi Leo imekuwa ni kitu muhim kuliko kitu chochote kile, hivi hawa si ndo mnawaita policcm???Pumbavu kbsa af kesho mje mtuletee ishu zenu za kixh*oger dhidi ya polisi na vyombo vyote vya dola.
We mngese, polisi wametoa report baada ya kufanya uchunguzi wa ajali ta mtikila.
kama ww unapingana na hyo report toa yako wewe ambayo uneshirikiana na bibi yako yule gagula wa msolwa ....jing@ wee
 
Hivi wale mnaowaita policcm leo kazi yao imekuwa yakutukuka kwa msiba wa mch. mtikila eee???mlangy, Ww ni Mnduku.
 
Msolwa lile eneo pana tuta pale na kibao cha kilometer 50 . Ripoti ya traffic naiamini kwa kua inaendana na mazingira halisi ya eneo husika na gari husika na pia uzoefu wa dereva aliyepata ajali. ,kua na uzoefu wa kusafiri umbali mrefu bila kupumzika ndani ya siku 3 tu kilometer zaidi ya 1300 toka Dar kwenda Njombe na kurudi had chalinze ilikua ni hatari sana, na usiku hakuna tochi na barabara eneo lile ina mawimbi mengi sana
 
Maajabu kuu ya dunia leo Chadema, CUF na NCCR wanakimbilia kukubali ripoti ya polisi na kusema ni sahihi 100%
Sasa kuanzia leo wamekosa moral authority ya kusema chochote
Swali ndogo tu: mbona mwili wa marehemu hauna hata mkwaruzo katika picha? Maana tumeipitia wengi na jamaa hajapasuka na kioo wala nini!
Hii ripoti haijajibu maswali mengi!
 
Mnamo tarehe 04/10/2015 majira ya saa 05:45hrs huko Msolwa Kata ya Bwilingu barabara kuu ya Dar es Salaam –Morogoro, Wilaya ya Ki-Polisi Chalinze, Mkoa wa Pwani.
Gari No. T.189 AGM aina ya Toyota Corolla likiendeshwa na George Steven Ponera miaka 31, mkazi wa Mbezi Mwisho Dar es Salaam liliacha barabara kisha kupinduka na kusababisha kifo cha Christopher Mtikila miaka 62,mpangwa, mchungaji wa Kanisa la Assemblies, na mwenyekiti wa Chama cha siasa DP mkazi wa Kinondoni "B" Dar Salaam.


Katika ajali hiyo, watu watatu waliokuwamo ndani ya gari hilo na marehemu Mchungaji Mtikila walijeruhiwa ambao ni Ally Mohamed miaka 42 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam, yeye alipata maumivu shingo, mabegani na kifuani, mwengine ni Patrick Mgaya miaka 37 ambaye ni mchungaji
wa Kanisa la Assemblies of God mkazi wa Mbagala Dar es Salaam ambaye alikuwa na michubuko midogo usoni na kuumia kichwani, pamoja na George Steven miaka 31 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam ambaye alipata michubuko kidogo eneo la mabegani. Majeruhi wote walipatiwa matibabu katika Kituo cha afya Chalinze na badae wawili kati yao katika Hospitali teule ya Tumbi na waliruhusiwa kutokana na hali zao kuendelea vizuri.

Baada ya kutokea kwa hiyo ajali, timu maalum ilifika katika eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji wa ajali hiyo ikiongozwa na Mkuu wa utawala wa Traffic kuu Dar es Salaam SACP J. Kahatano, pamoja na mimi mwenyewe,Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoa wa Pwani na kuwashirikisha wataalamu wa Forensic Makao Makuu ya Polisi ACP Kashindye na Dokta A. Makata.
Uchunguzi wa mwili wa marehemu tayari umefanyika, na taarifa ya Daktari aliyefanya uchunguzi huo katika Hospitali ya Rufaa tumbi Kibaha jana tarehe 04/10/2015 umeonyesha kuwa, kifo cha marehemu kimesababishwa na kuvunjika kwa mbavu nane (8) upande wa kushoto na kuingia kwa damu kwenye mfumo wa hewa na kusababisha kushindwa kupumua.

Kabla ya ajali hiyo kutokea marehemu na wenzake tarehe 02/10/2015 jioni waliondoka Dar es Salaam kwenda Mkoa wa Njombe na kufika tarehe 03/10/2015 alfajiri kwa ajili ya kampeni za Chama chao cha DP. Wakiwa huko walipata ajali kwa kugonga magari mawili yaliyopata ajali na
kusababisha uharibifu wa gari lao.Kulingana na taarifa ya Mkaguzi wa magari ya tarehe 03/10/2015 huko Njombe walishauriwa walitengeneze kwanza kabla ya kulitumia tena.Tarehe 03/10/2015 saa
21:30hrs waliondoka Njombe kwenda Dar es Salaam na ilipofika saa 05:45hrs katika eneo la Msolwa ndipo wakapata ajali hii.Uchunguzi uliofanywa kwa kukagua tukio na kuwahoji majeruhi walionusurika (katika eneo hilo hakuna watu wengine walioshuhudia tukio hilo kwa kuwa si eneo la makazi ya watu, ni mbuga). Ajali hii imeonyesha kuwa imesababishwa na sababu
Zifuatazo:
1. Mwendo kasi , dereva mwenyewe anakubali kwamba alikuwa mwendo kasi licha ya kuwepo kwa alama zinazooonyesha kwenda mwendo wa Km 50 kwa saa.
Aidha baada ya kuacha barabara kuu, gari hilo lilikwenda umbali wa mita 125 kabla ya kupinduka hali inayoashiria kuwa lilikuwa kwenye mwendo kasi.
2. Uchovu wa dereva kutokana na safari ndefu kwa kuendesha gari mchana na usiku kucha kabla ya
kuanza safari walikuwa wakishughulikia matengenezo ya gari hilo ambapo hakupata muda wa kupumzika.
3. Kutofunga mkanda ya usalama . Katika uchunguzi inaonyesha marehemu hakufunga mkanda kwa kuwa alirushwa nje kupitia kioo cha mbele (wind screen).
4. Ubovu wa gari. Gari hilo lilipata ajali tarehe 03/10/2015 na moja ya sehemu muhimu iliyoharibika ni mfumo wa usukana (steering system) yawezekana halikupata matengenezo kikamilifu na hivyo kuchangia kutokea kwa ajali hiyo.
Hivyo nitumie fursa hii kuwaomba wananchi kuwafichua maderva wanaokwenda mwendo kasi kupitia namba 08007575 ama 0715 009953 au 0658 376012. Aidha niwatake madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kwa wale watakao kaidi Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani hatutasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengi.

Asanteni kwa kunisikiliza.
Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa PwaniKamishina
Msaidizi Jafari Ibrahim.
 
Kibaha/Dar. Polisi mkoani Pwani, imeweka bayana sababu za kitaalamu za kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila ikisema alivunjika mbavu nane upande wa kushoto, damu kuingia kwenye mfumo wa hewa na kushindwa kupumua.
Mchungaji Mtikila alifariki dunia juzi alfajiri baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Njombe kwenda Dar es Salaam, likiwa katika mwendo mkali, kuacha njia na kupinduka. Alirushwa nje kupitia kioo cha mbele kutokana na kutofunga mkanda.
Katika ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Msolwa, Chalinze mkoani Pwani, watu wengine wawili waliokuwa kwenye gari hilo dogo walijeruhiwa na dereva anashikiliwa na polisi akitarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafari Mohamed alisema jana kuwa baada ya uchunguzi wa mwili wa marehemu, madaktari katika hospitali Teule ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi walibaini kuwa sababu hizo ndizo zilizosababisha kifo chake.
Ilikuwa ajali ya pili
Pia imegundulika kuwa, kabla ya ajali hiyo kutokea, Mtikila na abiria wenzake ambao waliondoka Dar es Salaam Oktoba 2 jioni kwenda Njombe na kufika Oktoba 3 alfajiri kwa ajili ya kampeni za chama chake, wakiwa huko walipata ajali kwa kugonga magari mawili yaliyokuwa pia yamepata ajali na kusababisha uharibifu wa gari lao hilo.
“Kulingana na taarifa ya mkaguzi wa magari ya Oktoba 3, huko Njombe, walishauriwa watengeneze gari lao kwanza kabla ya kulitumia tena. Saa 3.30 usiku waliondoka Njombe kurudi Dar es Salaam na ilipofika saa 11.45 alfajiri Oktoba 4 ndipo wakapata ajali,” alisema Kamanda Mohamed.
Sababu za ajali
Alisema uchunguzi uliofanywa kwa kukagua tukio zima la ajali na kuwahoji majeruhi, umeonyesha kuwa ajali hizo zimesababishwa na mambo manne.
Kamanda Mohamed aliyataja mambo hayo kuwa ni ubovu wa gari kwa kuwa lilipopata ajali Oktoba 3, moja ya sehemu muhimu ziliyoharibika ni mfumo wa usukani, hivyo inawezekana halikupata matengenezo kikamilifu na hivyo kuchangia ajali hiyo ya pili.
Jingine ni Mtikila kutofunga mkanda wa usalama na hivyo kusababisha arushwe nje kupitia kioo cha mbele, uchovu wa dereva kutokana na safari ndefu ya kuendesha gari mchana na usiku na kabla ya safari kurudi alikuwa akishughulikia matengenezo ya gari hivyo hakupata muda wa kupumzika.
Alisema pia kuwa mwendo kasi pia ni chanzo kingine cha ajali na kwamba dereva wa gari hilo, George Steven amekiri kuwa walikuwa mwendo kasi licha ya kuwapo alama zinazoelekeza mwendo na hivyo baada ya gari kuacha barabara lilikwenda umbali wa mita 105 kabla ya kupinduka.
Wataalamu wakusanyika
Kamanda Mohamed alisema: “Baada ya ajali, timu maalumu ilifika eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji ikiongozwa na Mkuu wa Utawala wa Trafiki Makao Makuu Dar es Salaam, Johansen Kahatano, mimi, mkuu wa upelelezi makosa ya jinai mkoani hapa na daktari wa maabara ya kisayansi inayohusu uchunguzi wa makosa ya jinai.
“Walishirikiana na wataalamu wa sayansi ya makosa ya jinai kutoka Makao Makuu ya Polisi wakafanya ukaguzi na uchunguzi wao ukabaini mambo hayo yalichangia ajali hiyo,” alisema Kamada Mohamed.
Mwili wa Mtikila tayari umekabidhiwa ndugu zake kwa taratibu za mazishi wakati dereva Steven akisubiri kufikishwa mahakamani wakati wowote.
Baraza laahirisha
Kutokana na msiba huo, Baraza la Vyama vya Siasa limeahirisha vikao vyake ili kumuenzi Mtikila mpaka baada ya maziko yake. Mwenyekiti wa Baraza hilo, Peter Mziray alisema kifo hicho ni pigo kwa maendeleo ya demokrasia nchini.
Kikwete atuma salamu
Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete ametuma salamu za rambirambi kutokana na kifo cha Mchungaji Mtikila. Katika salamu hizo Rais alisema: “Kifo hicho ni pigo kwa medani za siasa katika Tanzania na kimetunyang’anya mmoja wa viongozi hodari na wazalendo, aliyekuwa na msimamo thabiti na usioyumba katika kutetea mambo ambayo aliyaamini katika maisha yake yote.
“Ni jambo la kusikitisha pia kuwa tunampoteza Mchungaji Mtikila katika kipindi cha mchakato muhimu wa kisiasa nchini ambako mchango wake ulikuwa unahitajika sana. Hakika, tutamkosa mwenzetu katika uwanja wa siasa za nchi yetu.”
Imeandikwa na Julieth Ngarabali (Pwani), Ephrahim Bahemu, Julius Mathias na Kelvin Matandiko (Dar)
 
Yeah Mkuu...

Ban ya Maisha...!!!

Date lifted: NEVER... JF wana hasira..

Anyway.. natumia maneno ya upole, coz am FULL, once nikishusha NONDO hapa JF watanifungia tena...!!!

What remains is to pray, Lowassa awe Rais wetu...!!!

JF wanajua nikifunguka, wanaungua sana...!!!
Sikuona tofauti au Kosa la ule uzi maana upande wapili wanakuja na nyuzi zenye matusi ule haukuwa na tusi ila poa Mabadiliko yako pale pale hayaepukiki
 
akihojiwa kiongozi ambae nae alijeruhiwa amedai kabla ya Ajali kuna land cruiser ilipita mbele yao kwa spidi na ndio chanzo cha wao kupt Ajali
chanzo. ch10

my take: polisi msipuuzie kwan kwenye mitandao kuna kauli isemao huna haja kujiua taja ugonjwa wa mh it will happen.
 
akihojiwa kiongozi ambae nae alijeruhiwa amedai kabla ya Ajali kuna land cruiser ilipita mbele yao kwa spidi na ndio chanzo cha wao kupt Ajali
chanzo. ch10

my take: polisi msipuuzie kwan kwenye mitandao kuna kauli isemao huna haja kujiua taja ugonjwa wa mh it will happen.

Pole sana kijana.Vipi taarifa ya polisi umeiona?
 
DP inazikwa na Mtikila.
Hakuwa na katibu, katibu mwenezi wala mhazini..sembuse muhuri wa chama

Huyo kiongozi mtakuwa lumumba mmemuweka baada ya kudaka briefcase lake ambalo ndio ofisi,mlichukua na zile nyanya?

Weka ushahidi wa kiongozi mwingine zaidi yake aliyeongea siku za nyuma.
 
DP inazikwa na Mtikila.
Hakuwa na katibu, katibu mwenezi wala mhazini..sembuse muhuri wa chama

Huyo kiongozi mtakuwa lumumba mmemuweka baada ya kudaka briefcase lake ambalo ndio ofisi,mlichukua na zile nyanya?

Weka ushahidi wa kiongozi mwingine zaidi yake aliyeongea siku za nyuma.

mkuu uliangalia ch10
 
Ni kweli kuna mkono wa mtu, gari si ilikua inaendeshwa na dereva mwenye mikono? Kama unapingana na ripoti ya polisi peleka ya kwako basi.
 
Mtikila alivunjika 8 Ribs na alipata internal breeding na kusababisha damu kuingia kwenye njia ya hewa na kusababisha kifo chake mimi ni moja ya madaktari tuliokagua mwili wa rev. Mtikila ila alikua hana injuries zozote na tulivyoona kulikua hakuna mkono/mguu/kisigino wala korodani la mtu cause kama mkono wa mtu ni kuwa alikua assassinated but the deceased body passed all tests including gunshot, and whether he was hanged but he passed all test. Ninaomba uni pm number yako unipe your thoughts .
 
Back
Top Bottom