Mch. Daniel Mgogo: Kikokotoo cha pensheni ni wizi na utapeli

Ni wizi mtupu.
 
Janja janja hii.....
 
Ana maslahi binafsi kwenye Hilo anawinda fungu la kumi

Kuwa wakipewa fungu kubwa na yeye fungu la kumi ataambulia kubwa
 
Serikali inaibiwa wazee wastaafu alafu mjinga mmoja anaweza niamboa niombee sirkali labda niombee ianguke!!
Unamkopa mstaafu kinguvu alafu unasema eti unamuwekea ela zake!! Nchi hii Kwamba eti tunalo "bunge" ni jambo aibu saaana... Labda wanakutana kushindana mavazi na kumsifia Maza kwakuupiga mwingi nawao kupigana mwingii humo.
 
Alifanya kazi miaka mingapi Kabla ya kustaafu tuanzie hapo nikupigie hesabu uelewe
 
Duniani kote haiko hivyo Sasa hivi hakuna nchi hata moja yenye huo mfumo wa kulipa zote za pension kwa mkupuo Kwa mwajiriwa Mstaafu haipo duniani
Wacha kiherehere wewe unaijua Dunia yoote? Tukikuletea nchi watu wanalipwa mabilioni utasemaje? Kwanza yote manaka Nini maana bado hatazamani ilikuwa unalipwa Kila miezi mitatu
 
Wacha kiherehere wewe unaijua Dunia yoote? Tukikuletea nchi watu wanalipwa mabilioni utasemaje? Kwanza yote manaka Nini maana bado hatazamani ilikuwa unalipwa Kila miezi mitatu
Weka tu usiwe na shida weka hoja hujibiwa Kwa hoja
 
sijawahi mumwona mtu huyu akihuburi neno 🐒

ni life tips tu, kweli ni mchungaji huyu 🐒
 
Nafikiri sasa ifike mahali kila mfanyakazi wakati anaanza ajira yake ya kwanza achague mwenyewe wakati anajiunga na hii mifuko kuwa anataka malipo yake yawe kwa mfumo gani kati ya pensheni au mkupuo. Hii habari ya serikali kungángánia pesa za watu waliotumikia nchi hii kwa jasho na damu tena kwa uadilifu mkubwa eti kwa kisingizio kuwa watasumbua watoto na wajukuu zao ni kuwafanya hao wastaafu kuwa hawana akili. Na kama hawana akili wamefanyaje kazi serikali na sekta binafsi kwa miaka yote mpaka wakastaafu?

Vipi hao wabunge wanaopewa pesa yao yote kwa mkupuo baada ya miaka mitano mbona wao hatuwaoni wakisumbua watoto na wajukuu zao? Au wao pekee ndio wanaakili ya kutunza na kuwekeza pesa kuliko wastaafu? Hata kama mstaafu akitumbua pesa zake zote na akasumbua watoto na wajukuu zake hiyo inaihusu nini serikali hayo si mambo binafsi kati ya babu/baba na watoto/wajukuu.

Kwa kifupi kikokotoo ni ujanja ujanja fulani tu. Walau basi huyu mstaafu angepewa asilimia 75% kwa mkupuo halafu hiyo 25% iliyobaki ndio iwe analipwa kidogo kidogo kama pensheni. Hao wachache wa kutumbua pesa yote wapo tu kila ofisi hawakosekani lakini wasizuie walio wengi wenye maono ambao wangepewa pesa zao kwa mkupuo wengewekeza na kula uzee wao kwa raha baada ya kustaafu.
 
Ubunge sio kazi ya ajira pensionable Haina pension Ina terminal benefit tu mikataba wa miaka mitano ikiisha

Kazi za mikataba ambazo sio pensionable Zina utaratibu wake kama mtu anataka kuwa pensionable mfano kajiajori au mama nitilie nk yeye mwenyewe aweza Sema mimi nitakuwa nawakilisha michango yangu mwenyewe Kila mwezi mifuko ya pension ili nikifikia umri wa kustaafu nilipwe pension ya Kila mwezi. Na wako kibao hao waluojiajiri wenyewe hupeleka michango Yao NSSF kuogopa uzee ukifika hawezi endelea kujiajiri asihe sumbua watoto,ndugu au marafiki

Tofautisha kazi ya mikataba ya kulipwa terminal benefits tu bila pension na kazi za ajira ambayo mtu ni pensionable

Mbunge akilipwa chake ndio imetoka hiyo na wengi wengine huondoka mikono mitupu sababu pesa karibu yote huishia kulipa madeni waliyokopa ya Magari ,ujenzi wa nyumba nk waliyokopa wakiwa wabunge

Kuhusu wabunge na mawaziri ambazo pamoja na kulipwa vizuri baadaye husumbua wako wengi tu Mbona Kuna mmoja Kule ukerewe alikuwa mbunge na waziri aliishia kuwa na maisha magumu sana akawa ili ale anavua samaki na ndoana ziwani siku ziende akisumbua sana watoto na ndugu

Kuna mwingine alikuwa mbunge na waziri Toka Tabora aliishia maisha mabaya sana akitemvea Kwa miguu Hana hata nauli ya daladala
 
Huo ni ujinga kwanini fedha ya kwako upangiwe matumizi na mwingine.mbona wabunge wapo tu lkn waliishachukua chai?
 
sijawahi mumwona mtu huyu akihuburi neno 🐒

ni life tips tu, kweli ni mchungaji huyu 🐒
Wewe hujielewi umezoea kuhubiriwa habari za mashetani na kuligwa!!
Wachungaji wanapaswa kufundisha namna Bora ya kuiishi ili kumpendeza Mungu sio kukariri tuu vifungu vya maandiko!
Utachelewa sana kijana
 
Wewe hujielewi umezoea kuhubiriwa habari za mashetani na kuligwa!!
Wachungaji wanapaswa kufundisha namna Bora ya kuiishi ili kumpendeza Mungu sio kukariri tuu vifungu vya maandiko!
Utachelewa sana kijana

relax bas

nadhani huyo ni muelimishaji wa stadi za maisha sio muhubiri wa neno 🐒
 
Pension ya mwezi ni kumsaidia Mstaafu walau asiumie sana kipato cha mwezi kisiwe mbali sana na alichokuwa Akipata akiwa kazini

Mfano akipewa mkupuo asilimia 75 na ya mwezi asilimia 25 unajua maana yake ? Ni kuwa mfano mshahara wake milioni moja Kwa mwezi akipewa mkupuo asilimia 75 Ina maana yaani 750,000 Ina maana pensioni yake Kwa mwezi maisha yake yote itakuwa 250,000 Kwa mwezi maisha yake yote ambayo Iko chini hata kwenye kima Cha chini ataishi maisha magumu sana mbeleni huko

Lakini mfano akipewa mkupuo asilimia 25 ambayo ni Sasa na 250,000 atakacholipwa Kila mwezi pension yake itakuwa sawa na asilimia 75 ambayo ni sawa na 750,000 Kila mwezi maisha yake yote ambayo Kwa Sasa ni sawa na mshahara wa kuanzia wa mtu mwenye digrii Kabla kukatwa Makato.Kwa 750,000 anakuwa na tofauti ndogo na mshahara alikuwa Akipata ofisini Kabla kustaafu kuliko angelipwa pension ya Kila mwezi ya 250,000 Kwa mwezi maisha yake yote Hadi afe

Pension Iko kama bima inajaribu kukurudisha kwenye Hali ulikuwa nayo ya kipato cha kila mwezi kama ulivyokuwa ofisi ila Kwa kuwa uko tu nyumbani hawawezi kulipa sawa na aliye ofisini
 

Acha ujinga wewe. Hata mshahara basi sio wako maana mwajiri ndiye anakulipa.
 
Kuja kwa kikokotoo ni matokeo ya CCM kukosa hela ya kampeni 2015 ambapo walikopa hela za mifuko ya jamii bila security yoyote ile... Alipoingia JPM Ikabidi atafute namna ya kuwalipa wastaafu cha kwanza akaunganisha mifuko yote ya mafao maana kabla ilikuwa imegawayika akaleta NSSF NA PSSSF pia akabidili kikokotoo kutoka kupewa asilimia 75% ya mafao mpaka kupewa asilimia 25%


Kwa hiyo hili la kikokotoo mtapiga sana kelele haliwezi badilika leo hakuna hela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…