Hata hatujafika mbali sana, tayari wanaanza kusema waziwazi wenyewe mbinu haramu na za wizi wa kura walizotumia kushinda uchaguzi huu.
Katika video hii inayomwonesha mbunge mpya wa CCM - Jimbo la Kawe - DSM, Mch. Josephat Gwajima kuanzia dakika ya 8:50 ukitazama na kumsikiliza bila kujua ana kwa kujua asemacho, anaeleza jinsi jina la Rais John P. Magufuli lilivyotumika kuwapatia kura bila kutegemea watu (voters) kupiga kura.
Na hiki ndicho kinacholakamikiwa na vyama shindani vilivyopambana na CCM ya Magufuli katika uchaguzi ulioisha wiki juzi...
Wanasema kuwa huu haukuwa uchaguzi bali maigizo tu ya uchaguzi kwa sababu washindi walikuwa tayari wameshaandaliwa akiwemo Gwajima mwenyewe ambaye kwa kinywa chake anathibitisha hili.
Hakika kumbe ni kweli kabisa kuwa, MDOMO ULIPONZA KICHWA!
Hii maana yake ni kusema kuwa, kwa kuwatumia watu wao, walienda kwa wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wakurugenzi wa halmashauri za wilaya/miji/manispaa/majiji ambao ni wateule wa Rais Magufuli na kutoa amri ya utekelezaji tu kilichokwisha kuamuliwa;
Rejea kauli hizi za CCM;
"....nimekuteua mimi uwe DED, nimekupa mshahara mzuri mnono, nyumba nzuri na gari nzuri halafu sasa uende umtangaze mpinzani ameshinda uchaguzi ....", Rais John Pombe Magufuli (CCM)
".... hata kama mtapiga kura nyie, lakini CCM ndiyo itakayounda serikali...", Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan (CCM)
".... siyo kwamba 'Mungu akipenda tutashinda uchaguzi', HAPANA. Sisi tunasema Mungu apende ama asipende, CCM ni LAZIMA ishinde uchaguzi huu...", Hayati Marehemu Mary Edward..
Hivi ndivyo jina la Rais John Pombe Magufuli lilivyotumika kuleta ushindi. Je, unahitaji wapiga kura hapa kukupigia kura?
Your browser is not able to display this video.
Kinachonipa shida na taabu mimi zaidi ni ushiriki wa Mchungaji huyu, mtumishi wa Mungu kwenye uharamia na unyang'anyi huu wa haki za wananchi mchana kweupe bila yeye kuukemea na kuukataa.
Je, mchungaji huyu anaweza kusimama madhabahuni na kuukuemea uovu na unyang'anyaji wowote iwapo yeye mwenyewe akiwa mshiriki mshiriki na sehemu ya unyang'anyi huo?
I am afraid to say this, that he might have a bad ending like his counterpart the late Rev. Getrude Lwakatare!
Lugha nyepesi imetumika na Askofu, Jina la Magufuli lilitosha kbs. Hii ni kutokana na utendaji thabiti wenye matokeo dhahiri yanayoonekana ambayo TL alikaza shingo kuyaita maendeleo ya VITU!
Sasa waliogombea kwa kutaja TL imekula kwao, lakini waliogombea kwa kumtaja mchapakazi Magu imelipa hivyo kampeni zilikuwa nyepesi sana.
Ukitaka kuelewa kuwa uko nje ya muktadha, sikiliza hotuba zote kuanzia Rais wako Pombe, spika wako Ndugai na huyu mchungaji utagundua iko shida.
Mathalani, Gwajima anawafanyia "mockery" wazanzibari zaidi 90% walio kwenye msiba mkuu wa demokrasia ta nchi yao...
Anasema Dr Mwinyi Rais wa Zanzibar kuwa ni gwiji kwelikweli wa siasa kwa sababu amefanikiwa "...kuwageuza kichwa chini, miguu juu wapinzani wake."
Kama wewe ni msikilizaji mzuri na unayeweza kumsoma na kumwelewa mzungumzaji, tazama "body language" ya Mwinyi mara baada ya kauli ile ya Gwajima.
Dr Mwinyi hakuifurahia na ana sababu ya kutofurahia.
Ni kwa sababu mpaka sasa na pengine mpaka kesho, Dr Mwinyi anafanya kila juhudi kuwaunganisha na kuleta mwafaka miongoni mwa Wazanzibari baada ya majeraha ya uchaguzi wa wiki juzi.
Sasa anapotokea mtu "mjinga" tena ndani ya platform ya bunge na mbele yake Rais anatoa matamshi kama yale, bila shaka yanakuwa yanarudisha nyuma jitihada hizo na kutonesha majeraha ya Wazanzubari.
Kwa hiyo, kila kitu kiko inside the context. Wewe ndiye uliye nje ya muktadha. Rudi ndani tafadhali.
9Enyi wanyama wote wakali,
nanyi wanyama wote wa mwituni,
njoni muwatafune watu wangu.
10Maana viongozi wao wote ni vipofu;
wote hawana akili yoyote.
Wote ni kama mbwa bubu wasiobweka,
hulala tu na kuota ndoto,
hupenda sana kusinzia!
11Hao ni kama mbwa wenye uchu sana,
wala hawawezi kamwe kutoshelezwa.
Wachungaji hao hawana akili yoyote;
kila mmoja hutafuta faida yake mwenyewe.
12Huambiana, “Njoni, twende kutafuta divai;
njoni tunywe tushibe pombe!
Kesho itakuwa kama leo,
tena itakuwa sikukuu kubwa zaidi.”