Mch. Josephat Gwajima: Maeneo mengine hatukuhitaji kupiga kura ili kushinda bali kutaja jina la John P. Magufuli tu, kura zilipatikana

Mch. Josephat Gwajima: Maeneo mengine hatukuhitaji kupiga kura ili kushinda bali kutaja jina la John P. Magufuli tu, kura zilipatikana

Wewe ni msemaji wa Gwajima?
Alimaanisha kupiga kampeni ila ulimi ukateleza.

Kama kawaida Bavicha mtakomaa na mada za kijinga kama hivi weeee! Hadi ikifima tarehe 01/10/2025 ndio mnaanza kuulizia mambo ya tume huru.
 
NEC wanataka kusumbua WATU Tena na uchaguzi wa wale madiwani waliokufa.
Mngewapa tu CCM. Msipotezee watu muda.
 
Hilo siyo kosa la Rashidi. Kosa linaanza pale alipoanza kuitwa mchungaji.
 
ISAYA 56:

9Enyi wanyama wote wakali,
nanyi wanyama wote wa mwituni,
njoni muwatafune watu wangu.
10Maana viongozi wao wote ni vipofu;
wote hawana akili yoyote.
Wote ni kama mbwa bubu wasiobweka,
hulala tu na kuota ndoto,
hupenda sana kusinzia!
11Hao ni kama mbwa wenye uchu sana,
wala hawawezi kamwe kutoshelezwa.
Wachungaji hao hawana akili yoyote;
kila mmoja hutafuta faida yake mwenyewe.
12Huambiana, “Njoni, twende kutafuta divai;
njoni tunywe tushibe pombe!
Kesho itakuwa kama leo,
tena itakuwa sikukuu kubwa zaidi.”
Haswaa...
 
Yuko sahihi; mfano kwa Wagogo Dodoma na Ruvuma huko bado wao wanajuwa Tanzania iko kwenye mfumo wa chama kimoja😀😀😀😀😀 Hawana habari Kuna chama kinaitwa Chadema au Kuna mgombea aliitwa Tundu Lissu😜😜😜😜
 
ISAYA 56:

9Enyi wanyama wote wakali,
nanyi wanyama wote wa mwituni,
njoni muwatafune watu wangu.
10Maana viongozi wao wote ni vipofu;
wote hawana akili yoyote.
Wote ni kama mbwa bubu wasiobweka,
hulala tu na kuota ndoto,
hupenda sana kusinzia!
Gwajima somahiyooooo umeipata?
 
Ukijaribu kufuatilia utagundua hata utekaji wa baadhi ya watu akiwemo Dr Ulimboka jina lake limeonekana , fungua ubongo utaelewa
Maskini siku hizi unatia huruma. Ila nilikuonya ila una kichwa cha kutoelewa mapema mpaka yakukute. Unakumbuka sredi zako uchwara ‘Lissu aifuta CCM......’ unalo!
 
Nimesoma nimegundua mambo mawili:

1. Unamtambua Askofu Gwajima kuwa Mbunge halali wa Jimbo la Kawe & JPM kama Rais halali wa JMT

2. Maelezo yako yanapingana kabisa na kilichosemwa, na kila mtu anajua kuwa inajulikana kwamba wewe unajua vizuri kuwa umejua ulichoandika sicho tunachojua unajua; na sasa unajua vyema kama nani anajua kuwa nani mwongo kati yako na Askofu Gwijama.
 
Ujinga umetawala awamu hii wacha tuone mwisho wao utakuwaje.
 
Mmh, mmh, jamani muwe waelewa! Mchungaji Gwajima hakumaanisha hivyo mlivyomwelewa ninyi majameni Watz kwa kupindisha mambo!

Alimaanisha umaarufu wa Rais JPM na mapenzi ya wananchi yanayotokana na kazi nzuri aliyofanya ktk miaka 5 iliyopita iliwasaidia na kuwarahisishia wagombea ubunge (na madiwani) ktk kampeni zao.

Na jambo hili ni kweli; binafsi nimeshuhudia. Watu tuliwachagua wawakilishi hawa (walio wengi) kama kumlipa fadhira na shukrani na kumheshi u na kumtia moyo JPM na hata kutekeleza wito au ombi lake kwetu watanzania aliokuwa akisikika mara kadhaa akisema,

Tafadhali nileteeni Mtu huyu! Tafadhali msinichanganyie ..." nk, nk.

Kwa kweli "Jina" la JPM liliwabeba watu wengi, labda wale waliokuwa wamekinaiwa kabisa kama yule Mhuni wa Nkasi Kaskazini. Nasikia ati kuna mpango anaweza kuteuliwa viti maalum vya Rais; wasithubuti. JPM atakuwa amejivunjia heshima mno kwa wananchi. Hafai hata kidogo.

Tunatembelea Nchi jirani za wenzetu zinazotuzunguka; wanatustaajabia sana kwa kuwa na Rais kama JPM; wanatamani angekuwa kwao ili "anyooshe mambo". Wanatuonea gere Watz.

Kwa kweli tunamshukuru Mungu kwa kutupa JPM.

Anyway, Uchaguzi umekwisha ktk hali ya amani; yaliyotokea mabaya wakati wa mchakato mzima wa Uchaguzi yalitokea. Ni bahati mbaya; tusameheane. Nchi hii ni yetu sote, hatuna kwingine kwa kwenda. Tusigombanie fito.

Siasa za vyama vingi tuendelee kuijenga na kuiimarisha taratibu kwani inatakiwa kulelewa na kukua kama mtoto mchanga. Tusikurupuke tukataka tufanye na kuwa ktk viwango vya siasa na demokrasia za mataifa ya Ulaya magharibi na Marekani. Sisi baado sana! Ni "nyumba ya udongo" sisi

MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU MBARIKI JPM
MUNGU IBARIKI AFRIKA
 
Lugha nyepesi imetumika na Askofu, Jina la Magufuli lilitosha kbs....hii ni kutokana na utendaji thabiti wenye matokeo dhahiri yanayoonekana ambayo TL alikaza shingo kuyaita maendeleo ya VITU...!

Sasa waliogombea kwa kutaja TL imekula kwao , Lkn waliogombea kwa kumtaja mchapakazi Magu imelipa hivyo kampeni zilikuwa nyepesi sana.

Hivi kipi kigumu hapo kuelewa!!
Nileteeni gwajima
Nileteeni gwajimaaa
Nileteeeeni gwajima
Naskia watu wakaanza kuingia na vibegi
 
Back
Top Bottom